SAKATA la tuhuma za ubakaji zinazomkabili mume wa Flora Mbasha sasa limechukua sura mpya baada ya maovu yao mengine kuanikwa hadharani na ndugu wa Flora…..
Msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cathy ambaye ni dada binamu wa Flora amedai kuwa kinachowatafuna wawili hao ni laana waliyoipata kutoka kwa babu wa Flora, marehemu baba Askofu Moses Kulola…..
Ndugu huyo wa Flora amesema kuwa wawili hao waliwahi kufikia nyumbani kwa askofu Kulola huko Mwanza,siku chache kabla ya Kulola kuaga dunia na kufanya madudu mengi ikiwemo kuingiza askari polisi kwenye chumba cha Kulola.
Ndugu huyo alidai kuwa wawili hao walifikia hatua ya kuingiza askari kwenye chumba cha askofu Kulola kwa madai ya kuibiwa sh. 300,000 ( Laki tatu ) za Emmanuel Mbasha, mume wa Flora huku wakimwaga matusi mazito kwa wajukuu wa Kulola….
“Walifikia pale kwa babu, yule Mbasha akawa na pesa kama laki tatu hivi, akazihifadhi kwenye nyumba ndogo ya chini waliyofikia,nyuma ya nyumba ya babu, akawa amesahau alikoziweka zile pesa basi wakaanza kuwatukana matusi ya nguoni wajukuu wa babu pale kama hawana akili nzuri, yeye Mbasha na Flora,” alisema ndugu huyon wa Flora.
Akaendelea kudai kuwa walipoona hakuna ushirikiano kwa wajukuu wa babu wakaamua kuita polisi waliofika pale nyumbani na kuanza kufanya upekuzi wa nguvu kwenye kila kona ya nyumba ya baba Askofu….
“Walipoona hawajafanikiwa kuzipata akaamua kuwaingiza polisi mpaka chumbani kwa babu, na babu alikuwa hayupo nyumbani, alikuwa kanisani, sasa aliporudi ndipo alikuta askari chumbani kwake wakifanya upekuzi. Babu alikasirika sana na kujikuta akimwaga machozi,” alisema Cathy
Akaendelea kudai kuwa babu alishangaa sana kufikia hatua ya wawili hao( Flora na mumewe) kutomwamini hata yeye mpaka kuingiza askari ndani ya chumba anacholala lakini wawili hao walimpuzaa hata baba Askofu huyo….
“Babu aliwalaani wale na aliwaambia kuwa siku si nyingi maovu na uchafu wao utajulikana kwenye jamii huko Dar wanakowaibia watu kwa kujifanya wameokoka wakati siyo kweli na wanatapeli watu kila siku,akasema wataishia pabaya muda si mrefu,” alisema Cathy.
Akaendelea kudai kuwa Flora na mumewe hawakuwahi kuomba radhi kwa babu yao Askofu Kulola mpaka alipofariki, na mpaka leo hii laana yake bado inaawatafuna sana na haya yanayoendelea ni matokeo ya laana hiyo.
Flora Mbasha na Mumewe kumbe wana Laana ya Askofu Kulola
13
June 16, 2014
Tags
Duuuuuuuuuh,wat a shame?
ReplyDeleteFilam inaendelea ila hilo la kuokoka ni mtu mjinga tu anaeamini hawa wana kwaya hua wameokoka. Ni waimbaji hawa sio walokole ila hujifanya hivyo au cc ndo tunawaitaga hivyo.
ReplyDeleteKimsingi hawa ni watafutaji tu kama wa bongo flavor au machinga hivi. Njaa yao ndo inawafanya wamdhihaki Mungu live kwenye majukwaa.
Amini nakuambieni sio kila mtu atajaye bwana bwana atauona ufalme wa mbinguni!
kama ni kweli hayo mwenyezi mungu uwasaidie wawili hawa maana shetani amechukua nafasi...ni zaidi ya aibu
ReplyDeleteKweli walichokifanya nilaana tupu,huwezi kuingia chumba cha mzee wako bila ruhusa tena na polisi...hawa watu hawana adabu kabisa.
ReplyDeleteMh haya basi bora wasisesme wameokoka jamani wokovu ndio uko hivi kweli simjichanganye tu duniani sahz walamsingepata kashfa hz mnadhalilika kwakuwa mmelitumia jina la mungu vibaya.nahii kwa walokole feki wote wanajijua
ReplyDeleteMi walokoleeeeeeee wamenitokaaaa,maaskofu wao wazinzi,kutudanganyadanfanya tu,Mara Huyu askofu hapo hapo mbunge,mtatumikiaje mabwana wawili?ubunge Ni ushetani,umo ndani Ni uoZo,uaskofu Ni mambo ya Mungu,
ReplyDeleteFlora alimpenda sana huyo,mbasha a.k.a.sura nzuri na kumbe jamaa mqenyewe amekaa kimaslah,zaidi hapakua na upendo,pale na wengine ndo mjifunze kubabaikia wanaume wazuri
ReplyDeleteMmh! ila kama ni kweli walifanya kitu kama hicho kwa mtu wa mungu kama yule kulola na kikamuuzunisha, inabidi watubie uovu huo tena kwa kufunga na kuomba mybe mungu atapunguza hasira yake
ReplyDeleteHv mngemaliza huo upumbavu wenu kimya*2 hz aibu zingetoka wap...hata mkitoa nyimbo nzur kias gan hamtauza tena,mmeharibu sana kwa kwel.
ReplyDeleteHaituhusu
ReplyDeleteMsimchezee mw.mungu huo umaarufu mlionao ni kudura zake na akiamua mtauza maandazi mshukuruni muumba wenu msione ufahari kujianika kila sk miuandaoni.
ReplyDeleteyan uyu frorah awezi toa nyimbo ninunie labda nimsikie akiabudu kanisani tu
ReplyDeletekweli achamove iendelee sasa sijui na hi ni tamptation au ni majanga
ReplyDelete