Mitandao ya Kijamii Sasa Kudhibitiwa na TCRA...Onyo kwa Wanao Penda Kutukana Wenzao Kwenye Comments

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inajipanga kuja na mfumo wa kompyuta utakaoratibu taarifa zote zinazopakiwa mtandaoni ili kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na watu wasio na maadili ya uandishi wa habari.

Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa mamlaka hiyo, Dk Joseph Kilongola katika kongamano la kimataifa la habari lililo andaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kufanyika jijini hapa kwa mara ya kwanza, mwaka huu.

“Licha ya kuwaelimisha wadau wa habari hasa wamiliki wa ‘blog’ juu ya kuzingatia maadili ya uandishi kwa kila wapakiacho mtandaoni, sasa tunakuja na cyber security itakayosimamia upashanaji habari,” alisema Dk Kilongola.

Alisema mfumo huo utafanya pia kazi ya kuchuja habari zote kabla hazijawekwa mtandaoni na utatoa ulinzi kwa jambo lolote linalotishia usalama katika sekta yoyote ya uchumi na kabla madhara hayajatokea, wahusika watakuwa wameshajulikana.

Profesa Florens Luoga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alitahadharisha dhidi uhuru na haki ya matumizi ya majukwaa mbalimbali ya mawasiliano kuwa yanapaswa kuzingatia maadili ili kuepusha athari zinazoweza kujitokea katika jamii.

“Kila teknolojia mpya huja na athari zake. Maendeleo ya teknolojia ya habari nayo yamekumbwa na hilo. Athari zake zimeanza kujitokeza.

“Maadili ya kitaaluma ni vyema yakazingatiwa na wote wanaojihusisha na upashanaji habari ili kuchangia maendeleo yaliyokusudiwa,” alisema Profesa Luoga.

Alihimiza wataalamu wa habari kuhudhuria makongamano ya kitaaluma yanayoandaliwa.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wapi nana junior mamaa wa mitusi

    ReplyDelete
  2. Mayoo weee sasa tutaishije bila ya matusi eti Nana? si tutaugua jamani mimi ntatukana tuu kama noma na iwe nomaaaa!jamani mimi naasira sijui ninye mi ntakunya mie...?!

    ReplyDelete
  3. Hahaaaaa safihiyoooo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad