Mbasha 'Bora nijiue Sipo Tayari Kupata Aibu. 'Mke Wangu Amekuwa Tatizo Kwenye Ndoa Yetu'

Upande wa pili wa shilingi! Kwa mara ya kwanza tangu ahusishwe na skendo ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17, mume wa mwimbaji wa Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameibuka na kuzungumza na Uwazi katika mahojiano maalum dhidi ya kashfa yake hiyo huku akitishia kujiua.

Akizungumza kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa moja mwishoni mwa wiki iliyopita huku akikanusha kukimbilia mafichoni baada ya kuondoka nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar hivi karibuni, Mbasha ambaye pia ni mwimba Injili kama mkewe, alianika kila kitu akidai cha siri kwamba anajua anachezewa mchezo mchafu baada kuwepo kwa gogoro zito kati yake na mkewe hadi kutishia uhai wa ndoa yao.

ASIMULIA TUHUMA
“Tuhuma zilizoripotiwa na binti aitwaye... (anamtaja jina) ambaye kweli ni ndugu wa mke wangu (Flora) kwenye Kituo cha Polisi Tabata-Shule (Dar) si za kweli.
“Anayefanya mambo hayo yote ni mke wangu, anataka nipotee ili awe huru. Mimi najua hilo.”

KASHFA YA KUTENGENEZA
“Hii kashfa ni ya kutengeneza ili nipotee lakini sipo tayari kupata aibu, bora nijiue.
“Mke wangu amekuwa tatizo kwenye ndoa yetu.
“Kweli ndoa yangu na Flora ina matatizo lakini matatizo yetu ya ndani sana hakuwa na sababu ya ‘kuinjinia’ mpango mchafu wa kunimalizia gerezani mimi ili yeye aponde raha.
“Nyuma ya haya mambo kuna vitu mtu ukivisema ni aibu sana kwa upande wa pili. Lakini navijua.”

MKE ALIONDOKA NYUMBANI
“Mke wangu aliondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini. Hebu fikiria hapo. Mwanzo alianza kwenda ‘gym’ saa 11:00 alfajiri na kurudi saa 4:00 asubuhi. Pia saa 10:00 jioni aliondoka tenda kwenda gym akawa anarudi kati ya saa 3:00 hadi 4:00 usiku.

“Nilipomuuliza alinijibu kuwa ni kwa sababu anatembea umbali mrefu. Hebu ona sababu ilivyo dhaifu jamani! Hata kama ungekuwa wewe mwandishi, unaonaje?”
“Mimi ni mtu maarufu, ningetaka mwanamke ningepata, iweje nibake?

“Jaribu kufikiria, katika tatizo kubwa kama hili ambalo linaweza kunifanya nifungwe, nilitarajia mke wangu awe upande wangu, lakini cha ajabu yeye ndiye amekuwa nyuma ya adui zangu, niamini nini mimi zaidi ya yeye kuhusika na kuniangamiza?”
“Hausigeli wangu ni mzuri, kwa nini nisimbake yeye?”

AFUATILIA
“Nilipofuatilia niligundua tayari kuna tatizo kwenye ndoa yetu. Mdudu alikuwa ameingia ndani ya ndoa kwani hadi sasa mke wangu siishi naye. Anaishi hotelini.
“Anachokifanya mke wangu ni kitu kibaya mno. Alimtengeza yule binti ambaye nilikuwa namsomesha sekondari pale (anataja shule maarufu Dar), akampa semina ya kutosha kwamba aseme nimembaka ili nipate misukosuko na yeye awe huru.

“Kama hiyo haitoshi, akala dili na madaktari,  wakafoji majibu ya vipimo vikionesha kweli yule binti ameingiliwa, sasa sijui kama vipimo vilioneshaje kama ni mimi.
“Ukweli ni kwamba siwezi kuvumilia kuona napandishiwa kizimbani kwa jambo la kutengenezewa.
“Napiga picha nitakapofikishwa mahakamani jinsi ambavyo vyombo vya habari vitakavyoandika na picha zangu kwa kesi ya ubakaji ambayo si ya kweli.

“Dah! Inaniuma sana. Mke wangu nimemfanyia vitu vingi sana. Hakustahili kunitendea ubaya huu. Alikuwa hafahamiani na mtu yeyote mkubwa. Mimi ndiye nimempeleka kwa watu wakubwa wakamsaidia sasa amenigeuka, siamini. Narudia tena, heri kufa kuliko fedheha hii,” alisema Mbasha kwa uchungu.

HAYUKO MAFICHONI
Kuhusu kuwa mafichoni, Mbasha alisema: “Sipo mafichoni, sijaambiwa na mtu yeyote nikatoe maelezo polisi. Nipo nimejaa tele, nikiambiwa nahitajika nitakwenda kutoa maelezo yangu kwani sijawahi kutenda kosa hilo na Mungu awe shahidi yangu.”

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Dar, Marietha Minangi alithibisha kuwepo kwa ishu hiyo na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea.
Flora na Mbasha walifunga ndoa Agosti 22, 2002 hivyo mwaka huu wametimiza miaka 12 wakiwa pamoja ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Elizabeth.
Stori: Sifael Paul na MAKONGORO OGING’,GPL

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbasha mungu huwa haji nahakamani kutoa ushahidi bwanaaaa!!!!na mahakama huwa haihukumu bila kysikiluza pande mbili,unaogopa nini?hayo uliyomfanyia mkeo yanamhusu yeye siyo jamii na unaarufu ni wakwak,subiri upelelezi ukamilike kama kupanda kizimbani upande then ushahidi upimwe mambo yaishe,walipanda kizimbani watu maarufu wa kweli kina clinton sebuse wewe?

    ReplyDelete
  2. nenda na wewe wakupime kama ni kweli itajulikana kwenye vipimo usiende mahakamani bila ya kupimwa

    ReplyDelete
  3. USIJIUE MBASHA, KWA KUWA NYINYI NI WATUMISHI WA MUNGU, MUNGU ANAWASIKILIZA SANA KULIKO WATUMISHI WA DUNIA HII

    NI MAJARIBU YAMEKUIJIA, NA YANA MLANGO WA KUTOKEA, SISEMI UMEBAKA AU HUKUBAKA, ILA HATA KAMA MAHAKAMA ITAKUPATA NA HATIA, USIJIUE ILA MWACHIE MUNGU ASHUGHULIKE NA FROLA

    HAKUNA AIBU KUBWA KAMA ALIYOIPATA YESU, NA KUPITIA HIYO IMEFUTA AIBU ZOTE KWA WATUMISHI WA MUNGU

    AMIN AMIN NAKUAMBIA, KAMA KWELI HUKUBAKA, HILO SWALA NI JEPESI MNO

    ReplyDelete
  4. Ukienda mahakamani umekula kifungo cha maisha muulize babu seya najua mtakutana huko na kuna mabasha lazima watakufira na wewe.

    ReplyDelete
  5. hee siamin kama frola anaweza kufanya unyama huu mwee. jikaze babaa penye ukweli uongo hujitenga!

    ReplyDelete
  6. Hayo nimapito tu ya duniani wala yasikutie hofu mwanaume lazma upoganie ukweli wako na wala ckujiua huyo mkeo kuna mtu anamparaha huko hotelini sasa ww muombe mungu sana akutiw nguvu na uyayashinda yotw ktk bwana.

    ReplyDelete
  7. Kwa ushauri wangu ni bora utoroke lasivyo jela inakuita kweupe fanya hima kimbia nchini mbasha sijui unasubiri nini maskini

    ReplyDelete
  8. ukwel mnaujua nyinyi wenyewe ndan ya nafc zenu,ila n vzur kufanya vtu ambavyo hamtavijutia cku zijazo

    ReplyDelete
  9. Frola chukua nyimbo zote zifungie kwny trunker hamna dini wala fundisho toka kwako mtumishi malaya gym si tunaenda hamna ya masaa yote hayo. Shame on you

    ReplyDelete
  10. jamanii, dunia ina mambo, haya ngoja tusubir tuone mwisho wa hii story ni nini.

    ReplyDelete
  11. Mbasha unaweza kua umemfanyia mengi sana mkeo flora na akajua hayo yote lkn ukaja ukamfanyia unyama mdogo tuu ukakuangamiza wewe wanaume kuen makin sana na wanawake waangalien vizuri mana wao ndo wana funguo wa maisha yenu..km ulimtenda kidogo na kumuumiza kwa mda mfupi usitegemee km atakusamehe mana inaonekana mkeo analipa kisas na inaonekana kuna kitu umemuumiza nachoo wewe wanaume ndo hua chanzo sie wanawake hua tunamalizia tuu na ndo tunaonekana wabaya lkn kumbuken jkua wanaume wengi ni tatizo ktk ndoa lkn mwanamke anapofanya jambo zito inaonekana kua yy ndo mbaya ....mbasha utaozea jela kama ulimuuza flora.

    ReplyDelete
  12. Tena Ww muhubiri ni handsome kuliko kuliko huyo mkeo hebu mpige nachini uchukue mrembo mwengine ulebata mambo yakuhubiri tena uyaache laasivo kilasiku ukenda kuhubiri huku mwenzio nae anaenda gym

    ReplyDelete
  13. Kama ni kweli Mchungaji Gwajima ndie anayeikoroga ndoa yako na flora kwa kumpeleka gym,kumnunulia gari,kumpangishia chumba hotelini ya bei mbaya na hata kumuhifadhi nyumbani kwake anayedai kubakwa,basi, Gwajima na alaaniwe duniani na mbinguni!

    ReplyDelete
  14. Flora kama umejiingiza kwenye skendo kama za masuperstaa wa bongo muvi na bongo fleva umekwisha.Nyimbo za injili zinafungamana na imani,nani atakusikiliza kama umehamia hotelini kula uroda?

    ReplyDelete
  15. Flora umepata mafanikio unafanya ujinga ngoja uone saasa kama yesu unamtumia kwa style hiyo anakutoa nishai.....mra nyingi mwanamke akitoka nje ya ndoa......hua akukaliki ndani kuna moto hua unaxunguka na si utamu wa yesu...0717337536

    ReplyDelete
  16. Hata mimi nakushauri husijiue,ila piga chini huyo demu mnafki.Chukua dem mwingine akuliwaze

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad