Lowasa Atangaza Neema Kwa Vijana

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema vijana 10,500 waliojitokeza hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufanya usaili wa nafasi 70 za kazi katika Idara ya Uhamiaji, ni ishara kuwa bomu la ajira litalipuka muda wowote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya Viwanja vya Bunge, Lowassa alisema Serikali ni lazima ihakikishe inatengeneza ajira kwa kuwa kila mwaka zaidi ya vijana 30,000 wanahitimu katika vyuo mbalimbali nchini.

Wasomi hao wa fani mbalimbali walijitokeza katika uwanja huo Ijumaa iliyopita, kuanzia saa 12 asubuhi wakisubiri kufanyiwa usaili huo.

Lowassa ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008, amenukuliwa mara nyingi akiitaka Serikali kuchukua hatua kukabiliana na tatizo la ajira na akisema ni bomu linalosubiri kulipuka.

Mbunge huyo wa Monduli kupitia CCM, aliwahi kuingia kwenye malumbano makali na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka kuhusiana na suala la ajira kwa vijana.

Kabaka akiwa bungeni, Machi 21, 2012 alitoa takwimu za namna Serikali ilivyokuwa inatengeneza ajira kwa nia ya kumjibu Lowassa, ambaye alikuwa ameeleza tatizo la ajira linavyowaathiri vijana.

Jana, Lowassa kuongezeka kwa makundi ya vijana wanaopora watu katika maeneo mbalimbali nchini ni ishara ya ukosefu wa ajira. “Watanzania sasa tupo milioni 48 na kila mwaka vijana zaidi ya 30,000 wanahitimu vyuo vikuu na kazi hakuna, pamoja na hilo hatuambiwi ni vijana wangapi ambao hawana kazi,” alisema Lowassa.

Alisema lazima Serikali itengeneze ajira kwa wananchi wake, huku akimtolea mfano Rais wa Marekani, Barack Obama kwamba alishinda awamu ya pili kwa sababu ya kutengeneza ajira.

“Mfano mzuri ni katika uanzishwaji wa viwanda. Tunapofikiria kuanzisha kiwanda cha pamba kwanza lazima tuangalie tutatengeneza ajira ngapi,” alisema.

Katika kuonyesha kuwa ajira sasa ni tatizo nchini, juzi jioni wakati wa mjadala wa Bajeti Kuu, Naibu Spika Job Ndugai alisema Mtanzania mwenye nia ya kugombea urais mwaka 2015 ili aweze kuelekewa kwa wananchi ni lazima aeleze mikakati ya kuwasaidia vijana kupata ajira.

“Ajira ni tatizo kubwa na lazima lishughulikiwe. Kuna vijana hawaendi shule lazima watazamwe. Kuna wanaomaliza darasa la saba, kidato cha nne, cha sita na vyuo vikuu.

Nazungumza kutoka moyoni kabisa. Hizi ni dakika za mwisho za Serikali ya awamu ya nne, wale wanaojipanga kwa awamu ya tano kama hawataongelea ajira basi waandike wameumia.”

Ndugai alisema vijana wasio na kazi ndiyo wapigakura wakubwa na kusisitiza kuwa mgombea yeyote makini ni lazima afikirie suala la ajira kwa vijana.

 Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema: “Vijana 10,500 kufanya usaili wa nafasi 70 ni janga la taifa. Yupo kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM aliwahi kulizungumza hili lakini akapondwa kwamba anazungumza mambo kwa kuzua. Sasa huu ndiyo ukweli wenyewe.”
Credit: Mwananchi
Tags

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duuuuuuuuuh! kwel ajira bongo ni majangaaaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  2. bongo ajira ni kwaajili ya wachina cc 2komae na guta maana hata bodaboda saiv ni majaaaaaangaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  3. Lowasa uliajiri wangapi pindi wakati wewe ni waziri mkuu acha kuilaani nchi hapa hakuna cha bomukulipuka labuda utalipuka mwenyewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. IV WW huna akili timamu, lowasa alikaa muda mfupi but tayali alishaanza kuweka mambo sawa so unajuaje kama hilo lilikuwa kwenye plan yake mfano mzur alianzisha shule za kata unazani mwenyewe angekuwepo shule za kata zingezarauliwa? Bt mrith wake boomu

      Delete
  4. Tunahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa wa kupambanua na kutoa maamuzi hata kama ni magumu kama Lowassa naamini ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa sana wa maamuzi binafsi hata kama wenzake wakimpinga huwa hajali maana anajua anachokuwa amekilenga

    ReplyDelete
  5. Tusubiri 2015 maanina zenu ccm

    ReplyDelete
  6. Anajifanyia kampeni mumpe urais Huyo ale vizuri na kina Freddy na kina Pamela lowasa

    ReplyDelete
  7. Huyu akipata urais tutakoma mkewe anaringaaaa na roho Yake mbaya.

    ReplyDelete
  8. Hayo yako watanzania wanamkubali

    ReplyDelete
  9. Nasirdin,mejankunda,jigril,baby komba,mmemsia mtarajiwa?......roasa hoyeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. ninachotaka kujua mhs lowasa ni mikakati gani utafanya kuboresha ajira kwa vijana, maanake kila siku unalaumu tu, lakini hatusikii ukisema kama ukipata uraisi utafanya nini, kulitatua hilo bomu!!! jamani watanzania tumechoka kupambazwa na ujinga wa wanasiasa kutaka uraisi ilikuja jinufaisha binafsi, tunajua unataka uraisi ili uje linda mali zako tu.

    ReplyDelete
  11. wewe bwege kaa kimya unazani yeye mjinga mpk aongee teknik zake za kutatua ajira ili mwingine aibe ,mpeni nchi ndio mtajua acheni roho mbaya za kufata mkumbo ngedere ww unazani ana dhiki kama viongozi wengine

    ReplyDelete
  12. ILA kila nikiangalia nani ataifa nchi hii mi naona lowasa asee, wampe hata hiyo miaka mitano ya mwanzo tuone

    ReplyDelete
  13. ndiyo hizo akili za shule za kata alizokuanzishieni ndizo zinafanya akili zenu kuwa matope hivi, sasa matusi ya nini? wewe utakuwa mmojawapo uliofaidika na hizo shule za kata! hongera mdau!.

    ReplyDelete
  14. Duuu AMA kweli aliyenacho anazidi ongezewa,lowassa mnampa urais?haya

    ReplyDelete
  15. Yaani huyu anashida kweli na huo urais halali usiku yeye na urais..yaani hili fisadi tumeshalishtukia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa kimya WW bwege ulitaka amfikirie Baba yako,nyoo

      Delete
  16. ni Mungu ndiye atakayetupa raisi, akitupa lowassa, basi ndiyo ameula, lakini sidhani sababu watu wako wengi tu wenye maadili, wewe mdau unaotukana wenzako na kuwaita mabwege, wewe ndiyo bwege namba moja, sijui huyu lowasa unamshabikia kwanini?

    ReplyDelete
  17. HATA HIZO 70 WAMESHAPEANA KWA VIMEMO

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad