Majibu ya Ridhiwani Kikwete kuhusu NEC na kwa wanaosema anamiliki vituo vya mafuta.

Inawezekana hili likawa moja kati ya maswali uliyonayo na hujawahi kupata nafasi ya kumuuliza muhusika au inawezekana ikawa ni ishu ambayo umewahi kuisikia au kuisoma kwenye chombo chochote cha habari.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwenye exclusive interview na millardayo.com anasema >>> ‘kuwa mtoto wa Rais changamoto kubwa ambayo nimeiona mojawapo ni watu kukupa tafsiri ya vitu vingine ambavyo wewe huvijui, kumekua na malalamiko mengi sana kwamba huyu jamaa ana mali hizi na hizi’
‘Wanasema kampuni za mafuta, Oil Com, Camel Oil na Lake Oil ni za kwangu, sasa unajiuliza huyo mtu ambae anaweza akatengeneza kampuni tatu zinazofanya shughuli moja kwa nini asianzishe kampuni moja ikawa kubwa zaidi ?? kwa hiyo kumekua na manenomaneno mengi, hizo ni changamoto mfano kwenye siasa huku, watu wengi aidha hawajui nimetokea wapi au wanajitoa akili katika maana kwamba hawataki kujua nimetoka wapi’

‘Kuna kipindi unaweza ukashangaa Mwandishi wa habari anachukua kalamu anaandika maneno mpaka unashangaa kayatolea wapi? sitaki kuamini kwamba Mwandishi unaweza kuandika kwamba Ridhiwani kapata UNEC kwa sababu ya baba yake, ungechukua muda ukamsoma Ridhiwani vizuri ukauliza watu waliokaa na Ridhiwani, uliza huyu ameshawahi kuwa kiongozi??’
‘Wako watu ambao kwa kuwa wamemjua Ridhiwani baada ya Jakaya Kikwete kuingia Ikulu basi nao wanaanzia hapohapo Ikulu lakini hawajui Ridhiwani kabla ya baba yake hajawa Ikulu alikua anaishije, mimi nimekua naishi maisha ya kawaida nimekaa boarding school nimesoma Mkwawa baba yangu akiwa Waziri, nilikua na uwezo wa kwenda kusoma Ulaya lakini nimesoma chuo kikuu Dar es salaam pale japo nilikua na uwezo wa kwenda popote pale ninapotaka ila ni kwa sababu tu mzee wangu alitaka kuona naishi kama watu wengine’
Tags

Post a Comment

23 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hujajibu hoja,hujaondoa.kiu ya watanzania kujua chanzo cha utajiri wako,japo umetaja makampuni matatu ya mafuta kutuchanganya.Ridhiwan tuambie uhusika wako kwenye Lake Oil inayoendeshwa na mpambe na rafiki yako Mosha.Pia ni kwa vipi unahusika na uporaji wa shirika letu la umma la UDA kwa bei ya kutupa?.Iweje Tanganyika kazi ni moja tu,kuiba na kukana,imagine mpaka leo haijulikani ni nani mmiliki wa Richmond,Deep Green,Kagoda na kampuni kibao za kitapeli?

    ReplyDelete
  2. Ridhiwani kwa nini ni wewe tu na mama yako Salma kwa mara ya kwanza Tanzania nzima,ndo mliingia NEC bila ya kupigiwa kura eti mlipita bila kupingwa?

    ReplyDelete
  3. Uday saddam Hussein,Gamal Hosni Mubaraka,Major General Kainerugaba Yoweri Museveni,Bilionare Gideon Arap Moi, Qussay al-islam Saddam Hussein, Saif Al-Islam Gaddaffi

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete tayari huna kosa lakini unazo hizo tuhuma za ufisadi, maelezo yako hayatoshi kabisa kukuweka nje ya tuhuma hizo zilizotapakaa nchi nzima kuwa una utajiri wa kutisha. Kitaaruma wewe ni mwanasheria, unatakiwa maelezo yako yatuondolee mashaka ya tuhuma hizi, jitakase, jitakatifishe tukulejeshe katika kundi la wengi la WAKULIMA NA WAFANYAKAZI TULIOPORWA CCM YETU>

    ReplyDelete
  5. Mambo yakurisishana nchi hayo Tanzania zaidi yauijuavyo wht next kulahela mpaka uridhike.uongozi mmemchagua wenyewe so stay tuned

    ReplyDelete
  6. Mdogo wangu hapo umechokoza nyuki . Wajanja wenye kujua u

    dokozi wanakaaga kimya wanapochokonolewa mambo yao.....Umelikoroga dogooo.;

    ReplyDelete
  7. wewe kijana mzimu wa mwalimu unakusikia utakufa kifo kibaya sana wewe na familia yako yaani baba namama yako kwa kuwaibia watanzania wanyonge bila huruma.

    ReplyDelete
  8. ukweli nikwamba bado kiu ya mtanzania hujaitoa tunaomba ueleze kwa undani tukuelewe mbona umetaja hzo kampuni lakini hujafafanua kuwa ni zako au sizako silazima kampuni iwe na jina moja kubwa kwani unaweza ukatofautisha majina kwa sababu nyingi tu kwahiyo tuambie kuweli wewekama hizo kampuni sio zako kwa kutueleza kwa makini sio kutupiga danadana

    ReplyDelete
  9. Watz wa sasa sio wa mwaka 47 we Ridhiwan na babako Kikwete na Salma wote wezi tu

    ReplyDelete
  10. Tena umechukua tenda ya kununua mbaazi za wakulima wote babati na kuzuia wanunuz wengne na umeshusha bei toka sh 1000 hadi 600 kwa kilo ucvyo na huruma

    ReplyDelete
  11. WATANZANIA NI WAPUMBAVUU NAN ALIWATUMA MMCHAGUE HUYU KUKU MANA BABA AKE KAWAIBIA NA YY MNAMPA AIBEE SO WHAT NEXT KM SIO KURISISHA NCH MIKONON MWA KIKWETE FAMILY HUYU DOGO ANAKOELEKEA ATAKUA WAZIRI SUBIRIN MWONE MIAKA IJAYOO MTAJUUTA LABA LOWASSA ACHUKUE NCHI LKN KAMA HATACHUKUA HUYU DOGO ATAWAKALIA BABAYA BADAE..I HATE JAKAYA AND HIS FAMILY TO HELL

    ReplyDelete
  12. Ridhiwani siku ccm ikiangushwa hapa.patachimbika,itabidi ujiue au ukimbilie ughaibuni ww 'a familia.yako.

    ReplyDelete
  13. Nani sio mwizi? Acheni roho ndogo. Btw..hatuwezi kuwa sawa. Mnategemea mtoto wa Rais awe sawa na mkulima? ,nchi gani duniani iko hivo..acheni pressure

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni mtoto gani wa mwl.Nyerere ni tajiri?

      Delete
    2. Matatizo yao binafsi. Mwaya Riz songa mbele. Tunakujua ulikuwa kiongozi toka chuo na tulikuwa tunapanda daladala wote..kamua kama inawezekana

      Delete
  14. umdhaniaye kumbe siyo

    ReplyDelete
  15. Bila CCM tutayumba. Kamua Ridhiwani. if they can na wao waibe. as for ww kuwa mtt wa Rais na baadae km kuwa waziri nn shida. Baba na Mtoto Bush wa marekani wote walikuwa maraisi. Je Jk angekuwa daktari na Ridhiwani Nesi wangegoma kudundwa sindano. Acheni porrojaaa

    ReplyDelete
  16. tatizo uyu raisi anakopi kutoka marekani uku aangalii nchi yetu changa sana sisi yetu macho atuna nguvu ila ile wao

    ReplyDelete
  17. we subil tu atasema yote maisha ya watanzania yanawalilia

    ReplyDelete
  18. non sense hakuna hoja za msingi.........wasomi gani hawa

    ReplyDelete
  19. m naona upumbavu kusema riz anamiliki oil com na camoil au lake oil hapa tufanye mpango wa ss watz wakawaida kuwatoa hao watawala fake

    ReplyDelete
  20. Lowasa akipewa nchi basi twafa,hyujamaa ni Sumu,ndg n'a Kagamé,waulizewaliowahifanyakazi mbulu nasehemunyingine

    mnauliza utajili?mtotowa nyoka nyoka tu,wanabank comoro,Richmond ya lwasa n'a kikwete. Fungukeni shika silaha.mwanasheriagani hajibuhoja?weziwote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad