Mama Amkubatia kwa Upendo Mahakamani Mtu Aliyemuua Mwanae

Uchungu wa mwana aujuae mzazi, na ukitaka kujua thamani ya mtoto kwa mama hatarisha maisha yake. Lakini hii imekuwa tofauti kwa mama huyu aliyezingatia sababu ya kifo cha mwanae.

Mwanamke mmoja wa Florida, Marekani ameonesha moyo wa huruma na uelewa alipokuwa mahakamani baada ya kumkumbatia kwa upendo Jordyn Howe mwenye miaka 16 baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kufyatua risasi mwaka 2012.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo, Howe alikuwa na umri wa miaka 14 aliichukua bastola ya baba yake wa kambo na kwenda nayo shuleni ambapo alifika na kuanza kumfanyia utani rafiki yake aitwa Lourdes Guzman –DeJesus aliyekuwa na miaka 13.

Howe alijaribu kufyatua risasi chini kwenye ardhi na bahati nzuri hakuna kilichofanyika na risasi haikutoka, baada ya kuona hivyo alimnyooshea bunduki rafiki yake kiutani lakini wakati huu alipofyatua risasi ilitoka kweli na kumpiga Lourdes, tukio lililopelekea kifo chake.

Baada ya kusomewa mashitaka mtoto huyo alikiri mara moja kufanya kosa na kumuua rafiki yake na kisha kuomba msahama.

“Nasikitika kwa kumuondoa na naomba radhi kwa kufanya kile nilichokifanya.” Alisema.

Maelezo ya mama huyo yalimuingia moyoni na ikambini aseme huku akiishiwa maneno.

“Ni uzoefu unaoumiza sana.” Alizungumza huku akiwa anatetemeka mikono. “Wazazi wawili hawatakiwi….hapana…siwezi.”

Mtoto huyo alipewa kifungo cha miezi 22 gerezani. Mwanzoni mama wa mtoto aliyepigwa risasi aliitaka mahakama kumpa adhabu kali, lakini baada ya maelezo hayo alibadili msimamo na kumkumbatia mtoto huyo kisha kuzungumza na hakimu namna nyingine ya kuyamaliza.

Hakimu aliamuru mtoto huyo kutumia mwaka mmoja katika kituo/mahakama ya watoto na kisha yeye na mama huyo watapewa nafasi ya kuzunguka Florida wakihamasisha watu kuachana na matumizi ya silaha za moto.

“Nimemsamehe kwa sababu nimekuwa na amani, kwa sababu nahisi kama binti yangu sasa hivi yuko katika sehemu ya amani. Siwezi kumrudisha mwanangu, lakini angalau naweza kulitunza jina lake kuwa hai.” Alisema mama huyo.
udakuspecially.com

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. god bless you, and give you strength, few people has got such hurt . God is inside your heart

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad