Man United yaingia Mkenge kwa Moyes

KWELI Manchester United iliingia mkenge kwa David Moyes baada ya kila kitu alichokifanya klabu hapo kugeuka kuwa majanga.

Baada ya kocha huyo kuisababisha hasara kubwa ya kupoteza mamilioni ya pesa kutokana na kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya miamba hiyo ya Old Trafford itapata hasara kubwa kwa kiungo wao Marouane Fellaini, ambaye alisajiliwa na kocha huyo.

Kocha Mkuu mpya wa kikosi hicho, Louis van Gaal amesema haoni kama kiungo huyo anaweza kupata nafasi kwenye timu hiyo msimu ujao na kwamba yupo sokoni kwa pauni 15 milioni kitu ambacho kitaifanya Man United kuingia hasara ya pauni 12.5 milioni.

Fellaini alinunuliwa na Moyes mwaka jana kwa ada ya pauni 27.5 milioni, lakini kwa msimu mzima aliocheza kwenye kikosi hicho cha Man United hakufunga bao hata moja kitendo kinachomfanya kocha mpya, Van Gaal afichue bayana kwamba atakapoingia Old Trafford basi hamtaki mchezaji huyo.

Kiungo huyo Mbelgiji kwa sasa yupo kwenye fainali za Kombe la Dunia na kikosi cha Ubelgiji nchini Brazil na kitu kipekee kitakachomfanya aendelee kubaki Old Trafford msimu ujao kama atafanya kweli kwenye fainali hizo.

Hata hivyo, licha ya Man United kukubali kumuuza kwa hasara, hakuna klabu yoyote iliyojitokeza kutaka kumsajili kiungo huyo kitendo kijachothibitisha kwamba mzigo huo bado unaikabili timu hiyo.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Im not a coach but Fellain has no quality to play for Man u

    ReplyDelete
  2. Moyes was a stupid coach! manutd had never playd defensive approach tactics under Fergy but rather aggressive play. He bought fellaini for ths same approach expctng hm to mayb hold the ball. such a waste. Paka shume, nawasilisha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad