Maskini Watu Wengine 30 Wauwawa Kenya kwa Shambulio la Kigaidi

WATU zaidi ya 30 wameuawa, hoteli mbili, kituo cha polisi na kituo cha mafuta kuchomwa moto baada ya shambulio lililotokea eneo la Mpeketoni, Lamu nchini Kenya jana usiku.

Kituo cha Polisi cha Mpeketoni, hoteli ya Breeze View na Taweel ndivyo vilivyochomwa moto na moshi ulikuwa bado unafuka asubuhi hii.

Imeelezwa kuwa washambuliaji walitokomea na silaha na magari ya polisi kutoka kutuo hicho cha polisi baada ya kushambulia.

Awali washambuliaji hao waliteka daladala mbili 'matatu' eneo la Witu kabla ya kufanya shambulio hilo.

Wananchi walikimbilia katika nyumba zao wakati polisi wakijibizana risasi na magaidi hao ambapo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo anadai kusikia washambuliaji hao wakisema "ambieni baba yenu atoe jeshi Somalia” wakimaanisha wamwambie Rais Kenyatta aondoe jeshi nchini Somalia.

Makundi ya Al Shabaab na MRC militia yanadaiwa kuhusika na shambulio hilo

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sio ugaidi, ni kupigana kuutetea uis...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huo uislamu unaotetewa umedhulumiwa nini?

      Delete
  2. Umedhulumiwa wanawake wanaobakwa na majeshi ya kenya huko somalia na kuwauwa wanawake na watoto laana kum ww

    ReplyDelete
  3. Bado tanzania sasa mungu tunusuru maana serikali imewapoke wasomali 1500 uko tanga, je na serikali ya tz ikipeleka jeshi au kuingilia ugomvi wa alshabaab na kenya si nawao watatugeuzia kibao!! Kazi ipo jamani!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad