Halima Mdee (CHADEMA), Amemtaka Mbunge Mwenzake, Leticia Nyerere, Aache Ubunge na Akajiunge na CCM

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amemtaka mbunge mwenzake, Leticia Nyerere, aache ubunge na akajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuliko kuendelea kukipigia debe chama hicho akiwa upinzani.
Kauli hiyo ameitoa jana alipokuwa akichangia bajeti ya serikali kwa mwaka 2014/2015 ambapo alisema matendo anayofanya Leticia ya kujipendekeza kwa CCM yatamgharimu kama ilivyotokea kwa wenzake.
Juzi wakati akichangia bajeti hiyo, Leticia alisema serikali ikifanya vizuri, lazima ipongezwe kwakuwa imepeleka maendeleo katika jimbo analotoka.
“Serikali yangu imefanya mambo mengi, imeniletea maji, walimu katika jimbo langu la Kwimba, ni lazima tuipongeze si kila wakati tunailaumu humu ndani,” alisema.
Katika mchango wake jana, Mdee, alisema jukumu kubwa la upinzani ni kuikosoa serikali na kuonyesha mbadala katika masuala mbalimbali na si kuisifia kwa kutekeleza wajibu wake wa kuwahudumia wananchi.
“Serikali inapata fedha kutokana na kodi za wananchi, inalazimika kupeleka maji, barabara na huduma mbalimbali kwa lazima si hiyari, tunapoikosoa tunatimiza wajibu wetu kama yenyewe inavyotekeleza inapowahudumia wananchi.
“Leticia Nyerere anaweza kwenda CCM, kwakuwa Rais Kikwete ana nafasi mbili za uteuzi wa wabunge, lakini lazima ajue waliojipendekeza CCM wamepigika sana hivi sasa, aachie ubunge aende huko kwakuwa ana mapenzi nao,” alisema.
Mdee alisema kuwa Leticia anaiaibisha kambi ya upinzani inayofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha serikali inaboresha huduma inazozitoa kwa wananchi.
“Upinzani si lelemama, kama anafikiria CCM ni kuzuri zaidi ni vema akaenda huko kuliko kubakia hapa pasipomfaa,” alisema
Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sawa 100% Halima Mdee kazi ya Upinzani ni kupinga sio kusifia .

    ReplyDelete
  2. Huo upinzani wa kijinga hta kaka kuna mazuri nyie kupinga tuu. Mtawapata hao wajinga wenzenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mazuri kivipi kutekeleza wajibu? Mzazi akiilisha familia yake vizuri anahitaji kusifiwa?

      Delete
    2. Mazuri kivipi kutekeleza wajibu? Mzazi akiilisha familia yake vizuri anahitaji kusifiwa?

      Delete
  3. Huo sio upinzani,bali ni jambo jingine ambalo jina lake halijulikani,upinzani maana yake ni kumkosoa mpinzani wako pale anapokosea na kuacha kufanya mambo ambayo alipaswa kuyafanya kwa ajili ya wananchi,lkn pale anapoyafanya yale mlioyafikiria nyie bila hata kupata changamoto kutoka kwenu,pia mpinzani halisi anapaswa kusema kuwa"nawapongeza kwa hili na lile"ambalo mmefanya.Hupaswi kulaumu tuuuuu kila jambo lkn jema hulisemei.Yaani ni sawa na Simba na Yanga ni wapinzani wa jadi,lkn mshabiki haliki wa Simba kama mm,pale yanga anapofanya mambo mazuri kwa mfano ya kutuwakilisha vizur ktk mashindano ya kimataifa,ni lzm niwasifie hivyo mm nahisi huyo Leticia Nyerere ndiye mpinzani wa kweli hao akina Halima Mdee ni waroho wa madaraka tu.

    ReplyDelete
  4. mkiwasifia ndowataanza kuridhika nakusahau wajibuwao,waliyo haribu nimengi kuliko waliyo yatekeleza,mapesa mengi yamechotwa nahawa ccm ss kuweka vijibomba na hao walimu wanaominywa kwenye mishahara...kunalakusifiwa hapo? nyiekweli ccm watawaibia paka kizazi chawajukuu wa watoto wenu kamamtakua kama leticia nyerere.

    ReplyDelete
  5. hapo umesema mdau asifiwe kwa lipi jipya wangesema wamerudisha yale mapesa yaliochotwa uswiss ndio tungewaona wamerudi kwenye msitari lakini kutoa huduma kwa wananchi niwajibu wao kwani pesa sio zao bali ni za wanachi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli na wewe mdau pia umelonga kama jamaa hapo juu!hawa watu wana mabilion ya hela wameficha uswiss siku wakiyarudisha na kutubu kwa watanzania kweli watakuwa wameonyesha uzalendo na hapo watakuwa wanastahili pongezi!ila kwa masuala ya msingi ni hako ya kila mwana nchi tena sio ombi ni amri ya serikali kuhakikisha kila raia wake yuko katika hali nzuri!jaman hamuoni mfano kama marekani?sisi tunalipa kodi so ni haki yetu kisheria kupata huduma nzuri serikali haiitaji mpaka tuisifie ni haki yetu ile sema wananchi wengi ni mburula wanaona kama serikali imepiga hatua kuwasaidia.kodi zetu hizi ndio zinazotumika hapo.

      Delete
  6. Mimi naona upizani sio uadui wakuponda kila kitu upinzani ni kama referee kama watu wanacheza kukawepo moja anataka kuonyesha kuwa kuna dhambi imefanywa huwa refa huonyesha ishara yakusema endeleeni na mchezo. kweli chama kipo katika kushika hatamu ya serekali wapinzani nikuonyesha madhambi tuu na vitu vingine waone niwajibu je mtu akitekeleza huo wajibu tulio wanguana tunyamaze au tuseme ili tunapokosoa ifahamike kweli kuwa tunafanya kama referee. Je mtoto kama wewe kazi yako nikumuonyesha madhambi tuu atakuona wewe kama unamtakia mema au?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kutoa mapovu mdomon wewe, huelewi hata nini unaongea..nenda katafakari ndo uje umwage pumba zako...mpira na mambo unayoongea wapi na wapi,si kla.mfano basi unafit kila sehemu tu..

      Delete
  7. Halima upo sahihi,badala ya kuhoji ni.kwanini Kwimba hakuna maji wala barabara miaka hamsini ya uhuru licha ya kuzalisha pamba kwa wingi Leticia anasifia kinafiki.Ni bora chadema tubaki na wabunge wachache kuliko kujaza wasaliti kama Zitto,Walid Kaborou,Akwilombe,Mwigamba,Kitila,Shonza,Mchange na virusii vya ccm.

    ReplyDelete
  8. Nyie watz cjui mtafunguka lini.... hebu fikiria tangu uhuru serikali ya ccm ndo imetawala mpaka sasa.... lkn n mambo mangap mazuri waliyoyafanya?? huwex kujisifia kuwa na baiskeli kwa miaka 5, ukasema upiga ha2a wkt una rasilimali nyingi. kwa ufupi ccm ni wexi na uyo leticia arud drsani n mwehu....wixi wa RICHMOND serkal ilichukua ha2a gani? sakata la EPA serkal ilimleta babu wa loliondo kuwa anatibu magonjwa sugu yote unayoyajua ww!! wa2 walimiminika wakasahau km kuna EPA...tembo wameliwa weng kwny uongox wao inasikitisha sn!!! wkt gesi inagundulika srkali ilasema ttx la umem n historia je, n kwel limekuwa historia?? leo watz kila mmoja anadaiwa laki 6,,wahuni wakubwa ccm....

    ReplyDelete
  9. Leticia anajua siasa........haliama mdee pole sometimes siasa kama inakukimbia vile....zamani kweli lkn siku hizi siasa hujui....hakuna serikali iliyo madarakani duniani kwa ajili ya kuumiza nchi yake....mwenzio kaona lazima atoe big up!......then angalia ukoo aliotokea....mbowe kamsifia kikwete kule kwao kwa kupitisha barabara kiwango cha lami na chiaz wakagonga........swala la kusifia maendeleo ktk nchi si la kichama ni la kila mzalendo....mungu aendelee kutulinda tanzania na amani yetu,upendo wetu,ushirikiano wetu uliodumishwa na ccm kwa uwezo wake........0717337536

    ReplyDelete
  10. Letcia ndo Nani jaman???? Chademaa kwa MIZIGO WABUNGE!!! Mmmmh

    ReplyDelete
  11. Pamoja na kukosoa wanawake wana behave tofauti kuna personality ya kike hapo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad