Makahaba wa Kinyarwanda Wanaswa Dodoma Wakinyemelea Wabunge

Wanawake wanne raia wa Rwanda wametiwa mbaroni mjini Dodoma kutokana na kuingia nchini kinyemela na kujihusisha na biashara ya ukahaba.
Watuhumiwa  watatu kati ya hao, Saidat  Umotoni (28), Asha Abimana (25) na Asia Umotoni  Wase (30), hii ni mara yao ya pili kukamatwa mjini hapa wakidaiwa kujihusisha na biashara hiyo.
Mara ya kwanza ilikuwa Novemba mwaka jana ambapo wote  ( Asia, Asha na Saidat) baada ya kukamatwa, walirudishwa kwao baada ya kulipa faini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma,  Proches Kuoko, alimtaja mwingine aliyekamatwa ni Chalote Uwase (28) ambaye ameshahukumiwa kifungo cha miaka miwili anachotumikia katika Gereza la Isanga, mjini hapa.
Alisema wahamiaji hao wote kwa pamoja walikamatwa na maofisa wa kikosi cha Uhamiaji, baada ya kupata taarifa kwa kuwepo raia hao katika eneo la barabara ya Bahi ndani ya Manispaa ya Dodoma.

Alisema wanawake hao walikamatwa  usiku kwenye mitaa hiyo huku wakiwa kwenye harakati za kutafuta  wateja na walipohojiwa wote kwa pamoja hawakuwa na hati ya kusafiria na kuishi hapa nchini na walizokuwanazo zilikuwa zimeisha muda wake wa matumizi.
“Hata  walipopekuliwa,  walikutwa wakiwa na hati ya kusafiria iliyokuwa imeisha muda wake wa kuwawezesha kuishi hapa nchini na walipohojiwa zaidi walisema wao kazi yao ni uchangudoa,”alisema Kuoko.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa nini wanawafukuza na wakati wabunge wanashida ya mademu we huoni wkina komba wanachukua vijukuu labda kuna mheshimiwa alinyimwa ndio maana wamewsanuria

    ReplyDelete
  2. kweli kuna mbunge atakuwa kaomba kanyimwa

    ReplyDelete
  3. Wengi wao wanakuja kutafiti,ulinzi wa Tanzania,sio kama tunavyo fikiri,uhamiaji wawe makini sana,chochote kinaweza kutokea kwa viongozi wetu,nchi iwe makini,wako kazini ,kuichunguza bongo,wengi wana kuja kama wafanya biashara tuwe makini sana,Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Wote hao ni makachero wa.Kagame,hata.mashoga wa kinyaruwanda pia wapo dodoma kwa ajili ya waheshimiwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad