Kilichomuua ‘Mtoto wa Boksi’ Chabainika; Wahusika Kunyongwa!

Kufuatia kifo cha mtoto Nasra, almaarufu kama ‘mtoto wa boksi’, kuna kila dalili kwamba kifo chake kimetokana na maradhi aliyoyapata wakati akiwa anaishi kwenye boksi. Kwa kuwa imethibitika kwamba mtoto alifariki kutokana na ugonjwa wa pumu—kufuatia kufungiwa kwenye mazingira machafu, kutoogeshwa na kupigwa na baridi masaa 24, na kwa kuwa wahusika waliokuwa wakimfanyia ukatili huo tayari walishakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kula njama za kumtesa mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia na asiyeweza kujitetea, mawakili wanaosimamia kesi hii watabadilisha masitaka ya kesi na kuwa KESI YA MAUAJI YA KUKUSUDIA.

Adhabu kwa mtu anayeua kwa kukusudia ni KUNYONGWA MPAKA KUFA. Kwa hiyo, wahusika wanasubiri kunyongwa hadi kufa pindi hukumu ya kesi hii itakapotoka. Na kwa kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani hawa wanadamu wasokuwa na haya, wajiandae kupokea kitanzi ili liwe fundisho kwa washenzy wengine wenye tabia za kinyama kawa hawa wendawazimu.

NIONAVYO:
Natoa wito kwa watanzania wenzangu kutoa taarifa polisi haraka pindi waonapo ukatili wowote dhidi ya wanyonge, hasa watoto wadogo, ili sheria ichukue mkondo wake. Tatizo la watanzania walio wengi ni kwamba hatujaliani. Unaweza ukamuona mzazi/mlezi akimtesa mtoto lakini ukakaa kimya. Kufanya hivyo ni kutomtendea haki yule kiumbe anayeonewa au kunyanayaswa. Tuweni na huruma kwa viumbe hawa wa mwenyezi Mungu wanaoonewa bila sababu za msingi huku wakiwa hawawezi kujitetea kwa namna yoyote ile. Tukio la mtoto Nasra, ambaye Mungu amemuita kwake, liwe fundisho kwa watu wengine wanaofumbia macho ukatili kwa watoto na wanyonge.

Nawasilisha.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hao wangekua uku pakistan, mbona ni mawe mpk kifo

    ReplyDelete
  2. yaani inaskitisha sn..!huyo mama au alikuwa na ugomvi na mama yk huyo mtoto ndo mpk akafikia kumkatili huyo mtoto au ttz ni nn mpk amemfanyia hvy nashndwa kuelewa sbb ni nn mpk ikawa hvy...hebu jeshi la polisi chunguzen kwa kina...!

    ReplyDelete
  3. Watu kama hawa huwa. Hawanyongwi adabu yake kila siku moja unamkata pua next day unamkata mdomo next day unamkata. Ulimi nex day mapumbu kidogo kidogo kila siku azabu mpaka wanakufa na uko wanapokwenda uko wakifika tu hawakai chini

    ReplyDelete
  4. Yaan imeniuma sna...sijui kwann alimua kumpa mateso makali mtoto kwa miaka yote mnne...najiuliza kwann....yaan hakuwa ata na chembe ya hurumu.....Eee Mungu wang.....wengine tumekuja hapa duniani kwa mateso....inauma sna ukifikiria maisha aliyokuwa anaishi marehem mtoto Nasra ndani ya box....uyo mama hiyo adhabu ya kunyongwa mimi naiona ni ndogo sna......labda aliwe na mambwa mpaka afe

    ReplyDelete
  5. Hii habari inanisikitisha sana natamani ningemwuliza yule mama nikwanini alifanya ukatili kama ule.

    ReplyDelete
  6. Unajua mungu nomaaa......mtoto huyu angekufa siku nyingi....ukizingatia alikua +,hakupelekwa clinic kwa ajili ya dozi,maendeleo ya ukuaji kwa mtoto,muda wote huo mungu hakumchukua......mwisho mwisho baada ya kuwaumbua walezi......jinsi walivyomkatili haki ya kuishi na wao wanaupitia ukurasa ule waliompitisha nasra.....inauma nasra alikua hawezi kutoa maelezo.......raha kwao maelezo wanyoosha.....hiyo ndio malipo hapahapa duniani.....kwa style yoyote ile....0717337536

    ReplyDelete
  7. Wapumbavu sana natamani niwachape bakora

    ReplyDelete
  8. Yaan inahuzunisha...kanaonekana kangekuwa kabinti karembo kweli. Imeniuma mno...roho hiyo ni mbaya sana.

    ReplyDelete
  9. hao wazazi kweli boko haramu

    ReplyDelete
  10. adhabu stahiki na wao wafungiwe kwenye sanduku la chuma badala ya box kwa muda ule ule na kwa staili ile ile waliyomtendea yule mtoto

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad