Arnold Kayanda 'Siku Hizi Vipindi vya Jioni Redioni Vimepungua Utamu, Huwezi Linganisha Tulivyokuwa Mimi na G-Habash

"Huyu ni ndugu yangu Captain Gardner G Habash. Juzi kati tulikutana kwenye radio mpya mjini , walituomba maoni mawili matatu kuboresha. Nimemkumbuka! Gardner nilipojiunga Clouds FM yeye alishakuwa maarufu sana. Tofauti na watu maarufu wa wakati huo, alinipa nafasi sana na hata akafikia kuwa ananifanya Co-captain mara moja moja. Siku moja aliniambia, "nataka kuondoka nitakuachia 'Kipindi'". Alipoondoka hawakunipa 'kipindi'. Baada ya miezi kadhaa waliniita 'niokoe Jahazi'. Watu wanasema nilivaa vizuri viatu vya G. Habash (Sidhani kama nilimfikia hata nusu). Ingawa kila mtu ana mtazamo wake lakini pengine utaniunga mkono kuwa siku hizi vipindi vingi vya jioni vimepungua utamu. Hakuna tena uchambuzi wa kina wa masuala nyeti unaofanyika kiburudani, hakuna tena Maelezo juu ya muziki yaliyokuwa matamu kuliko muziki wenyewe unaozungumziwa. I publicly #ThankYou Captain Gardner G Habash" 
Anold Kayanda

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu anold kwa matamshi haya aliacha kazi Clouds?
    Kama bado basi nasubiri movie part 2 sio mida.

    ReplyDelete
  2. Keshatendwa uyo na clouds

    ReplyDelete
  3. kweli kabisa watu wanakosa ubunifu,mabifu tuuuuu,na kuja kulete habari zao za nyumbani redioni,na bata zao.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad