Maskini:Utumbo wa Pacha Aliyekuwa Ameungana na Mwenzake Uko Nje

Mmoja wa watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana na kutenganishwa kwa upasuaji nchini India, hali yake ni mbaya na utumbo wake mkubwa sasa umetoka nje.

Mtoto huyo Eliud Mwakyusa na mwenzake Elikana walizaliwa Februari 20, 2013, Kyela, Mbeya wakiwa wameungana kiunoni na Serikali iliwapeleka India ambako walitenganishwa.

Walirejea Februari, mwaka huu na kusherehekea siku yao ya kuzaliwa wakiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili walikofikia baada ya kutoka India katika hafla iliyoandaliwa na gazeti hili.

Hata hivyo, siku chache baada ya watoto hao kurejea kijijini kwao Kasumulu maarufu kwa jina la Juakali, Kyela, afya ya Eliud ilianza kubadilika baada ya sehemu kubwa ya utumbo wake mpana kuanza kutokeza nje.

Utumbo wa mtoto huyo umetoka nje kupitia tundu lililoachwa na madaktari jirani na kitovu chake kwa ajili ya kutolea haja kubwa.

Wakizungumza na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki nyumbani kwao, wazazi wa watoto hao, Grace Joel na Eric Mwakyusa walisema tatizo la Eliud lilianza mwezi mmoja uliopita.

Grace alisema hali hiyo imesababisha mwanaye aanze kudhoofika naye akiwa hajui cha kufanya kutokana na hospitali iliyowafanyia upasuaji kuwa mbali.

Alisema baada ya kutenganishwa walitengenezewa mirija maalumu ya kutolea haja. “...Waliingiza kwa ndani na kubakiza kidogo nje ya tumbo kwa ajili ya kutolea haja kubwa. Hivyo baada ya kuanza kuugua akawa anatapika na anapotapika utumbo huu ukawa unatoka nje kidogokidogo kama unavyoona,” alisema huku akionyesha utumbo huo.

Alisema kuwa hali hiyo ya utumbo kutoka nje iliwahi kumtokea mtoto huyo hata wakiwa bado hospitalini nchini India, lakini haikuleta madhara yoyote.

Mama huyo alisema afya ya Eliud imekuwa ikidhoofu kila kukicha na sasa imefikia hatua anashindwa kukaa peke yake tofauti na aliporejea kutoka India.

Mwenzake aendelea vizuri

Afya ya pacha mwenzake, Elikana ni nzuri na muda mwingi amekuwa akikaa na bibi yake mzaa baba, Subira Kasekele.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ee Mungu mtazame malaika wako huyo.Fanya muujiza baba juu ya mtoto huyo.

    ReplyDelete
  2. Naomba serikali isichoke kuhudumia huyu kiumbe kwani anataabika

    ReplyDelete
  3. Eemungu saidia mtoto apone Amin.

    ReplyDelete
  4. Kwel serkar tunaomba msichoke kumsaidia mtoto huyo anateseka

    ReplyDelete
  5. Mungu tenda muujuza wako mtoto apone,pia endelea kunitunzia na mm mapacha wangu alvan na alvis

    ReplyDelete
  6. Ee Mungu baba nakuomba umtazame mtoto huyu na umponye kwa jina lako kwani hakuna liclowezekana kwako Amina.

    ReplyDelete
  7. Serikali naomba msichoke tafuteni namna ya kumsaidia mtoto huyo ikiwezekana mrudisheni india yawezekana tatizo likawa c kubwa sana waweza muokoa! TAFADHALI SERIKALI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad