Chenge: Serikali Imekosa Ubunifu Vyanzo vya Mapato

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge amesema Serikali imekosa ubunifu na haitaki kupokea ushauri kuhusiana na vyanzo vipya vya mapato.

a uchumi kwa mwaka 2013, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2014/15 pamoja na utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2013/14, Chenge alisema kuongeza ushuru katika bia, soda, juisi na vinywaji vikali, kumepitwa na wakati.

Wakati Chenge akieleza hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imetaja vyanzo mbadala vya mapato vinavyofikia Sh6 trilioni.

Katika taarifa yake, Chenge alisema mpaka mwisho wa mwaka wa fedha 2013/14, Bajeti ilikuwa pungufu kwa Sh2 trilioni, huku Bajeti ya mwaka 2014/15 ikiongezeka kwa asilimia 8.8 (trilioni 1.6), huku ikiwa na deni la Sh1.3 trilioni ambalo halikuingizwa katika Bajeti ya mwaka 2014/15.

“Hali hii inaweza kutafsiriwa kuwa Bajeti ya mwaka 2014/15 tayari ina pengo la Sh4.9 trilioni. Yaani Sh2 trilioni ambazo hazikupatikana mwaka wa fedha 2013/14 na Sh1.6 trilioni ambayo imeongezeka ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana na deni la Sh1.3 trilioni.

“Kuna umuhimu wa kuharakishwa kuletwa bungeni sheria ya bajeti itakayofanya kazi sambamba na sheria mpya ya ununuzi ili kudhibiti matumizi mabaya kwa nia ya kuweka nidhamu katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali,” alisema Chenge.

Alisema wakati Serikali ikiwa haina vyanzo vya uhakika vya mapato, Deni la Taifa lililofika Sh30 trilioni sawa na asilimia 57 ya pato la taifa ni mzigo wa taifa na tishio kwa utengamavu wa uchumi jumla.

“Uwiano uliopo wa Deni la Taifa na Pato la Taifa kiuchumi siyo wa kuridhisha. Ukubwa wa deni hili hauwiani na kiwango cha uzalishaji mali na ukuaji wa uchumi wa sasa wa asilimia 7.0,” alisema na kuongeza:

“Yalifanyika manunuzi ya Dola za Marekani 810,000 katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ambayo hayakupata kibali cha Mlipaji Mkuu wa Serikali.”

Alisema tatizo la kutokusimamia kwa umakini matumizi ya Serikali lilisababisha Bajeti ya mwaka 2013/14 kuanza na deni Sh611.4 bilioni, ambazo ni matumizi ya mwaka wa fedha 2012/13 na kwamba deni hilo halikuingizwa kwenye bajeti ya 2013/14... “Hali hii inatarajiwa pia kujitokeza tena kwa kiwango kikubwa zaidi kwenye bajeti ya mwaka 2014/15. Malimbikizo ya madai hayo hadi Desemba 2013, yalifikia Sh2 trilioni sawa na asilimia nne ya pato la taifa. Tatizo hili ni lazima litafutiwe dawa haraka,” alisema Chenge.

Alisema ongezeko la Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15 kwa Sh1.605 trilioni, ikilinganishwa na Bajeti ya Serikali inayomalizika ya mwaka 2013/14 linatia shaka iwapo malengo ya ukusanyaji na matumizi yatafanikiwa.

Alisema katika mwaka wa fedha 2013/14 utekelezaji wa bajeti katika baadhi ya mafungu ulifanyika kinyume na matarajio ya Serikali, kwa maelezo kuwa yapo baadhi ya mafungu ambayo hayakutengewa fedha lakini walipewa fedha nje ya bajeti za fungu husika.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sio kuwa kwa ajili ya vyanzo vya mapato tu ila utaratibu mzima hauko kwenye sera za kisasa bado tunategemea bajeti yetu iendeshwa kwa misaada.THe people and the goverment as a whole spent much time thinking and spent most of the time thinking how to steal and luxurious life.If someone steals and have money in banks and build houses.cars thats what they call development!

    ReplyDelete
  2. Chenge turudishie vijisenti vyetu

    ReplyDelete
  3. ni aibu kubwa kwa hawa wasomi wanaotayarisha bajeti ya nchi yetu kila mwaka toka tuko watoto hadi leo wazee mapato kutegemea bia ,soda,juice,sigara na petrol.some time kubalini ushauri wa kambi ya upinzani.sio kila kitu toka upinzani ni kibaya.hii nchi sio masikini kiasi hiki,tumejaliwa rasilimali nyingi sana tatizo wabunge wetu kuzalauliana kumezidi hata kwenye hoja za msingi.awamu ya nne tulitegemea makubwa kumbe ndio bule kabisaaaaaaa

    ReplyDelete
  4. BURE KABISA, na huyu chenge si ndiye mwenyekiti wa hiyo kamati au? yeye hausiki na mipango ya hiyo bajeti? kwakweli tunaviongozi BURE KABISA wa kizazi kipya! kila siku bia, sigara na soda! aibu!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad