Huyu Ndiye Mpenzi Mpya wa Irene Uwoya! Azungmzia Tofauti ya Umri wao na Mipango Yao.

Mkali wa Sound Track ambaye pia ni mkali wa kuvunja (dancer) amezungumzia uhusiano wake na muigizaji mrembo wa Bongo Movies, Irene Uwoya.

Akiongea na tovuti ya Times Fm, Msami alizunguka sana mbuyu kutaka kutoa maelezo kuhusu ukweli wa mambo kati ya wawili hao lakini kwa mara ya kwanza aliamua kuiambia tovuti ya Times Fm kauli yake kutokana na jinsi alivyoulizwa.

“Kaongea kwa upole huyu jamaa, kaapproach ili apate jibu. Ni kweli (kicheko)…nimekuridhisha lakini, nimeamua kukuridhisha.” Amesema Msami..

Muonekano wa Irene Uwoya na Msami kwa muonekano uliwafanya wengi wazungumze kwenye mitandao ya kijamii kuwa Msami amegeuka Serengeti Boy kwa Uwoya ambaye wanaamini anamzidi sana umri. Lakini ukweli ni kwamba Msami ni mkubwa kwa Uwoya. Chukua hiyo!

“Unajua mimi mwanzo, Serengeti Boy nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Yaani ile deeply nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Kwa hiyo leo ndio nimepata tafsiri yake ‘Serengeti Boy’ kumbe ni mtu ambaye amezidiwa umri. Tofauti na mimi nilivyokuwa nawaza kuhusu Serengeti Boy.

“Lakini mbona nikasema kama ni hivyo, as we are best friends lakini (joke), lakini mbona mimi nimemzidi umri Uwoya. Lakini mimi ni mkubwa kwake sema yeye ananizidi umri. Mimi ni mkubwa kwake nimemzidi miezi mingi…yaani wewe jua nimemzidi miezi mingi. Mimi ni mkubwa kwa Uwoya.” Alisisitiza Msami 

Katika hatua nyingine, Msami ameeleza mpango wake na Uwoya kutoa filamu ya pamoja na jinsi filamu itakavyokuwa.

Amesema katika filamu hiyo yeye ndiye mhusika kuu na kwamba ni filamu ambayo itahusisha dance na muziki. Filamu hiyo itatoka mwaka huu lakini bado haijapata jina rasmi na tarehe ya kutoka.

“Movie inakuja very soon, watu wakae tayari.” Amesisitiza
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vitoto vingine kwa kupenda maisha ya softwear vinatudhalilisha sana, na ndomaana mnakufa mapema kabla ya umri kusogea

    ReplyDelete
  2. iyo kweli vitoto skuizi vikishajua kupaka poda bas

    ReplyDelete
  3. Hawana lolote ni wale wale ma losers

    ReplyDelete
  4. Uwoya ni wa 87 sasa shida apo iko wap

    ReplyDelete
  5. Huyo nae hana utoto wowote muache kukuza habar sianajua kukojoa au hajui kulengesha ilipo msitutoshe

    ReplyDelete
  6. Hahahahahahaa mbavu zangu zinauma kwa kicheko mdau 3.54 umeniacha hoi eti akikojoa na kulengesha tundu hana cha utoto. well done umefunga mjadala upo wapi uje kupata drinks hapa ww ndo mtu bana umetoa point ya msingi

    ReplyDelete
  7. Uwoya ni wa 88 na siyo 87 ana mwill mkubwa tu. Na kuhusu huyo msami ni uongo mtupu hawana uhusiano wa kimapenzi, vjana wa siku hizi wanatafuta scandal .ili wawe maarufu

    ReplyDelete
  8. uwoya anajishusha miaka ni wa 87 kalaghabao

    ReplyDelete
  9. mtoto wa umemzaa wewe?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad