Dawa za nywele zinazosababisha uvimbe wa kizazi kwa wanawake

Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

“Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

“Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

“Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,” anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. duh asante doc,,, sasa kama zina madhara kwa nini zipo madukani,, si watu wote wana uwezo wa kusoma maelezo na kuelewa,, cha msingi hapa TFD wasiruhusu uuzwaji wa dawa hizo za nywele

    ReplyDelete
  2. Dk chipata hebu ingia Google kidogo, hakuna sehemu inayo onyesha Fibroid ina sababishwa na Relaxer, Fibroid couses is Unknown mpaka sasa ila Female Hormones estrogen na progesterone it seems like Making fibroid to grow fast.Jaman hata kana wa bongo taaluma yetu ya afya ndogo basi Ma Dr msitudanganye kivile siku hizi uki Google tu unapata information zote unazotaka.

    ReplyDelete
  3. tena kichekesho dawa ya nywele inaweza kua na madhala mengine tofauti na hayo DR. CHAPATI unayoelezea maana mimi nilikua na fibrods tangu usichana wangu na dawa nimeanza kuweka hivi karibuni haya elezea hapo DR. CHAPATI fanya uchunguzi zaidi labda madawa ya watu wanao jichubua ngozi ili wae weupe ongelea hilo kwanini wanachanikachanika mwili?

    ReplyDelete
  4. Huyo dr chipata ni kihiyo kabisaaaa. USA ndiyo wamemfelea naabara ya ulaya Asia dawa wanawela haya watoto wadogo si ungekuwa na uvimbe wote Dr anatoka shule ya kidumu mfagio hajuo english anakariri mpka chuo kikuu sasa afanyaje??? Na siyo kama shule hizo nibaya ila wapo wanatoka huko na uelewa mdogo mwenyewe nimesoma huko

    ReplyDelete
  5. Mmmh urembo huu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad