Flora Mbasha na Mumewe kumbe wana Laana ya Askofu Kulola

SAKATA  la  tuhuma  za  ubakaji  zinazomkabili  mume  wa  Flora  Mbasha  sasa  limechukua  sura  mpya  baada  ya  maovu  yao  mengine  kuanikwa  hadharani  na  ndugu  wa  Flora…..

Msichana  mmoja  aliyejitambulisha kwa  jina  la Cathy  ambaye  ni  dada  binamu  wa  Flora  amedai  kuwa  kinachowatafuna  wawili  hao  ni  laana  waliyoipata  kutoka  kwa  babu  wa  Flora, marehemu  baba  Askofu  Moses  Kulola…..

Ndugu  huyo  wa  Flora  amesema  kuwa  wawili  hao  waliwahi  kufikia  nyumbani  kwa  askofu  Kulola  huko  Mwanza,siku  chache  kabla  ya  Kulola  kuaga  dunia  na  kufanya  madudu  mengi  ikiwemo  kuingiza  askari  polisi  kwenye  chumba  cha  Kulola.

Ndugu  huyo  alidai  kuwa  wawili  hao  walifikia  hatua  ya  kuingiza  askari  kwenye  chumba  cha  askofu  Kulola  kwa  madai  ya  kuibiwa   sh.  300,000 ( Laki  tatu )    za  Emmanuel  Mbasha, mume  wa  Flora  huku  wakimwaga  matusi  mazito  kwa  wajukuu  wa  Kulola….

“Walifikia  pale  kwa  babu, yule  Mbasha  akawa  na  pesa  kama  laki  tatu  hivi, akazihifadhi  kwenye   nyumba  ndogo  ya  chini  waliyofikia,nyuma  ya  nyumba  ya  babu, akawa  amesahau  alikoziweka  zile  pesa  basi  wakaanza  kuwatukana  matusi  ya  nguoni  wajukuu  wa  babu  pale  kama  hawana  akili  nzuri, yeye  Mbasha  na  Flora,” alisema  ndugu  huyon wa  Flora.

Akaendelea  kudai  kuwa  walipoona  hakuna  ushirikiano  kwa  wajukuu  wa  babu  wakaamua  kuita  polisi  waliofika  pale  nyumbani  na  kuanza  kufanya  upekuzi  wa  nguvu  kwenye  kila  kona  ya  nyumba    ya  baba  Askofu….

“Walipoona hawajafanikiwa kuzipata  akaamua  kuwaingiza  polisi  mpaka  chumbani  kwa  babu,  na  babu  alikuwa  hayupo  nyumbani, alikuwa  kanisani, sasa  aliporudi  ndipo  alikuta  askari  chumbani  kwake  wakifanya  upekuzi. Babu  alikasirika  sana  na  kujikuta  akimwaga  machozi,” alisema  Cathy

Akaendelea  kudai  kuwa  babu  alishangaa  sana  kufikia  hatua  ya  wawili  hao( Flora  na  mumewe)   kutomwamini  hata  yeye  mpaka  kuingiza  askari  ndani  ya  chumba  anacholala  lakini  wawili  hao  walimpuzaa  hata  baba  Askofu  huyo….

“Babu  aliwalaani  wale  na  aliwaambia  kuwa  siku  si  nyingi  maovu   na  uchafu  wao  utajulikana  kwenye  jamii  huko  Dar  wanakowaibia  watu  kwa  kujifanya  wameokoka  wakati  siyo  kweli  na  wanatapeli  watu  kila  siku,akasema  wataishia  pabaya  muda  si  mrefu,” alisema  Cathy.

Akaendelea  kudai  kuwa  Flora  na  mumewe  hawakuwahi  kuomba  radhi  kwa  babu  yao  Askofu  Kulola  mpaka  alipofariki, na  mpaka  leo  hii  laana  yake  bado  inaawatafuna  sana  na  haya  yanayoendelea  ni  matokeo  ya  laana  hiyo.

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duuuuuuuuuh,wat a shame?

    ReplyDelete
  2. Filam inaendelea ila hilo la kuokoka ni mtu mjinga tu anaeamini hawa wana kwaya hua wameokoka. Ni waimbaji hawa sio walokole ila hujifanya hivyo au cc ndo tunawaitaga hivyo.
    Kimsingi hawa ni watafutaji tu kama wa bongo flavor au machinga hivi. Njaa yao ndo inawafanya wamdhihaki Mungu live kwenye majukwaa.
    Amini nakuambieni sio kila mtu atajaye bwana bwana atauona ufalme wa mbinguni!

    ReplyDelete
  3. kama ni kweli hayo mwenyezi mungu uwasaidie wawili hawa maana shetani amechukua nafasi...ni zaidi ya aibu

    ReplyDelete
  4. Kweli walichokifanya nilaana tupu,huwezi kuingia chumba cha mzee wako bila ruhusa tena na polisi...hawa watu hawana adabu kabisa.

    ReplyDelete
  5. Mh haya basi bora wasisesme wameokoka jamani wokovu ndio uko hivi kweli simjichanganye tu duniani sahz walamsingepata kashfa hz mnadhalilika kwakuwa mmelitumia jina la mungu vibaya.nahii kwa walokole feki wote wanajijua

    ReplyDelete
  6. Mi walokoleeeeeeee wamenitokaaaa,maaskofu wao wazinzi,kutudanganyadanfanya tu,Mara Huyu askofu hapo hapo mbunge,mtatumikiaje mabwana wawili?ubunge Ni ushetani,umo ndani Ni uoZo,uaskofu Ni mambo ya Mungu,

    ReplyDelete
  7. Flora alimpenda sana huyo,mbasha a.k.a.sura nzuri na kumbe jamaa mqenyewe amekaa kimaslah,zaidi hapakua na upendo,pale na wengine ndo mjifunze kubabaikia wanaume wazuri

    ReplyDelete
  8. Mmh! ila kama ni kweli walifanya kitu kama hicho kwa mtu wa mungu kama yule kulola na kikamuuzunisha, inabidi watubie uovu huo tena kwa kufunga na kuomba mybe mungu atapunguza hasira yake

    ReplyDelete
  9. Hv mngemaliza huo upumbavu wenu kimya*2 hz aibu zingetoka wap...hata mkitoa nyimbo nzur kias gan hamtauza tena,mmeharibu sana kwa kwel.

    ReplyDelete
  10. Msimchezee mw.mungu huo umaarufu mlionao ni kudura zake na akiamua mtauza maandazi mshukuruni muumba wenu msione ufahari kujianika kila sk miuandaoni.

    ReplyDelete
  11. yan uyu frorah awezi toa nyimbo ninunie labda nimsikie akiabudu kanisani tu

    ReplyDelete
  12. kweli achamove iendelee sasa sijui na hi ni tamptation au ni majanga

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad