Mdee Atoboa Uozo, Ahoji Safari za Rais Kupewa bil. 50/-,Awataka Wakulima, Wafugaji Kuipiga Mawe CCM

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amewataka wakulima, wafugaji kuipiga mawe Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutenga sh bilioni 50 kwa ajili ya safari za rais huku ikitenga sh bilioni 51 kwa maendeleo ya kilimo.

Akichangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Mdee alisema serikali haina nia ya dhati ya kuutokomeza umasikini, ikiwemo kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi.

Alibainisha kuwa katika bajeti ya mwaka jana, serikali iliahidi asilimia 10 ya bajeti itakwenda kwenye kilimo, lakini ikaishia kutenga asilimia nne, na bajeti ya mwaka 2014/2015 imetenga sh bilioni 51 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kilimo.

Alisema kiwango hicho kimepishana kidogo na kile kilichotengwa kwa ajili ya safari za Rais Jakaya Kikwete, ambazo zimetengewa sh bilioni 50.

“Wakulima, wafugaji na wavuvi wanapaswa kuipiga mawe Serikali ya CCM, hapa mmetuletea bajeti, lakini ukiangalia kwa kina utaiona haina dhamira ya kuwasaidia wananchi,” alisema.

Mdee, alisema bajeti ya Wizara ya Kilimo kila mara imekuwa ikitengewa fedha, lakini hazifiki kwa walengwa, hivyo mipango mbalimbali imeshindwa kutekelezeka.

Alisema kuwa serikali kupeleka huduma kwa wananchi ni lazima na sio hiyari, hivyo wabunge wa upinzani wanapokosoa utendaji wa serikali hawafanyi jambo baya bali wanatekeleza wajibu wao.

Aliongeza kuwa serikali kila mara imekuwa ikipewa ushauri mbalimbali, lakini inashindwa kutekeleza jambo linalosababisha kukosa mapato yanayotakiwa.

Alisema miaka minne iliyopita upinzani ulipendekeza kodi ya mishahara kwa wafanyakazi ishuke chini ya asilimia 10, lakini serikali ilishindwa kutekeleza jambo hilo hadi hivi sasa ilipoamua kushusha kutoka asilimia 13 hadi 12.

Aliongeza kuwa Kamati ya Bajeti inafanya kazi kwa niaba ya Bunge na imelalamika inatoa mapendekezo serikalini lakini inapuuzwa hali inayoonyesha serikali haina dhamira ya kutafuta vyanzo vipya vya mapato visivyowaumiza wananchi.

Mkosamali amvaa Chenge

Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), aliituhumu Kamati ya Bajeti kuwa inafanya vikao visivyo na tija ilimradi ihalalishe wajumbe wake kupewa sh 500,000 kwa kila kikao.

Alisema anashangazwa na kamati hiyo kuendelea kulalamikia kupuuzwa kwa ushauri wanaoutoa kwa serikali wakati wana uwezo wa kutoa azimio la kukataa bajeti hadi walichokishauri kifanyiwe kazi.

“Jamani tuwe wakweli hapa, sisi tunalalamika tu wakati uwezo wa kubadilisha mambo tunao, tukubaliane hapa kuikataa bajeti hii mpaka serikali itakapoleta bajeti yenye tija kwa taifa.

“Kamati ya mzee Chenge taarifa yao inalalamika kuanzia mwanzo mpaka mwisho halafu inasema inaunga mkono bajeti, hivi kama si unafiki ni nini? Inakaa hivi sasa na mashirika kujadili kuwapunguzia kodi… hii ni rushwa tupu,” alisema.

Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisema serikali imeshindwa kutumia ushauri wa kuanzisha kituo cha uvuvi wa samaki katika bahari kuu, ambako samaki wanavuliwa bila kulipiwa ushuru na kampuni kubwa.

“Nyinyi serikali mna tatizo gani kila mwaka tunawapa ushauri na wataalamu wenu wanaandika ripoti zinazoonyesha umuhimu wa kuanzia kituo cha uvuvi katika bahari kuu, huko tunapoteza mapato mengi lakini hamjali, nyinyi akili zenu zinawaza nini?” alihoji.

Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jaffo (CCM), alisema kiwango cha asilimia kilichopunguzwa kutoka katika kodi inayotozwa kwenye mishahara ni kidogo na hakina msaada kwa wafanyakazi.

Alisema serikali inapaswa kujikita zaidi kwenye kutafuta vyanzo vipya vya mapato badala ya kila kukicha kuwabana wafanyakazi na wananchi.

Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CM ni janga la kitaifa mapesa yote hayo jamani yanatengwa tu ili mtu mmoja na wapambe wake wakazurure Ulaya! !!! What if zingepelekwa mashuleni kununua madawati c watoto wa wakulima wangepata ahueni jamani. Hii CCM 2015 piga kimyaaaaaa

    ReplyDelete
  2. Alshababy tusaidieni katika kuweka mambo sw

    ReplyDelete
  3. jamani muoneni MUNGU,wkt wengine huku tunalipwa laki mbili kwa mwezi wengine millioni tatu kwa mwezi wengine billion 50 kwa kwenda kutembea! hv huyu wa laki mbili ungemuongezea elfu 50 cangefungua banda la nyanya ajikwamue.nyie jifanyeni hamnazo.

    ReplyDelete
  4. duh!!!! ccm 2meichoka sn!!! undai makampuni yalipe kodi wamili n vigogo wa ccm? ktk majimbo yanayomilikiwa na wapinxan serikali haileti miradi ya maendeleo ili wkt wa uchaguz wadai chama hiki kimewaletea nn? hawa kwl dawa yao ni alshabab/boko haram....... kidadek xao...

    ReplyDelete
  5. swala la paye ni zito kwetu cc walipwa hela ya mbuzi tena serikalini! ww kisa unalipwa mamalioni ya hela na posho juu ndo unaona kwako 1% ni kubwa .huku hakuna posho wala nn na hela ynywe ukilipa kodi ya pango,maji,umeme hakuna salio! hv mbona mnautani namaisha ya watu jamani.anyway dawayenu ni kumiboko haram uchaguzi ujao.

    ReplyDelete
  6. CCM cham kibaya sana na watu wake waroho hakuna mfano,,,,cwapendi mnatuonea maskini tukiongea mnatuua,,,,all of you gona end up in hell i swear.....

    ReplyDelete
  7. CCM cham kibaya sana na watu wake waroho hakuna mfano,,,,cwapendi mnatuonea maskini tukiongea mnatuua,,,,all of you gona end up in hell i swear.....

    ReplyDelete
  8. CCM cham kibaya sana na watu wake waroho hakuna mfano,,,,cwapendi mnatuonea maskini tukiongea mnatuua,,,,all of you gona end up in hell i swear.....

    ReplyDelete
  9. Kaka nakuunga mkono, ccm tiba yao ni kuwaletea tu alshabaaby na boko haramu 2015 ili kieleweke pambafuuu zenu

    ReplyDelete
  10. Malza ccm tena ilbid kuwaweka mjengoni alaf tunawaita Alshaabab wafanye yao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad