Baada ya kuchapwa nne bila, Ureno yaendelea kumeguka vipande vipande

Beki wa pembeni wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, Fabio Coentrao ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno ambacho kwa sasa kipo nchini Brazil kikishiriki fainali za kombe la dunia.

Coentrao, ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno, baada ya kuumia goti akiwa kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa kundi la saba ambapo A Selecção walikubali kupoteza mbele ya Ujerumani kwa mabao manne.

Coentrao, aliondolewa kabisa kwenye kikosi cha Ureno baada ya kufanyia vipimo katika mguu wake wa kulia na kubainika aliumia vibaya, hivyo itamlazimu kukaa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa kabla ya kurejea tena.

Kuumia kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 26, kunakuwa pigo la pili kwa timu ya taifa ya Ureno ambayo itamkosa beki wa kati Képler Laveran Lima Ferreira Pepe, aliyeonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Adhabu hiyo kwa Pepe inamfanya aikose michezo miwiwli ya hatua ya makundi iliyosalia, hivyo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno Paul Bento, atalazimika kutumia ubunifu kwa kumpanga beki mbadala wakati wa mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Marekani utakaochezwa June 22.

Wachezaji wengine ambao ni majeruhi katika kambi ya timu ya taifa ya Ureno, ni mshambuliaji Hugo Almeida anayesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja pamoja na mlinda mlango Rui Patricio anayesumbuliwa na maumivu ya paja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad