Boko Haram Wateka Wanawake 20 Kuongezea Idadi

Wakati bado kuna vilio na mipango ya kuwaokoa wasichana 200 wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haram la Nigeria, watu wanaosadikika kuwa ni wanajeshi wa kundi hilo wamevamia na kuteka wanawake wengine 20 kutoka kwenye eneo lile lile walilowateka wasichana awali.

Shuhuda wa tukio hilo ameiambia BBC kuwa watu hao waliokuwa na bunduki waliwalazimisha wanawake hao kupanda gari walilokuja nalo huku wakiwatishia kwa kuwanyooshea midomo ya bunduki.

Jeshi la Nigeria bado hatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo lililotokea katika maeneo ya wafugaji wa kabila la Fulani.

Jeshi hilo la Nigeria limekuwa likikosolewa kwa kushindwa kuchukua hatua na kudhibiti maeneo ya kaskazini Mashariki.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haiwezekani wasikamatwe au hiyo sehemu kusiwekwe usalama labda wanashirikiana na wakubwa serikalini hao Boko Haram

    ReplyDelete
  2. Boko haram ni nusu ya wanasheria wa nigeria.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad