Mbasha:Gwajima Niachie Mke Wangu Flora

Na Makongoro Going’
MUME wa mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha anayedaiwa kumbaka binti wa miaka 17 (jina lipo), Emmanuel Mbasha ameibuka mzimamzima na kumtaka Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la jijini Dar, Josephat  Gwajima amuachie mke wake, yaani Flora.

Akizungumza kwa machungu kwa njia ya simu kutokea alikojihifadhi huku akionesha waziwazi hasira juu ya hisia zake, Mbasha alisema:

“Nimesika mke wangu baada ya matatizo yetu amehamia nyumbani kwa Gwajima. Nataka mumwambie Gwajima aniachie mke wangu, mbona ananifanyia hivyo?”

KINACHOMSHANGAZA
Mbasha ambaye mpaka sasa hajulikani alipo, aliendelea kudai kwamba kinachomshangaza zaidi ni kwamba, Flora amekiuka utamaduni wa Kiafrika, kwamba kama mke na mume wamegombana kiasi cha kushindwa kuishi nyumba moja, mke anakwenda kwao lakini hilo la Flora kukimbilia kwa Gwajima ndilo la ajabu zaidi kwake.

“Kama kweli Flora ameshindwa kuishi nyumbani kwetu (Tabata-Kimanga) kwa nini asiende Morogoro kwa mama yake. Au kwa nini asirudi Mwanza kwenye chimbuko la familia ya mzee Moses Kulola?
“Yeye badala yake amechukuliwa na Gwajima na kwenda kuishi naye nyumbani kwake. Mimi sijapenda, sijapenda na sitapenda kamwe,” alisema Mbasha.
ATUHUMU MTOTO KULIPIWA ADA YA SHULE 
Akiendelea kutoa la moyoni, Mbasha alituhumu kuwa mke wake kwa sasa ana pesa nyingi licha ya kwamba wakati matatizo ya yeye kutuhumiwa kubaka yanatokea na kuingia mitini alimwacha hana kitu.
Anasema: “Wakati matatizo yanatokea Flora nilimwacha mweupe. Mtoto wetu (Elizabeth) alitakiwa kupelekwa shule, kwa hiyo ina maana hakwenda.

“Sasa nasikia mtoto amelipiwa ada na anakwenda shule. Nani kamlipia ada mwanangu kama si Gwajima? Mimi naumia sana, kwa nini iwe hivyo? Kama Gwajima ameamua mke wangu kukaa kwake kwa ajili ya kumsaidia kipindi hiki cha matatizio ajue mimi sijapenda.
“Yeye Gwajima ana mke wake, najua hawezi kusema kitu kwa sababu Gwajima ni kila kitu lakini sijapenda.”

GWAJIMA SASA
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilimtafuta Mchungaji Gwajima kwa njia ya simu ambapo alisema hataweza kuzungumza kwa sababu yupo Mikumi akielekea Dar.
Uwazi: “Sawa, lakini inadaiwa Flora yupo kwako. Hata jijini Dar habari zimeenea kwamba yupo kwako. Mbasha mwenyewe pia amesema mke wake yupo kwako. Unasemaje kuhusu hili?”
Gwajima: “Flora hakai kwangu na wala sijui alipo. Hao wanaosema anaishi kwangu si wa kweli. Hata mkija kwangu hamtamkuta Flora.”

UWAZI LAMSAKA FLORA
Uwazi lilianza kuingia mitaani kumsaka mwimbaji huyo kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya kiintelejensia.
Ilikuwa kazi kubwa sana iliyoanza saa mbili na nusu asubuhi ya Jumapili na ilipofika saa tano, Flora alipatikana kwenye hoteli moja (jina tunalo) iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Alikuwa akijiandaa kwenda kanisani ikabidi hekima zitumike ili aweze kutoa dakika ishirini tu za mahojiano ambapo alikubali.

KUMBE ULIANZA UGOMVI
Akizungumzia kuhusu ugomvi katika ndoa na tuhuma ambazo mumewe anadai kuhusika nazo, Flora alikuwa na haya ya kusema:

“Mimi sina ugomvi na mume wangu Mbasha ninampenda sana ila ninamshangaa kutoa  taarifa yetu ya ndani  katika vyombo vya habari.

“Nimeshtushwa sana na kitendo hicho  kwani kama ingekuwa  ni ugomvi baina yake  na mimi tungekaa chini  na kuyamaliza kama wanandoa. Siamini kama njia hii anayoitumia italeta suluhu, bali itaendeleza matatizo.”

KUHUSU MADAI YA UBAKAJI 
“Nakumbuka ilikuwa asubuhi ya Ijumaa ya wiki mbili zilizopita, Ima (Emmanuel) aliniambia nijiandae kwenda ofisini kwetu kuangalia shughuli, alinipitisha ofisini kisha yeye akarudi nyumbani.
“Baadaye alinipitia ofisini kurudi nyumbani. Nilimkuta  binti mlalamikaji akiwa  hana raha na  hali siyo nzuri, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia.

“Ilipofika Jumapili nilimwambia mume wangu twende kanisani  lakini alikataa, nilimuomba ufunguo wa gari ili mimi niende  na familia, akagoma. Ndipo ugomvi  ulipoanzia, nilimuuliza umekuwaje? Mbona uko hivi? Au  umechanganyikiwa? Alinijibu anataka aondoke  aniache na familia.
“Baadaye akabadilika, akasema hapana haiwezekani yeye akaondoka, bali mimi ndiyo niondoke.”

ATISHIWA KUCHINJWA
“Nilimuomba tuwaite  watu wazima  ili waje  kutupatanisha, akaniambia nikiondoka kwenda kutafuta watu atanichinja.

“Niliamua kuachana naye, nilimpigia simu rafiki yangu mmoja aje anipitie  na gari  kwenda kanisani, lakini huyo rafiki yangu alipita na kuniambia kuwa  amepata  dharura  hivyo asingenipeleka kanisani.
“Nikamrudia mume wangu na kumwambia mbona kama umerogwa? Akasema ndiyo amerogwa, nikamwambia twende kanisani ukaombewe, akakataa. Matokeo yake akanikaba shingoni mpaka nikashindwa kuongea.

Nikamwambia unaniua ndipo akaniachia.
“Nilichukua gari la watu na familia yangu tukaenda kanisani. Kufika kanisani nilimweleza Mchungaji Gwajima tatizo lililonipata, akaniambia nirudi tu nyumbani kama hali itakuwa mbaya ataangalia cha kufanya.

“Baada ya ibada nilimwambia mdogo wangu arudi nyumbani na watoto, mimi nikaenda kukaa mahali nikiwaza cha kufanya.”

BINTI AMPIGIA SIMU
“Ilipofika kesho yake (Jumatatu) nikapigiwa simu na yule binti akidai anaondoka nyumbani kwa sababu shemeji yake amemdhalilisha sana. Nilimwambia asiondoke kuna mtu atakwenda kumchukua mchana kumleta nilipokuwa.

“Alipoletwa nilishangaa kumkuta katika hali ambayo hawezi kutembea sawasawa. Nikamuuliza vipi? Ndipo akanielezea jinsi mume wangu alivyomfanyia.”

BINTI AENDA HOSPITALI
Flora aliendelea kusema kuwa, binti mwenyewe aliamua kwamba anakwenda hospitali kucheki afya. Akasindikizwa na mdogo wake Flora. Kule vipimo vilionesha kweli aliingiliwa kimwili. Madaktari walimshauri aende polisi.

“Ndipo akaenda polisi na kutoa maelezo na kuandikiwa faili ambapo mume wangu akawa anatafutwa.
“Mume wangu amekuwa akisambaza habari kwamba nina mwanaume sijui nani! Hicho kitu hakipo. Hata mwaka jana nilikwenda Uingereza lakini tulikuwa wote.”

KUHUSU KUWA NA PESA, MTOTO KULIPIWA ADA
Kuhusu madai kwamba mtoto amelipiwa ada, yeye hana pesa, Flora alisema:
“Pale kanisani waumini walipojua nina matatizo na mume wangu na sipo nyumbani, walipitisha harambee ambapo niliweza kupata shilingi milioni tisa ndiyo maana  mtoto akaenda shule na mimi nikabaki na za matumizi maana kila kitu kuhusu akaunti ya benki anakijua mume wangu.”

MBASHA AOMBA KESI IFUTWE
“Mume wangu aliniomba msamaha baada ya haya mambo kutokea, nimemsamehe. Aliniomba nifute kesi polisi, nikamwambia si mimi niliyepeleka kesi polisi. Mimi siwezi kumsaliti yeye, kwanza nampenda sana Mungu kisha yeye.”

AKUTWA AMEVUA PETE YA NDOA
Uwazi lilimkuta Flora akiwa hana ile pete ya ndoa iliyozoeleka kuwepo kwenye kidole chake. Alipoulizwa alisema hakuna uhusiano wa pete kutokuwepo kidoleni na ugomvi.

FAMILIA YACHAFUKA
Mwimbaji huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwamba ugomvi kati yake na mume wake umesababisha familia kuchafuka maana umekuwa gumzo katika kila kona ya mtaa.
GPL


Post a Comment

28 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukweli mnao nyie wawili..acheni utoto na kuwapa watu faida..why mnampa shetani nafasi acheze na akili zenu..rudi nyumbani kwako kalee wanao kaa kimnya usizungumzie tena hayo mambo mnajivua tu nguo watu wanamajanga zaidi yenu na wapo kimnyaa..kma mmechokana achaneni kimnya kimnya mtaheshimika..

    ReplyDelete
  2. washenzi wote tena matahira .hivi na wewe gwajima kanisa linaanza kukushinda unaingilia ndoa za watu .kafufue misukule yako achana na ujinga.mwehu nini

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Ni usanii mtupu hapa.Gwaj ataiona Nyapu ya flora chungu.

      Delete
  4. Yani wewe Mbasha ni mnafiki na mwanaume muongo na laghai siijawahi kuona,Wewe ni mzungu?Kilichokushinda wwe kwenda kwenu au kwa kina florah ni nn baada ya kubaka,Achana na mfumo dume,Wanaume mshazoea kufanya maujinga yenu mkitegemea kusamehewa na wake zenu wasipowasamehe mnaanzakakiuka mila za kiafrica sijui nn!

    Na ambavyo huna akili na kujidhihirisha wew ni dhaifu kiasi gani na muuaji kiasi gani unajigamba kumuacha mkeo mweupe tena na mtoto anayetakiwa ada kwenda shule alafu unashangaa nwanao anaenda shule hv we Mbasha ni mzima kweli?

    Umeona haitoshi unanuingiza mtumishi wa Mungu bila hata woga na aibu haya uwazi wamemkuta mkeo sinza hotelini ndipo anapokaa Gwajima?Eti Gwajima niachie mke wangu!Hv unamuonaje na kumchukuliaje?Unejipalilia mkaa mjinga ww .

    ReplyDelete
  5. Mbasha bado hujajiua kwa nini?si ulisema bora ujiue kuliko kudhalilishwa?mbona bado unajidharirisha wewe mwenyewe?
    pumbavu malaya mkubwa,wewe umebaka,ufungwe tu.unakuwa na jina kwa kutumia sauti ya mkeo halafu humuheshimu,nafsi yako inakusuta kwa kuwa unajua ukweli wa mambo,na Kama wewe ni baba bora kwa nini usifatilie kama mtoto wenu kalipiwa ada?kwa taarifa yako imepitishwa harambee na mtoto hatakosa kusoma hata kwa nini,kaa na umalaya wako huko mafichoni uliko.usipotubu,dhambi ya umauti inakujia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na wewe flora dhambi ya kutembea na huyoooo itakusuta.ndoa umeivunja mwenyeweeee,haafu unalalamika mumeo kabaka,Mbasha kaa mbali na hao mafreeMason

      Delete
  6. eti kweli jamani,huyu mbasha hajachukuliwa hatua tu ?au ametoa rushwa?hatusikii kama mbasha kashikwa zaidi ya kuambiwa yuko mafichoni.

    ReplyDelete
  7. Alichokiunganisha mungu binadam hawezi kukitenganisha. Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake

    ReplyDelete
  8. mtu ajifiche wapi tanzania asijulikane na polisi,hii iko namna,rushwa tu.

    ReplyDelete
  9. flora akiolewa na mchungaji ndio mpangi mzima.mbasha! kaa single

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siukaolewe wewe nana...unapendeza kuitwa mama mchungaji...

      Delete
  10. Eee mwenyezi Mungu saidia watumishi wako wamshinde shetani. daaa! soo shame.

    ReplyDelete
  11. Hizo msgs hapo juu kaziandika flora.zinajionyesha wazi wazi,hayaaa Acha movie iendeleee

    ReplyDelete
  12. Mmmh wakakuchangia million Tisa ?chap chap,duuu walokole wana pesa kweli,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wala wanaangalia mtu Wa kumchangia,mi nilikuwa na shida ya laki tano ya Ada ya shule,nimeomba msaada sikupata hata sumni,

      Delete
    2. Na wakazichanga milioni 9

      Delete
  13. Swalli kwa flora,gwajima kakununulia prado jipyaaa,kakusomesha Uingereza ,tupe maelezo Ni nani yako?baba yako,Mjomba au Ni nani yako?msaada tutani.

    ReplyDelete
  14. Sitaki kuhukumu lakini haya makanisa ya kilokole mmmmmhhhh????????Ni dhambi tupuuuuu Mungu nisamehe,mambo yanayotendeka umo Ni ya ajar ajabu(uchawi)wanatumia nguvu za Giza.Wachungaji wazinziiii,mwanzo mwisho,na wake zao au waume zao kimyaaaaa,mafreemason wakubwa

    ReplyDelete
  15. Kwa kesi jinsi ilivyoilivyo Mbasha Kama kweli umebaka UKO FREE.gwajima na flora wanataka Mbasha aozee jela ili waendelee kulitumbua tunda la mtini

    ReplyDelete
  16. Mimi napata shida kidogo mambo ya ndani kuwekwa hadharani tena kwenye media!!! duh Nawaomba kwakweli watumie hekima ya ki Mungu,kwanini kujivua nguo hivi?Mnadhani mnakomoana?La hasha mnajivua nguo ,mnajidhalilisha kam alivyosema mdau hapo juu.
    Flora Maneno yako hayo sio ya kusema in public iko siku macho yako yakifumbuka yanaweza kukupa majuto.Sikia,Emmanuel ni Mume wako wa ndoa tena ndoa safi ya kanisani,hata angekuwa mbaya kiasi gani,hutakiwi kumvua nguo maana,ni mumeo tu vyovyote alivyo,akiaibika na wewe umeaibika maana ninyi ni mwili mmoja.Kumbuka hakuna mtu angemjua Mbasha kama sio wewe na Kazi ya Mungu unayofanya.Je unajua hili sakata lemeshusha sana heshima yako na kiukweli hata kukuficha ndani usitoke kwenye public?Na kimsingi and you should trust me on this mapato yako nayo yanakuwa chini kwa sababau sii rahisi kwasasa kuitwa kwenye tamasha au hata kanisa lolote kutumbuiza!Unajua kuwa hii ni adhari kuwa kwa uchumi wenu?Kwanini mmeamua kuwatesa watoto wenu?NAOMABA SANA JIRUDI KAA CHINI FIKIRI ACHENI KUWAPA WATU FAIDA PLZ.UKWELI WA YOTE MWAJUA NYIE WENYEWE.Kumbuka Biblia inasema samehe saba mara sabini.Hivyo wanandoa wote wangeweka wazi mambo yao ya ndani,Media zingekuwa na nafasi ya kuandika mambo ya maendeleo?sii Rahisi/Binafsi ninaumia sana,Flora una mahubiri mengi mazuri sana yaliyokwenye kanda zako je wadhani bado yatagusa watu kwa kiasi kile kabla hawajasikia sakata hili?My brethren think!! uwe kioo na mafano bora kwa jamii kama public figure.Mungu akusaidie Amen.

    ReplyDelete
  17. Flora kwasasa Hana shida yoyote ya pesa,gwaji anatunza ,prado kanunuliwa ,shule Uingereza alipelekwa.waumini toeni sadaka kwa masikini na sio kwenye hayo makanisa,

    ReplyDelete
  18. Jamani ni kweli zilichangwa,kwanza ilianzwa na maombi baadae ikawa hiyo harambee,ilipotangazwa tu yaani
    ilikuwa ni mimi laki 5,laki 2, elfu hamsini ndani yaa dk chache mil.9 na kidogo zikapatika.lakini Kanisa hilohilo kuna watu wana maisha duni huwezi amini.walokole?

    ReplyDelete
  19. mifumo dume haikemei wanaume wanapokosea, eti mwanamke mjinga hubomoa nyumba yake. we msenge nini, kwahiyo akae kwenye ndoa mpaka apewe ukimwi au achinjwe kisha aseme asante MUNGU, unafirwa na baba yako si haba.

    ReplyDelete
  20. achene ujinga mbasha keshatomba sana inje ya ndoa na kila mtu analijua hilo mbona hamu muhukumu?? wote nyie wanafiki kutwa kushadadia ya watu ya kwenu yamewa ozea magoli kipa pyeeeee

    ReplyDelete
  21. Ni mwsho wa Flora kuimba,labda amuimbie Gwaj chumbani,na ni mwanzo wa anguko la msanii Gwaj.Dawa zake zimeanza kuexpire,atakwisha taraatiibu.Mungu hachezewi!

    ReplyDelete
  22. CHUNGA SANA WEWE UNAYE ANDIKA MATUC.PIA UCCHANGIE MANENO UCYOKUWA NA UHAKIKA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad