Baada ya Mambo Kuwa Mazito GWAJIMA Ajitosa Kumwokoa Mume wa FLORA MBASHA

Wakati  mume wa mwimba Injili Bongo,  Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiachiwa huru kwa dhamana kufuatia kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye, Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima ameibuka na kunena mazito kuhusiana na sakata hilo.

Mbasha aliachiwa kwa dhamana juzi akitokea Gereza la Keko, Dar baada ya kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juni 17, mwaka huu na kusomewa mashitaka mawili ya ubakaji ambayo hata hivyo, aliyakana.
ILIVYOKUWA KORTINI

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mheshimiwa Wilbeforce Luago siku hiyo ya Juni 17, alitoa hoja kwamba upande wa jamhuri hauna pingamizi hivyo dhamana ipo wazi.

Alisema mshitakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, mfanyakazi wa serikali na wa kutoka katika taasisi inayotambulika sanjari na shilingi milioni 5 kila mmoja. Mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo siku hiyo hadi hadi juzi alipotimiza, akaachiwa.
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo ambaye ni wakili wa serikali, Nassoro Katuga bila kuchelewa aliitaja kesi hiyo yenye namba CC/186/2004 ambapo rafiki wa Mbasha aliyejitambulisha kwa jina la George Mushi na baba wa mtuhumiwa aitwaye Mwahimu Juma ndiyo waliofanikisha dhamana hiyo. Kesi yake itatajwa tena Julai 17, 2014.
GWAJIMA SASA

Akizungumza na mwanahabari wetu juzi wakati Mbasha akiwa nje kwa dhamana, Mchungaji Gwajima alieleza namna ambavyo sakata hilo limeitikisa Injili nchini Tanzania kutokana na kuibuka kwa madai mengi likiwemo suala la Flora kusemekana amehamia nyumbani kwake kitu ambacho alikipinga.
Gwajima alisema anasikitika sana kuona ndoa ya Flora na Emmanuel Mbasha inatikisika akizingatia Flora ni muumini wake hivyo moja kwa moja ugomvi wao unaonekana kutia dosari mwenendo mzima wa uinjilishaji katika jamii.

“Naumizwa sana na sakata hili lakini hivi karibuni niliamua kuwaita ndugu wa pande zote mbili (Flora na Mbasha) nikazungumza nao kwa kirefu na tukamaliza tofauti zote lakini tatizo likabaki lile la kisheria zaidi (mashitaka ya ubakaji kwa Emmanuel),” alisema Gwajima ambaye makao makuu ya kanisa lake yapo Kawe jijini Dar.
AANDAA TAMKO ZITO

Mchungaji Gwajima alisema kutokana na sakata hilo kugusa Injili, ameandaa tamko zito ambalo atalitoa rasmi atakaporudi safari yake ambayo hakueleza anakokwenda.

“Hatuwezi kukaa kimya juu ya hili, nasafiri lakini nikirudi tu nitatoa tamko rasmi kwa kuwaalika waandishi wa habari,” alisema.

IBADANI JUMAPILI

Katika hatua nyingine, ndani ya ibada ya kanisa hilo iliyofanyika Jumapili iliyopita, Mchungaji Gwajima alitumia dakika kama 15 katika mahubiri yake kutupa kile kilichodaiwa kuwa ni jiwe gizani ambapo wengi waliamini ni kuhusiana na sakata hilo.

“Mimi siyo kama wale, sijibu hoja kama zile, mfano ukiwa unaoga halafu chizi akachukua nguo zako na ukamkimbiza nani ataonekana chizi? Tatizo la Watanzania ni kuwa wakisikia kitu kipya kinaanza kwao badala ya kukithamini wanakididimiza ili kisiendelee, lakini mimi siyo kama wao,” alisema.

Aliongeza: “Mimi kila mwaka naenda Japan na ninawa-lecture Wajapani ambao pia huja hapa kanisani zaidi ya 40 kila mwaka na mwaka huu watakuja Septemba, lakini Watanzania hawashtuki na kuja kujifunza juu ya ufufuo wa wafu wengi wao wanakalia kuandika stori kwenye magazeti lakini mimi siyo kama wale.”
AMEFUNGUKIA SAKATA LA MBASHA?

Ingawa Mchungaji Gwajima hakueleza moja kwa moja kuhusu tukio la Mbasha lakini maneno hayo yalitafsiriwa kwamba ni ya kujibu hoja zinazomhusisha yeye na tukio hilo.

Anaendelea:”Mimi nimehubiri nchi zaidi ya 53 duniani na nyingi za Ulaya na Marekani halafu mtu amekaa Magomeni miaka yote anatengeneza stori ya gazeti, unatarajia niijibu, mimi siyo kama wale nimetumwa na nina kazi natakiwa kuifanya duniani na siwezi kufa mpaka niimalize.”

“Inawezekana mlishawaangamiza wengi kabla ya mimi, kwa kuwatungia stori hizo za uongo lakini mimi siyo kama wale na mwezi huu wa nane ninaendelea na mkutano Iringa, waache waandike lakini mimi ni chombo kingine na siyo kama wale.”
DONGO GIZANI?

Baadhi ya waumini waliokuwa katika ibada hiyo, walibaki njia panda na katika giza nene ingawa wengi waliamini alitupa vijembe katika sakata la Mbasha haswa alipokuwa akisema, ‘mimi siyo kama wale’.


Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Gwajima mtoto wa mjini sana, big up uncle mpiga hela nzur,

    ReplyDelete
  2. Huyu mzee unafki umemjaa...na ipo siku Mungu atampiga kofi. Hauwezi tenganisha ndoa ya watu afu akaendelea kuhubiri

    ReplyDelete
  3. tapeli mkubwa wewe! Kama unafufua wafu mbona unatafuta wasiofahamika?! Endelea kuponya kwa nguvu za GIZA ndani ya mwamvuli wa roho mtakatifu.. Tapeli malaya mkubwa wewe Gwajima.

    ReplyDelete
  4. akamfufue babu yake na bib yake,au atufufulie kanumba kama kwel

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kabisaaaa atufufulie tunaowajua ili tuamini.utapeli mtupu

      Delete
  5. Huyo
    Emmanuel na mkewe ukweli wanaujua wenyewe. saivi anatajwa gwajima, mala
    lana ya babu kulola,, mala anatembea na kigogo. in a time like that no
    one dare to speak the truth.

    ReplyDelete
  6. Gwajima namuamini.........hawezi kutembea na flora....ni maneno ya wakosaji....aliyelikoroga atalinywa....emmanuel mbasha amelikoroga matokeo yake misukosuko inamsonga ajifikirie nini ambacho anapendelea kufanya cha ajabu aache yataisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kampeleka Uingereza kusoma,kamnunulia prado jipyaaaa,na mambo kesekede kamfanyia flora,Mbasha kulia Gwamaji niachie mke wangu,kosa la ubakaji likazuka,wewe umfanyie mambo yoote flora,freeee of charge?SIAMINI Acha nichume dhambi,sitakaa niamini,hotel huu Ni mwaka sasa unalipa bill,Mmmmhhh

      Delete
  7. ushauri wangu ni kuwa mzee gwajima mengi yamesemwa na watu ya uongo na ya ukweli,hivyo naomba wewe kama mchunguji simama na utete ndoa ya hawa ndugu zetu wasiachane maana wakiachana itakuwa na wewe umeshiriki maana cheo chako ni mchungaji mkuu katika kanisa hilo.

    ReplyDelete
  8. gwajima kama kweli we ni mchungaji jitahidi kwa njia zako zote uokoe hiyo ndoa aibu maana utakuwa umeshiriki katika hiyo ndoa ife

    ReplyDelete
  9. unaongea kwa nyodo eti mimi si kama wale, hela na misukule na ufree mason ndo unaotambia, eti huwezi kufa na unaendlelea kuhubiri, we mchezee mungu unafikiri ni wa mchezo ipo siku utaisha kama mshumaa na watu watashangaa, acha sheria ichukue mkondow wake wakati mnajua kabisa mmeshamuweka katika hali mbaya huyo mbasha leo kwa kuona mbasha yuko mahabusu ndo unaongea mbona mwanzo hukuongea chochote shame on you mungu huwa hamfichi mnafiki subiri 50 zako zinakuja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen,Mungu fanya kazi yako kwa wanafiki wanaodanganya watu kwa kupitia jina lako lipitalo kila Jina.

      Delete
  10. Wanapata utajiri kupitia demonic power hakuna Mungu hapo Ni ushetani mtupu

    ReplyDelete
  11. Kama Ni njia safi ya Mungu mtumishi Wa Mungu awezi vunja amri ya 6,simsemi gwamaji Nasema kwa watumishi Wooote kiujumla,amri nyingine inasema" usiabudu Miungu wengine lakini watumishi wanaojiita Ni watumishi Wa Mungu wananjia zao chini ya kapeti kuwaingizia pesa Kama mchanga Wa baharini.Demonic power.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad