Bara la Afrika leo alfajiri limetupa karata yake ya pili kwenye michuano ya kombe la dunia, kwenye mchezo kati ya Ivory Coast vs Japan.
Mchezo huo ambao ulianza majira ya saa 10 usiku, umeisha kwa Ivory Coast kuitoa kimasomaso Afrika kwa kuwa timu ya kwanza kushinda kwenye michuano ya mwaka huu baada ya kuitungua Japan 2-1.
Magoli ya Ivory Coast yamefungwa na Wilfred Bony na Gervinho – Keisuke Honda aliifungia Japan goli la kufutia machozi.
Mchezo mwingine kwenye kundi hilo ulichezwa mapema kiasi saa mbili usiku kati ya Colombia dhidi Ugiriki.
Matokeo yalikuwa 3-0 kwa ushindi wa Colombia ambayo ilimkosa staa wao Radamel Falcao.
safi xana kiukweli ninefurah
ReplyDeleteI'm proud of Africa.wanastahili pongezi. Nimefrahi sana
ReplyDelete