Stori: Haruni Sanchawa
NYUMAya pazia! Yule msichana Yusta Lucas (20) mwenyeji wa Mkoa wa Tabora ambaye alifika jijini Dar kufanya kazi ya u-hausigeli na kufanyiwa ukatili wa kutisha na bosi wake kisha habari zake kuandikwa, ametoa siri nzito, Uwazi limemegewa.
Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili akiwa wodini kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala jijini Dar, Yusta ambaye amefanya kazi kwa tajiri yake huyo kwa miaka mitatu alisema:
“Kwanza nataka watu wajue kuwa mwajiri wangu ni binamu yangu, alinileta hapa Dar kwa ajili ya kumsaidia kazi za ndani pamoja na kumlelea mwanaye.
“Kipigo hasa kilianza mwanzoni mwa mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuning’ata kwa meno mwili mzima, ndiyo maana mwili wangu wote unaonekana una mabakamabaka.
“Mateso yangu majirani walikuwa wakiyajua kutokana na kilio changu lakini walikuwa wanashindwa kunisaidia kwa sababu ya ushirikiano mdogo.
“Kwanza nashangaa sana kwa adhabu yake ya kuning’ata meno mpaka damu zinabaki kwake. Je, kama nina virusi vya Ukimwi si na yeye anavipata?
“Sijajua alikuwa anapata wapi ujasiri wa kuning’ata meno. Kwa kweli nimeteseka kwa muda mrefu sana. Mungu ndiye anajua, lakini nawashukuru sana majirani walioliona hilo na kuamua kuchukua hatua.”
KUHUSU MAISHA YA TAJIRI WAKE
Aidha, Yusta alianika mienendo mitano ya bosi wake huyo na kusema imekuwa ikimshangaza sana.
MWENENDO WA KWANZA
“Mimi katika kuishi kwangu pale sijawahi kumwona jirani yeyote amekuja ndani kusalimia wala yeye kwenda kwa jirani kufanya hivyo jambo ambalo si la kawaida.”
MWENENDO WA PILI
“Yeye (bosi wake) hana mume. Lakini tangu nimeishi pale kwa miaka mitatu sijawahi kumwona mwanaume ameingia ndani ya nyumba achilia mbali wanawake wenzake, hata mgeni. Kifupi yeye ni yeye kwa pale nyumbani kama ana marafiki labda wanakutana mbali.”
MWENENDO WA TATU
“Muda wake wa kurudi nyumbani siku zote ni usiku mnene, amewahi sana ni saa mbili usiku. Kwa hiyo, muda mwingi mimi ndiyo huwa nyumbani.”
MWENENDO WA NNE
“Anajiweza, sijui kwa nini aliamua kunifanyia hivi. Maana mtu ana gari, anaendesha mwenyewe na anasema ana hela, ndiyo maana namshangaa kuniadhibu kwa kuning’ata kwa meno.”
MWENENDO WA TANO
“Sikumbuki lini nimewahi kumwona akicheka. Muda mwingi anaonekana amekasirika tu kiasi kwamba nimekuwa nikimwogopa siku zote.”
OMBI KWA SERIKALI
Yusta alisema kufuatia matatizo makubwa yaliyompata ameiomba serikali imsaidie aweze kurudi nyumbani kwao Tabora.
SHUKURANI KWA MAJIRANI
Yusta alitoa shukurani kwa majirani waliojitokeza kuokoa maisha yake ambapo alisema kama wasingekuwa wao hajui ingekuwaje.
MANENO YA MUUGUZI
Kwa upande wa hospitali hiyo, muuguzi kiongozi wa zamu siku hiyo, Mahija Swalehe alikemea tabia za waajiri wa wafanyakazi wa ndani kuwatesa na kuiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa jicho la tatu ili kukomesha vitendo hivyo.
TUJIKUMBUSHE
Yusta alikumbwa na masaibu hayo kwa muda mrefu hadi hivi karibuni majirani wakiwa na polisi walipovamia nyumba hiyo na kumkamata bosi wake kisha kumpeleka Kituo cha Polisi cha Oysteraby, Dar ambako anashikiliwa na yeye kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibu baada ya kukutwa na majeraha.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa ametiwa mbaroni.
GPL
pole dada mungu atakusaidia
ReplyDeletepole
ReplyDeleteOh! Akiwahi sana nyumbani ni saa 2 kama sio jambazi atakua muuza uchi serekali itachua hatua pole sana myamwezi karibu Tabora.
ReplyDeleteNI DEVIL WORSHIPPER HUYOMAMA
ReplyDeletePole dada duh noma . Ila mwaka mzima unang'atwa tu unakubali mtu mwenyewe hashindi nyumbani kwanini usingemtoroka
ReplyDeleteni devil huyo muuza uchi akirudi hua ashachokeswa hatakua nanguvu za kumtesa hivyo
ReplyDeleteVipi mtu anayependa kuona damu, anayeng'ata mpaka damu inatoka, ambaye jiraha la jana kwake si kitu, kovu la juzi si neno....ni kuendelea kuona damu...tumuiteje? Kuna kitu si sawa kwa huyu mama...kweli kuna kitu si sawa...yapo yatakayofumuka zaidi...!!!
ReplyDeleteDada pole, Mungu ni mwema akusaidie na akulinde daima. Amina.
devil ni noma!!!!!!
ReplyDeletesheria ichukue mkondo wake tu hakuna haja ya hili wala lile, tuwaache polisi waendeleea na uchunguzi wao kisha ichukue hatua zinazofaa
ReplyDeleteatakuwa Vampaya
ReplyDeleteAtakua vampire aka zombie
ReplyDeletemungu ana kaz kubwa dunian mwanandamu km huyu hatakiwi kuishi kamwe...mana anashindwa kutimiza ahadi za mungu manyanyaso makubwa kamfanyia binti huyu mungu amrehemu
ReplyDeleteHUYO BOS KAMA SIO VAMPARE BAS NI ZOMBI POLE DADA.
ReplyDelete