BRAZIL 2014: Messi amfunika Ronaldo vibaya

Lionel Messi ni mchezaji mwenye thamani kubwa duniani kutokana na kulipwa karibu mara mbili zaidi ya Cristiano Ronaldo anayemfuatia.

Hiyo ni kwa sababu umri wa Messi ni miaka 26 wakati Ronaldo ana miaka 29.

Pia Raheem Sterling ni mchezaji mdogo (19) na mkubwa ni Andres Iniesta (30) walioingia katika orodha hiyo ya wachezaji 25 wanaolipwa zaidi kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Uswisi kiitwacho Neuchatel kwa kushirikiana na OptaPro, uliangalia thamani za wachezaji wa ligi tano kubwa za Ulaya kwa kutazama mishahara yao na gharama za uhamisho.

Messi kwa sasa ana thamani ya Pauni 175.6 milioni za Kiingereza akifuatiwa na Cristiano Ronaldo mwenye thamani ya Pauni 92.7 milioni za Kiingereza huku Eden Hazard akishika nafasi ya tatu kwa thamani ya Pauni 66.7 milioni,

Wachezaji 23 kati ya 25 walioshika nafasi za juu kwenye tafiti hiyo ni washambuliaji. Walobaki ni viungo wakabaji ambao ni Sergio Busquets na Paul Pogba.

Katika kundi hilo la wanasoka 25, 11 wanatoka Ligi Kuu ya Uingereza, nane wanacheza Hispania huku Ufaransa, Ujerumani na Italia zikitoa wachezaji wawili kila mmoja.

Katika soko la juu la nyota hao 11, Ronaldo na Gareth Bale (Pauni 51.2m) wamenunuliwa kwa gharama kubwa zaidi kwani Messi hajahama Barcelona toka ajiunge nao.

Kyle Walker na Luke Shaw pia wameingia katika kikosi cha wachezaji 11 wenye thamani zaidi duniani, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na CIES Football Observatory.
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ronaldo atabaki Kuwa bora tu acheni porojo.

    ReplyDelete
  2. Thubutu, ubora huo wa kufoce kupiga penalt

    ReplyDelete
  3. Ronaldo anatisha

    ReplyDelete
  4. ronaldo mkali miaka 800

    ReplyDelete
  5. messi anajuwa kuliko huyo mwanariadha wenu

    ReplyDelete
  6. mec anajuwa jaman achen upenz wenu w chuki kisa messi alifunga tim yako goli 4 peke yake sio sababu umchkie. wenyewe ulaya wametoa takwim hizo halafu ww upo bongo unabisha. huo ni uchizi messi uwezo 1000% huyo mwanariadha wenu atasubili xana na umli unaenda hivyo.

    ReplyDelete
  7. Mess noma..hyo bishoo wenu anaforce ukali.....goli LA matuta anashangilia km nn sijui nyoko zake

    ReplyDelete
  8. Messi 90% Ronaldo 10%

    ReplyDelete
  9. Mmeonaeee LEO anavyotisha, hataki goli la kupewa ye kazi yake kuwafungasha tela kuelekea golini. Ndio mana wamemuona mkaliii

    ReplyDelete
  10. Cristiano Ronaldo "CR7" El Magnifico

    ReplyDelete
  11. CR-7 Super Human

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad