Kundi la Al Shabaab Lakiri Kushambulia Kenya na Kuuwa Watu 49

Watu zaidi ta arobaini na tano wameuawa katika mashambulizi ya Mpeketoni
Kundi la wapiganaji wa Al Shabaab nchini Somalia, limekiri kufanya mashambulizi katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu, Pwani ya Kenya.
Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu 49.

Taarifa ya kundi hilo ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi dhidi ya serikali ya Kenya kwa kufanya msako dhidi ya waisilamu kwa njia ya kuwafunga kiholela na kuwaua wahubiri wa kiisilamu.
Baadhi ya walioshuhudia mashambulizi hayo wamearifu BBC kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.

Mji wa Mpeketoni uko umbali wa kilomita miamoja kutoka eneo la mpakani na Somalia
Kenya imekumbwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa kisomali wa Al Shabaab tangu ipeleke wanajeshi wake Somalia mwaka wa 2011.

Duru kutoka kisiwa cha Lamu zimearifu kuwa wapiganaji hao walifika katika malori mawili na kurusha kifaa kama bomu ndani ya kituo cha polisi kisha wakakivamia na kuiba silaha.
Pia waliteketeza hoteli na vijiji huku wakiwapiga watu risasi kiholela

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. m/mungu alisiema dalili za kiame zitakapofika kila balaa litatoke na kweli dunia ya leo vituko vingi! wadau dunia inakwIsha tumrudie mungu wetu!

    ReplyDelete
  2. allah akbar, yaani ubinaabamu unaisha polepole jamani. mbwa hawa woote serikali ya Kenya na Mashabab. wanaharamu. kama kweli ni kisasi si ukapige jeshi? sio wanaichi wa kawaida kabisa hawana hata hatia yeyote. inshallah m.mungu awalaze pema peponi Amin

    ReplyDelete
  3. mwanaharamu baba yko na wao mbn wakenda somalia hawawapigi al shabaab wanapig watu wa kawaida ilo hujaliona au?

    ReplyDelete
  4. Inasikitishasana sasa hayamambo yataendelea hivi hadilini jamani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad