Kampuni ya MultiChoice Africa inayoandaa mashindano ya Big Brother Africa imetangaza tarehe ya usaili wa shindano hilo mwaka huu katika nchi mbalimbali za Afrika.
Waandaaji hao wameitaja nchi ya Rwanda mwaka huu kuwa miongoni mwa nchi zitakazokuwa na washiriki katika shindano hilo mwaka huu ambapo mshindi ataondoka na kibunda cha $300,00.
Nchi zitakazoshiriki mwaka huu ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Afrika Kusini, Sierra Leone, Nigeria, Botwasana, Malawi, Namibia, Ghana, Zimbabwe na Ethiopia.
Kwa Tanzania, usaili utafanyika July 11 na July 12 jijini Dar es Salaam (New Africa Hotel).
Ni muda wa kuona sarakasi nyingine na kuibua mengi mapya yakiwemo mahusiano ambayo mengine huwa na nguvu hata baada ya kumalizika kwa shindano hilo.
Mwaka jana mshiriki wa Namibia, Dillish Mathews aliibuka mshindi wa msimu huo ulipewa jina la The Chase.
sintah kasema tatenda.eeeeeeh makubwa
ReplyDeleteNana best kumbe unakumbukaaaaae Bi Sinta alisema tutamuona big brother Africa, haya ndo hiyo inakuja we are waiting for her, mama wa masters, sasa sijui atakuwa anawakilisha Uganda au Tanzania maana tanzania ndo mchakato wa kutafuta mshiriki/washiriki unaanza ila yy alisema tangu feb if not march kuwa tujiandae kumuona big brother which means alishachaguliwa tayari. All the best mama Nature sory Okwi.
ReplyDeleteTunamsubiri jimama dida nae
ReplyDelete