Mshiriki wa Bongo Star Search, Wababa aliwatuhumu Diamond Platinumz na Nay wa Mitego kwa wizi wa kazi zake za muziki kwa wakati tofauti.
Akiongea na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm,inayoongozwa na Jabir Saleh Wababa alidai kuwa Diamond Platinumz alimuibia wimbo wake wa Kitorondo kwa kuurudia bila kumwambia, wimbo ambao anadai aliuimba miaka minne iyopita akiwa na Dogo Aslay wakati huo yeye anatumia jina la Nurdi.
Alidai baada ya wimbo wa Diamond kuvuja ukiwa na jina la Kitorondo yeye alipigiwa simu na watu wakamwambia na akausikiliza akaona ni kweli amefanya kile alichofanya yeye miaka mingi iliyopita. Hata hivyo anadai wimbo huo Diamond ameubadilisha baadae na kuuita Kidogo Kidogo huku akibadilisha ujumbe(Wimbo mpya wa Diamond).
“Mimi nilikuwa naongelea msichana mdogo, lakini yeye ameongelea mapenzi lakini melodies, mtiririko ni ule ule bado.” Alisema Wababa.
Hata hivyo Wababa alidai kuwa hana cha kufanya kwa upande huo na kwamba anaona kama Diamond anarudi nyuma kwa kuwa yeye anamchukulia kama mfano wa kuigwa kwa hatua alizopiga, lakini kurudi kuchukua wimbo wa msanii mchanga aliofanya miaka minne iliyopita ni kujirudisha nyuma.
Katika hatua nyingine, Wababa alimrushia lawama Nay wa Mitego ambaye anadai amemshirikisha kwenye wimbo wake alioufanya Mazoo Records lakini Nay alimzunguka na kurudi kwa producer Mazoo akidai anataka aununue wimbo huo na ataulipia shilingi milioni moja.
“Watu wa pale ndio walinishtua kuwa aisee njoo kwa sababu kuna kitu kinaendelea hapa Nay anataka kuchukua wimbo wako aulipie milioni moja.” Ameeleza Wababa.
Anasema alimpigia simu Mazoo lakini muda huo alikuwa na Nay wa Mitego hivyo hakupokea na yeye hakuweza kwenda. Lakini tangu kipindi hicho akimpigia simu Nay wa Mitego hapokei na akipokea anamwambia yuko busy amtafute baadae.
“Mimi nataka tu Watanzania wafahamu kwa sababu akija kutoa wimbo halafu mimi nikalalamika, ndio yataibuka yale yaliozoleka pale msanii anapoibiwa na kudai haki yake anaambiwa anatafuta kick….”
Bongo Dot Home ilimtafuta Nay wa Mitego ambaye alieleza kwa upande wake nini kilitokea na mpango uko vipi kuhusu tuhuma hizo.
“Sijui niongee nini kuhusu hii issue…mimi nimeisikia. Lakini mimi napenda beat nzuri, mimi sijataka ile beat. Lakini kilichofanyika ni kwamba producer ametaka kunipa mdundo wa design ile lakini sielewi ni kwa nini tena maneno yamekuja kwamba mimi nimetaka kuilipia ile beat. No, mimi nilisema napenda ule mdundo wa design ile kwa gharama yeyote naweza nikaulipia lakini sio kama nimetaka mdundo wa dogo..no.
“Ngoma ya dogo nzuri, mimi mwenyewe nimependa the way nilivyoimba lakini sio kama nitake ngoma yake au beat yake hapana ntakuwa nakosea, nitakuwa nakosea sana. Lakini mimi nilichoongea ni tofauti na hicho labda wale wameninukuu vibaya. Mwisho wa siku naweza kusema mimi siwezi…kwanza muziki wangu watu wanaujua uko tofauti sana. Hiyo ngoma yenyewe ukiisikia iko tofauti sana, na mimi nimetaka changes kwenye muziki wangu.. nilimwambia producer nataka beat ya design hii ambayo inaweza kuwa kali zaidi ya hii na mimi nikailipia hela yoyote unayoitaka. Kwa hiyo mwisho wa siku sijui nini kiliendelea hapo katikati.
“Si kweli…ni nyimbo nzuri kweli mimi niliipenda niliisifia na ndio maana nilikuwa na nguvu ya kuweza kuifanya naweza kusema kwa asilimia mia moja. Mimi sijafanya featuring tangu mwaka jana. Kwa mwaka huu nilifanya featuring mbili tu, nilifanya ya kwanza ya Kala Jeremiah na hii ni ya pili tena baada ya kutumiwa demo nikaoni ni nzuri sana. Niliifanya kwa nguvu kwa sababu niliona ni nyimbo nzuri ambayo hata mimi mwenyewe watu wanaweza kuendelea kusema ‘okay mwana amefanya collabo nzuri’. Siwezi kuchukua nyimbo yake yeye, nyimbo yake yeye.
“Mimi anitafute, siku mbili tatu hizi nilikuwa busy na mambo yangu. Nilikuwa namalizia nyumbani kwangu huku na kule vitu vingi shows na vitu vingine. Anitafute tutaongea. Mimi naweza kusema hivi ni mdogo wangu, hakuna ambacho kitaharibika lakini sidhani kama itaweza kufikia hatua tukagombana mimi nay eye. Labda yeye alininukuu vibaya."
Msikilize hapa:
mjini ni shida wtu kwa kubadilisha maneno
ReplyDeleteMakubwa aseee
ReplyDelete