Huyu Ndiye KASA Aliyetabiri BRAZIL Kuifunga CROATIA kwenye mechi ya Ufunguzi Leo

BAADA ya pweza Paul aliyekuwa akiishi Ujerumani kujizolea umaarufu wakati wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, fainali za mwaka huu nchini Brazil ameibuka mtabiri mwingine aitwaye Cabeção au Big Head.

Big Head ambaye ni kasa mwenye umri wa miaka 25, anayeishi katika kijiji cha Praia Do Forte nchini Brazil ameitabiria nchi yake ya Brazil kuibuka na ushindi katika mechi ya ufunguzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Croatia kesho.

Big Head ameanza kazi yake hiyo jana, Jumanne kwa kutabiri mechi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia. Kasa huyo anafanya utabiri kwa kuchagua vyakula. Alichagua mmoja wa samaki waliokuwa wananing’inia katika bendera za Brazil, Croatia na kwenye mpira.

Mwanzo alikwenda kama anakula samaki aliyekuwa kwenye mpira ambapo angemaanisha sare, ila baadaye alielekea katika bendera ya nchi yake Brazil na kula samaki akimaanisha ushindi kwa wenyeji kwenye mechi ya kesho itakayochezwa saa 5 usiku.

Utabiri wa Big Head umeonekana kuwa wa kawaida na baadhi ya wapenzi wa soka maana kikosi cha Brazil kinaonekana kuwa kizuri zaidi kuliko Croatia, japo bado hakuna mwenye uhakika wa nani ataibuka kidedea kwenye mechi hiyo!
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu pia ni wakukaanga kama vile pweza alivyofanywa! haya maviumbe yanatuharibia ladha ya mpira kama hamjui coz kama ikiwa kweli hapo unafikiri nani atakaye kesha usiku kusubiri mechi wkt kasa kashaicheza mechi kitambo.

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa mdau hapo umenena

    ReplyDelete
  3. Ahahahahh n shhiiiiiiidaaaaaaaah dunianiiiiiii

    ReplyDelete
  4. ndo ivo tena casa katabiri kweli

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad