Hili la miaka nane ya uchakavu magari ni kuwakomoa wananchi na kulinda barabara zisizo na Viwango

Nimejaribu siku hadi siku kuangalia hili swala la serikali kudai inalinda nchi na magari chakavu na sasa imepunguza miaka ya uchakavu kutoka kumi hadi nane. Hivi serikali hii imeangalia uwezo wa wananchi kununua magari yasiyo chakavu? Mbona hayo ya miaka nane yapo mengi yana zaidi ya milage 200,000? hapo siyo uchakavu?

Je wametathmini gharama za hayo magari yenye miaka nane kama mtanzania wa kawaida anaweza kuyanunua au lengo ni kupunguza uwezo wa wananchi kununua magari? Au hii ni mbinu mbadala ya kuongezea wananchi mzigo na wao kuvuna kodi? Wabunge nao watakaa kimya? Mbona hayo ya miaka kumi yapo mengi yenye milage chache na hayo ndo siyo chakavu ukilinganisha na haya ya miaka nane yenye mileage hadi laki 3? 

Ni imani yangu kuwa kutokana na mipango mibovu ya miundombinu ya barabara hii ni mbinu ya kupunguza watanzania wenye uwezo wa kumiliki gari. Waziri asisingizie kupunguza ajaili kwanza hana justification yeyote kuwa hayo magari analeta ajali ukiachilia ambayo tayari yapo. Asilimia 90 ya magari yaliyopo tz yakiwemo magari ya waziri mwenyewe ni mabovu zaidi na ungeyapeleka japani yasingeruhusiwa kuuzwa tena kwani ni mabovu mara mia ya yanayokuja yakiwemo yaliyotengenezwa miaka ya 90. 

Serikali iache ubabaishaji na badala yake wajenge barabara zenye uwezo na kuwapa nafasi wananchi kumiliki magari.
By nginda JF
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tushawachoka hao weusiongee sana 2015 simbali fanya unyama kwenyekura mabadiliko hayatakuja bila kuamua kurayangu sasa ngoja ale mwingine nae hawa wanaorisishana nchi tumewachoka.so 2015nyimakura.wakaibe kama kawaidayao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad