MBASHA: Maisha ya Jela hayafai kabisa.

Kufuatia  Mahakama  ya  Ilala  jijini  Dar  kumuachia  kwa  dhamaa  Emmanuel  Mbasha  ambaye  ni  mume  wa  muimbaji  wa  nyimbo  za  Injili  maarufu  nchini  Flora  Mbasha  anayekabiliwa  na  tuhuma  nzito  za  kumbaka  mdogo  wa    mkewe, inaelezwa  kuwa  siku  moja  tu  aliyokaa  mahabusu  ilimfanya  kubadilika  muonekano  kutokana  na  kudhoofika…..

Emmanuel  Mbasha  ambaye  alifikishwa  mahakamani  kwa  mara  ya  kwanza  juni  17  mwaka  huu  na  kukosa dhamana  kutokana  na  kushindwa  kutimiza  mashariti, alilazimika  kutupwa  mahabusu  katika  gereza  la  Keko, kabla  ya  juni  19  kupandishwa  tena  kizimbani  ambapo  aliachiwa  kwa  dhamana  baada  ya  kutimiza  masharti  hayo….

Baadhi  ya  watu  ambao  walimshuhudia  Mbasha  katika  viunga  vya  mahakama  hiyo  walioneklana  kulengwa  na  machozi  huku  wengine  wakitamka  kwamba  wanamuachia  Mungu

Mume  huyo  wa  Flora  aliwasikitisha  zaidi  watu  kutokana  na  kuwa  na  mawazo  mengi  huku  miguuni  akiwa  amevaa  malapa  ambayo  thamani  yake  haizidi  sh. 2000  wakati    katika  hali  ya  kawaida  huwa  anavaa  mavazi  ya  bei  mbaya  na  kujiweka  msafi  muda  wote…..

“Maskini  Imma  amevaa  ndala  na  amekonda.Hakika  yupo  katika  kipindi  kigumu  sana. Jela  mtu  hukonda  siku  moja  tu.Jela siyo  kuzuri  hata  hata  kidogo,”  alisema  raia  mmoja  nje  ya  mahakama  hiyo.

Hakimu  aliyesikiliza  kesi  hiyo  Wilberforce  Luhwago  aliahirisha  kesi  hiyo  hadi  July  17  mwaka  huu  itakapo tajwa  tena…..

Baada  ya  kuachiwa, Mbasha  alitoka  nje  ya  mahakama  hiyo  kwa  kasi  na  kuingia  kwenye  gari  kisha  kutoweka  eneo  hilo….

Akizungumza  na  mwanahabari  wetu, mmoja  kati  ya  ndugu  wa  Mbasha  ambaye  hakupenda  jina  lake  litajwe  alisema  kuwa  mume  wa  mwanamuziki  huyo  aliwaambia  hana  hamu  na  jela,

“Mbasha  alisema  kuwa  jela  hakufai  kabisa  na  alisisitiza  kuwa  asaidiwe  kutoka  kwa  dhamana. Alisema  siku  moja  aliyoishi  mahabusu  ni  kama  mwaka  mzima,” alisema  ndugu  huyo.



Aidha  ndugu  huyo  alisema  kwamba  kitendo cha  Flora  kutomtembelea  mume  wake  ni  cha  kinyama  na  hakuna  aliyekitarajia.

“Hakwenda  kumuona  mume  wake.Kwa  kweli  jambo  hili  limetushangaza  sana  na  kutuumiza  sana, sijui  mwisho  wake  utakuwa  vipi  lakini  tunaamini  yatakwisha, kwa  uzuri  au  ubaya,” alisema.

Baadhi  ya  mahabusu  ambao  walikuwa  selo  moja  na  Mbasha  katika  gereza  la  Keko  wamesema  kwamba  wamefurahi  kuwa  na  nyota  huyo  kwani  wamekuwa  wakimsoma  kwenye  magazeti  tu

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbasha hakuna mtu asiyepatwa na majaribu kwani yamewekewa binadamu ninacho kushauri sali sana na kufungu ili uuone mkono wa mungu juu yako kwani usifikiri aliyoeokoka hapati majaribu huwa majaribu yanakuja ili uzidi kumjua mungu tunakuombea tuko pamoja nawe kwani mungu wetu yuhai (majaribu ni mtaji)

    ReplyDelete
  2. Mungu ndiye Masada tosha. Omba bila kuchoka, washieikishe waumini wa dining zoote wakuombee. Hakuna dini isiyosikiwa na Mungu. Funga na kuomba. Mwombe Mungu akufanyie wepesi wa jambo hili. Yeye ndiye mweza wa vyote na muumba wa vyote. Pole sana.

    ReplyDelete
  3. Du kinacho fwata azidishe mawombi na ache tamazangono ndo ziliyo sababisha kwenda maabusu kila lenye mwanzo linamwisho

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nahisi utakuwa miongoni mwa askari wa M23 waliojificha huku Tanzania. Jifunze Kiswahili kabla hatujakutoa huko mafichoni.

      Delete
    2. Hahahahahahaha we negro umenchekesha

      Delete
    3. My ribs nimechekaaa

      Delete
  4. Asieeee wanawake ni nyokaaa sitaki kuamini mlokole tenaaaaaa najiamini mimi na huyo mungu tu!!! Hakuna cha nabii mfufua msukule wala nini!!! Amepata mbuchuchu nyeupe ya flora amesahau kondoo wa bwanaaaaaa

    ReplyDelete
  5. pole sana mbasha . kama ukutenda hicho kitendo muombe sana
    mungu wako akusaidie .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad