Baada ya Kudondoka Kutoka Kwenye Gari na Kufariki Maiti yakaa eneo la ajali saa 21

MWILI wa Idd Shamba aliyefariki dunia kwa ajali ya barabarabi katika Kijiji cha Engaruka wilayani hapa, imekaa barabarani kwa zaidi ya saa 21 ikisubiri polisi na daktari kufika eneo la tukio kwa ajli ya kupima ajali hiyo na kuufanyia uchunguzi mwili huo kabla kwenda kuzikwa.

Polisi walifika eneo la tukio majira ya saa saba mchana ikiwa ni saa 18 tangu kutokea kwa ajali hiyo ambapo baada ya kumaliza kazi ya kukagua na kupima eneo la ajali, mwili huo ulihamishiwa chini ya mti kuukinga na jua usiharibike wakati wakisubiri daktari kuja kuufanyia uchunguzi.

Tanzania Daima ilishuhudia wananchi na viongozi wa Kata ya Engaruka wakiulinda mwili huo wakati akisubiriwa daktari kutoka Mto wa Mbu ambaye naye alifika eneo la tukio majira ya saa 10 jioni.

Ajali hiyo ilitokea Juni 12 mwaka huu baada ya Shamba kudondoka kutoka kwenye gari la mizigo aina ya Toyota DCM, lenye namba za usajili T 995 AMB lililokuwa likitokea mnadani Engaruka kwenda Kijiji cha Selela.

Diwani wa kata hiyo, Pashet Sengerwan (CCM), alisema kuwa mwili huo ulifanyiwa uchunguzi kwenye eneo la ajali kisha kuzikwa Juni 13, majira ya saa 11 jioni kwenye makaburi ya kijijini hapo bila kuwasubiri ndugu zake waliokuwa wakitokea Singida.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, alisema tayari wameshamhoji mmiliki wa gari hilo, Sauli Kitomari huku wakiendelea na juhudi za kumtafuta dereva wa gari hilo ambaye alitoroka mara baada ya kutokea ajali hiyo.

Alisema kuchelewa kwa polisi kufika eneo la tukio, kulitokana na kukosekana kwa kituo cha polisi kwenye eneo la Engaruka ambalo pia lina tatizo la mawasiliano ya simu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moduli, Dowika Kasunga, alisema hali hiyo ilisababishwa na tatizo la mawasiliano na mamlaka husika kwani katika Kata ya Engaruka ili upige simu, lazima uende umbali mrefu kutafuta mawasiliano hayo.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ooh! Wow! Such a sad sad story. What a n awful way to die jamani. Mwenyezi mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi na pole sana wafiwa mwenyezi mungu awatie nguvu na moyo wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu. Mwe!!!

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli imenisikitisha sana. How would this happen. Kweli Mungu aiweke Roho ya Marehemu mahali pema Peponi. It's so sad. Hii ni aina ya matendo mengine ambayo ni so disgraceful wanafanyiwa raia wa Tanzania wakati wale viongozi wamekaa pale juu wanaendelea na corruption zao. Kwa kweli inabidi tufungue macho kwani huu uozo utaendelea mpaka lini bila ya watu kuwajibika.....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Disgraceful endeed yaani hii nchi sijui itaisha lini majanga wananchi wanateseka mpaka wakiwa wamekufa oh mola tusaidie viongozi wanaishi sooo large its disgusting walah

      Delete
  3. Dereva wote wajitambue wawapo barabarani.....maana wanavyoendesha gari utazania wamepakia mizigo tuu.....

    ReplyDelete
  4. mwenyezi mungu pumzisha roho ya marehemu pema peponi ila serikali yetu iangalie madhaifu yake sio haki kabisa masaa 21maiti ndio inafanyiwa uchunguzi Allah awape nguvu na faraja wafiwa inaumahebu fikiri angekua ndugu yako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad