Alikiba: Sina bifu na Diamond lakini alinikosea na nikaumizwa na nilisha samehe

Msanii Alikiba ameamua kufungaka na kuweka waZi kili kinacho hitwa tofauti au bifu kati yake na Msanii Diamond!Kwanza lazima tukubaliane kuwa ALikiba ni mmoja wa Wasanii wasio penda maneno na malumbano na wasanii wenzie ndio maana hukaa kimya. Kwanza Alikiba alisema hana bifu na diamond na hana sababu ya kuwa na bifu nae japo yanayo ongelewa yana muumiza sana na aliamua kuondokana na hayo yote busara ya haraka ilikuwa kukaa kimya.

Aliendelea kusema aliumizwa sana aliposikia kuwa amefuta mistari ya diamond kwenye wimbo wa Single boy ambao aliimba na lady jaydee na hakuimba kabisa na diamond na hata producer aliye record wimbo huo alithibitisha. Aliendelea kusema kuwa aliumizwa sana na uongo huo kuhusu yeye na hakupenda kuuongelea sana kwa sababu ange onekana anatafuta kick wakati hakuKuwa na kitu kama hicho.

Pia Alikiba aliamua kusema kuwa aliumizwa sana na kitendo cha Diamond kufuta mistari yake kwenye wimbo wa Lala salama maana Diamond hakumwambia kwanini kafanya hivyo na hadi leo hakuwai kumwambia. Alisema hilo swala amechukulia kama na Kitendo cha mtu kuomba mtihani wako aangalizie alaf baadae ana kurudishia mtihani wako na kusema sitaki majibu yako au ana yafuta yote alaf unategemea atajisikiaje? na alisema yeye alisha samehe lakini Diamond alimkosea na hadi leo hawakuwai kukutana.

Ameweka wazi kuwa aliamua kuwa kimya ili watu waongee lakini hana tatizo na Diamond. Katika hili sikuona sababu ya Diamond kutomwambia Alikiba kuwa wimbo naufanya upya na nimetoa mistari yako maana sikuipenda na nimeamua kuimba mwenyewe.

Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umesahau Kiba,uliumia tena zaidi uliposikia Dai ametoka na Lulu. Mapenzi hatari sana.

    ReplyDelete
  2. Namkubali kibasana anaustaarabu simtu wa mjungu.baki hivyohvyo usiwe na mbwembwe fanyayako kimyakimya mradi yanakuendea kiba

    ReplyDelete
  3. nakupenda we jamaa pamoja na mziki wako hatari huna ulimbukeni mstaaraba hujawai kuvua nguo stejin wala hujawai kuvaa sketi

    ReplyDelete
  4. Penda mimi Ali Kiba wewe. ... Huna uswahili km wa domo big up

    ReplyDelete
  5. big up sana ikufikie ally k' yaani kiukweli sijaona msanii mwenye busara kama wewe kiba,hujisikii mtomto wa watu, endelea hivohivo malipo yako utayakuwa achana ana huyo domo zege pambafuu zake.

    ReplyDelete
  6. kukaa kimya ni jibu la mjinga bado tunakupenda sana huyo domo tunajua kuwa mwisho wake utakuwa wa aibu.

    ReplyDelete
  7. nadhani mamaako alikulea vyema kabisa hongera yake tumbo liliokuzaa

    ReplyDelete
  8. All uko juu sana kaka penda sana weye.

    ReplyDelete
  9. Kwanini umuombee dai dua mbaya? Kwani kuna ubaya gani yeye kufuta mistari? Dua la kuku alimpati mwewe. Poleni sana na wivu wenu watu wanaendelea kupeta. Wanafiki wakubwa.

    ReplyDelete
  10. Dada we mdau hapo juu umeumizwa ulipoona watu wanamsifia aly kwa tabia yake nzuri, wewe ndo mwenye wivu, fikta ndogo

    ReplyDelete
  11. ally kiba wewe ni mstaraabu sana...kweli kuna wakati niliposikia katika media kwamba kuna bif kati yako na Naseeb niliogopa. ila nimegundua pia hata Naseeb hutumia busara yakivumishwa maneno. kwa hili sina uhakika ila nasema vijana hawa sio wasema ovyo, ila ukinambia nani namkuli zaidi kwa kuwa yuko soooo HUMBLE ntasema ALLY KIBA MEEEEEEEEEEEN!!! big up mdogoangu Mungu akupe busara na mafanikio katika game. uko poa sana.

    ReplyDelete
  12. Mimi ni wa gospel lakini namkubali Ali sana,hana makuu kabisa,ana nidhamu.Mungu ambariki.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad