Je, Tume ya Uchaguzi wa Tanzania Inaweza Kudhubutu Kukaidi Amri ya Serikali au Hata Rais Kama Walivyofanya Malawi

Natafakari mchakato wa uchaguzi wa viongozi Malawi ukihusisa kumchagua Rais wa nchi hiyo jinsi ulivyofika mahali ukaleta sintofahamu hasa pale Rais aliyeondoka madarakani mh. Joyce Banda alipoamuru tume isitishe shughuli za uchaguzi hadi utakaporudiwa upya baada ya siku 90. 

Tume ilionyesha msimamo kinyume na amri haram ya mh. J. Banda na kujitanabaisha kama chombo huru chenye kuendesha shughuli zake kwa kufuata taratibu na mamlaka huru za kisheria na kikatiba pasipo kuingiliwa wala kuamrishwa ni lipi walifanye na lipi wasifanye. Hatimaye kama wengi tujuavyo tayar tume imemtangaza Prof. kuwa mshindi na Rais mpya wa Taifa la Malawi.

Je, tume yetu ya uchaguzi wa Tanzania inaweza kudhubutu kukaidi amri ya serikali au hata Rais na kufafanua kwa nini amri yake haitekelezwi? Tume hii ambayo hata katibu tu mwenezi wa CCM anaipa maagizo na maelekezo nayo inayatekeleza mara moja!! Tume ambayo inasema mikutano isifanywe siku fulan lakini CCM wanaweza kufanya ila kikifanya chama cha upinzani ni haramu yanapigwa mabomu na m/kiti wa tume anasema kilichofanyika ni sawa......!!!!!

Bado naendelea kutafakari................
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania itakuwa inajifunza mengi tu katika haya. yanayojili katika bara hili, Malawi wameonyesha mfano mzuri na nchi zingine za Africa zitaiga mfano wake, bado Joyce Banda ni mwanamke shujaa, alikuwa pale kikazi zaidi kama kiongozi kuongoza jamii, sio kuvuruga jamii, hii ndio demokrasia inayotakiwa, ajakaa kifisadi kujumu nchi ata, alikaa kam kiongozi anaetumikia Taifa lake, klwani hata haya uongozi yana mwisho, uwezi kufanya kazi ya uongozi siku zote

    ReplyDelete
  2. Mbele ya ccm mahakama mavi tu. Nchi hii sie walalahoi ilimrad tunapumua....

    ReplyDelete
  3. kwa nchi yetu bado sana,ikifikia kama Malawi tume ya uchaguzi kufuata utaratibu basi CCM wanaweza kung'oka madarakani.

    ReplyDelete
  4. tumeyetu ya uchaguzi ijifunze nayo,iache kuwa kibalaka cha chama tawala.

    ReplyDelete
  5. The rule of law ,Tanzania ,hakuna chini ya chama cha Ccm,hapo ndio kuna ,shida,na bunge lipo,na mahakama yapo,Mungu tusaidie,

    ReplyDelete
  6. aliyeteuliwa na rais, kamwe hawezi kwenda kinyume na rais...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na yule wa malawi mbona amekata na amekwenda kinyume na rais?nyinyi ndio maboya utumbo mtupu mmeshanakirishwa kuwa mkiwapa upinzani basi vita itatokea kutakuwa na njaa huku wenyewe wakila nchi kiulaini!we mburula siku nyingine usilete coment zako za kikuma humu sawa?sema ndiooo mkundu wewe.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad