Kauli ya Michael Wambura Baada ya Kurudishwa Kwenye Uchaguzi wa Simba

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

SAA chache baada ya kamati ya Rufani ya shirikisho la kandanda Tanzania, TFF, chini ya mwenyekiti wake, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya kumrudisha, Michael Richard Wambura kwenye uchaguzi wa Simba sc, mgombea huyo amesema sasa haki imetendeka na uchaguzi utakuwa wa amani.

Wambura amezungumza na mtandao huu dakika chache zilizopita na kusema kuwa anaufananisha ushindi wake kama mchezo wa mpira wa miguu.

“Mpira wa miguu una mechi ya nyumbani na ugenini, unaweza ukafungwa ugenini, ukashinda nyumbani, bila kujali umeshinda goli ngapi, lakini ninachoweza kusema ni kwamba haki imetendeke, matokeo yametoka, tujipange kwenda kwenye uchaguzi ili wanasimba wapate viongozi wao wanaowataka”. Amesema Wambura.

Mgombea huyo ameongeza kuwa hiki sio kipindi tena cha kutafuta mchawi, bali ni kipindi kinachohitaji wanasimba kuwa makini.

“Ni kipindi cha kuwa makini, kuweka sera zetu hadharani, malengo yetu hadharani, ili wana Simba wapate fursa ya kuchagua kwa sera, nadhani hilo ndio ombi langu”. Ameongeza Wambura.

Hata hivyo, Wambura amesema kesho ataongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Simba mtaa wa Msimbazi, kariakoo jijini Dar es salaam.

- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=1912#sthash.rYmIk93x.dpuf
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwenye mchezo wa soka kuanzia FIFA kuna michezo michafu sana haswa kwenye uongozi.Wambura is a big threat kwa wezi na waporaji wa mali za club na hata tff na ndio maana inatumika nguvu nyingi sana kumzuia kila anapogombea uongozi wa mpira mahali popote maana anajua siri nyingi sana za viongozi wa vilabu na vyama vya mchezo wa soccer.hongera sana Wambura kwa ushindi.usikate tamaa pambana hadi last drop.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad