BBC Waianika Vibaya Tanzania Tena!
10
June 20, 2014
Baada ya kufanikiwa kwenye pembe za ndovu, BBC wametukung'uta tena. Safari hii ni kwenye madini ya tanzanite. Wanadai tanzanite inachimbwa na watoto. Wameweka video ya "the gemstone mined by child labour". Huu utakuwa ni mkakati wa makaburu wa tanzaniteone ambao mara zote wameutangazia ulimwengu kuwa tanzanite yao pekee ndiyo halali maana haichimbwi na watoto. Hili ni pigo jingine kwa ndugu zetu wanaotegemea tanzanite kuendesha maisha yao
Tags
the point is hiyo ni kweli au uongo? kama nk uongo basi sawa wametuonea but kama ni kweli acha waitangazie dunia. ukifanikiwa kufika maeneo ya migodi kama una akili timamu hautatamani kuona mwanao huko watoto wanateseka sana sana kwa malipo madogo na udhalilishwaji mwingi. watutangaze watoto wetu wapone
ReplyDeletemsiniambie niwe mzalendo kwa gharama ya maisha ya watoto wasio na hatia.
kuambiwa ukweli sio kosa,kwa hiyo ulitakaje wewe udaku?
ReplyDeleteni kweli na ndio waache watoto wanadhalilishwa bana
ReplyDeletekama mamlaka husika za nchi mmelala usingizi mnasubili mishahara ya bure acheni BBC wafanye kazi nakushangaa udaku unalalamika nini..
ReplyDeletesio malipo madogo tu hata kulawitiwa watoto kupo sana,serikari iko bize na wasanii wa bongo movie na bongo flavor
ReplyDeleteTanzania zaidi ya tuijuavyo ndio hivi acha tuanikwe tu
ReplyDeleteiyo taznt ina msaada gan kwako.
ReplyDeleteukweli unauma, wache waanike madudu yale vyombo vya habari vya nchini hawawezi kuyaanika
ReplyDeletebado na hospitali zetu zanikwe maana huu umeshakuwa ujinga maradhi vifo, kila dakika tano ya maisha hospitalinimkwetu wana kufa si chini ya 15, ajali za barabarani, imekuwa kama fassion siku hizi kufa kwa ajali imeluwa kitu cha kawaida
ReplyDeletewalichosema BBC ni ukweli, enzi ya mwalimu ndiyo ilikuwa enzi ya kusifia tuuu hata madudu..... sasa hivi ni pasu kwa pasu
ReplyDelete