Mh.Zitto: Ukawa Rudini Bunge la Katiba Kumuenzi Marehemu Mama Yangu

Zitto Jana katika maziko ya Shida, ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wa kuteuliwa na Rais, Zitto aliwataka wajumbe wenzake kumuenzi mama yake kupitia viongozi wao, Mwenyekiti wa Kamati namba nane, Job Ndugai na Mwakilishi wa Ukawa, Profesa Ibrahimu Lipumba.

Alitoa ujumbe huo nyumbani kwa marehemu mama yake, mtaa wa Kisangani Mwanga, muda mfupi kabla ya kwenda makaburi ya Rubengela mjini Kigoma ambako mwili wa Shida Salum ulizikwa. Zitto alisema kama kweli viongozi hao wanataka kumuenzi mama yake, wamalize tofauti zao na kulifanya Bunge Maalumu la Katiba, kuendelea na shughuli yake ya kuwaletea Watanzania Katiba itakayowafaa kwa muda mrefu.

Alisema kuwa mama yake alikuwa mjumbe wa Bunge hilo baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, nafasi ambayo ingempa fursa ya kuandika historia ya kuwa mmoja wa wajumbe wa Bunge hilo, katika kuandika Katiba mpya ya Tanzania.

Hata hivyo, alisema kwa kuwa mama yake aliugua na Mwenyezi Mungu kwa kudra zake akamuondoa katika nafasi ya kuandika historia hiyo, kilichobaki ni viongozi na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kufikia maridhiano na kuandika Katiba hiyo.

Zitto alisema amejitahidi kwa kadri ya uwezo wake kumsaidia mama yake kupata matibabu ambayo yangerudisha afya yake, na kumpa fursa ya kushiriki katika shughuli zake za kawaida, lakini Mungu alipitisha uamuzi wake ambao hakuna wa kumpinga.

Naye Ndugai, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeongoza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye maziko hayo, alisema Shida alikuwa mtetezi wa Watanzania wa hali ya chini.

Alisema yaliyotokea ni mapenzi ya Mungu na kuitaka familia wasihuzunike kiasi cha kupitiliza, badala yake wakae pamoja na kuweka familia pamoja na kusonga mbele katika utekelezaji wa majukumu yao ya Taifa.

Naye Profesa Lipumba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, alisema kuwa Shida alisimama kuwapigania watu wenye ulemavu mchango ambao alikusudia kuutoa kwenye Bunge Maalumu la Katiba.

Hata hivyo Lipumba alionya kuwa kama kweli watu wana nia ya kumuenzi Shida, hawana budi kusikiliza maoni ya wananchi walio wengi katika kuipata Katiba mpya, badala ya watu wachache kutaka kuichakachua.
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kumbe mama yake na Zitto alikua mjumbe wa katiba!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Lipumba upo sawasawa,maoni ya wananchi ni lazima yaheshimiwe la sivyo patachimbika.

    ReplyDelete
  3. tena patachimbikabila jembe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haswa wadau maana hawa mafisadi sasa wamesha tudharau vya kutosha sasa!

      Delete
  4. Huyo zitto ni mamluki wahedi sasa kikwete alimpa nafasi mamake ili iweje chadema timyeni huyo mtu mnangoja nin sijui

    ReplyDelete
  5. Mbona chadema sijawasikia wala kuwaona kwenye msiba wa mama Zitto?

    ReplyDelete
  6. sasa kama Rais na mwenyekiti wa sisiem alimpa mama ujumbe then chadema itakuwa na maana gani kwa mtoto.huwa watu wanalaumu kwa nini Mbowe hataki kuachia Uenyekiti lakini hawajui ya kuwa kumpata mtu wa kumwamini si kitu kirahisi na inachukua muda!!nani angeamini miaka mitano iliyopita kuwa Zitto wangemtuliza kirahisi kama iivyohivi sasa!!?

    ReplyDelete
  7. zito inaonekana hakuumia kabisa kwenye msiba wa mama yake

    ReplyDelete
  8. nina wasiwasi, undugunaizesheni katika Serikali yetu! tunapeana tu, hadi wazazi!

    ReplyDelete
  9. mama shida salumu alikua anastahili, yule mama alikua na upeo wa hali ya juu, sema ukuwahi kukaa chini na kubadilishana nae mawazo, hakuna cha undugunaizesheni kama unavodai

    ReplyDelete
  10. Kama mama Zitto hakuwa UKAWA,ataenziwa na ccm na si vinginevyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad