Mrembo Aliye Piga Picha na Komba Chumbani Aibuka na Kusema Haya



SIKU chache zimekatika baada ya tukio la kusambaa mitandaoni kwa picha tata zenye pozi kati ya mheshimiwa Komba na mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Angel.

Hatimaye mrembo huyo ameibuka na kuanika mambo mazito kama si makubwa, Risasi Mchanganyiko linakudadavulia.

Awali katika gazeti hili toleo la Jumamosi iliyopita ukurasa wa mbele kulikuwa na habari hiyo ikiwa na kichwa; KHAA! KOMBA! Katika habari hiyo picha zilizomuonesha mheshimiwa Komba akiwa na mrembo huyo zilipamba ukurasa huku mwenyewe (Komba) akidai ni picha za kutengeneza).

OFM YAINGIA MITAANI
Kwa vile Komba alikataa picha si zake huku baadhi ya vyombo vya dola kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) vikitangaza kuingia kazini kumtafuta sosi wa picha hizo, ilibidi timu makini ya Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kutoka Global Publishers iingie kazini kumsaka mrembo huyo kwa udi na uvumba.

YATUMIA NUSU SIKU
OFM ambayo huwa haishindwi kitu, ilitumia nusu siku ya Ijumaa iliyopita na kufanikiwa kuinasa namba ya simu ya mkononi ya Angel pamoja na picha nyingine ikiwepo iliyotumika ukurasa wa mbele wa gazeti hili.

Aidha, ilibainika kwamba, mrembo huyo anaitwa Angel Kissanga, mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, bila ajizi Paparazi wetu alimwendea hewani Angel na kumuuliza kama ana habari zozote kumhusu yeye.
Angel: “Habari kama zipi? Mimi sina habari zozote.”

Paparazi: “Hujaona kwenye mitandao ya kijamaii wameweka picha zako ukiwa katika mapozi tata na mheshimiwa Komba?”
Angel: “Ngoja kwanza, nitakupigia.”

MUDA UNAKWENDA, ANGEL ARUDIWA
Baada ya kuona muda unakatika bila mrembo huyo kupiga simu kama alivyokuwa ameahidi, paparazi wetu alimrudia hewani ambapo safari hii simu yake ilipokelewa na mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni dada wa Angel.

“Mimi si Angel, ni dada yake. Angel amepandwa na presha baada ya wewe kumwambia kuna picha zake na mheshimiwa Komba kwenye mitandao.
“Unajua ngoja nikuambie ukweli. Mdogo wangu ameshtuka sana, hivi hapa tupo Hospitali ya Micco Sinza, amelazwa.”

PAPARAZI ATIA TIMU HOSPITALINI
Kusikia hivyo, paparazi wetu alifunga safari hadi kwenye hospitali hiyo ambapo kweli mrembo huyo alikuwa amelazwa kwa matatizo ya presha ya kupanda.

Mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni mama mdogo wa Angel alimjia juu paparazi wetu akidai yeye ndiyo chanzo cha mwanaye huyo kupandwa na presha ghafla, akamtimua asimuone mgonjwa.

MAZUNGUMZO YA BAADAYE
Siku iliyofuata, paparazi alibahatika kuzungumza na Angel ambaye aliweka wazi mambo yake kuhusu picha hizo kama ifuatavyo:

“Mimi nataka kusema kwamba picha nimeziona, nazifahamu kweli ni mimi.”
Paparazi: “Ni kweli ulipigwa ukiwa na mheshimiwa Komba?”
Angel: “We jua tu kwamba picha nazijua. Zilipigwa na simu ya LG.”
Paparazi: “Alipiga nani?”

Angel: “Nimesema nazifahamu.”
Paparazi: “Hiyo simu ni ya nani?”
Angel: “We wa nini?”
Paparazi: “Okey, mheshimiwa Komba unamfahamu?”
Angel: “Namfahamu ndiyo.”
Paparazi: “Ni nani wako?”

Angel: “Nimekwambia namfahamu.”
Paparazi: “Sasa mbona mheshimiwa Komba anasema picha zimetengenezwa?”
Angel: “Mimi sijui sasa.”

ANGEL ATAKIWA KUTIA TIMU GLOBAL
Baada ya mazungumzo hayo, paparazi alimtaka msichana huyo kufika kwenye ofisi za magazeti ya Global ambapo alikubali.

Hata hivyo, baadaye alisema amebatilisha baada ya baba yake kuingilia kati sakata la picha hizo akidai yeye ndiye atakuwa msemaji mkuu.
Habari za chini kwa chini zilidai kwamba, kusita kuweka miguu kwa Angel kwenye ofisi za Global kulitokana na zuio la mheshimiwa mmoja ambaye alimchimba mkwara kwamba asitoe ushirikiano wowote na vyombo vya habari.

MASWALI MUHIMU
Maneno ya Angel na mheshimiwa Komba yanapingana. Mmoja anasema picha zilitengenezwa, mwingine anazitambua na zilipigwa kwa simu ya LG, nani mkweli? (endelea kufuatilia Magazeti Pendwa ya Global Publishers).

ANATAJWA PAULINA
Mbali na kupishana kwa maneno ya wawili hao, mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Paulina anatajwa kuwa nyuma ya sakata hilo.

Mwanamke huyo anadaiwa wakati fulani kuingia kwenye mzozo na Angel na akaja kudai ameipata simu yenye picha za mrembo huyo na mheshimiwa bila kujulikana alikoipata. Je, aliipata kwa Angel au mheshimiwa Komba? 
(endelea kusoma magazeti ya Global).

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kidemu chenyewe kishamba..ila vinyonyo saa 6.....kwani akipiga nae picha tatizo nini...alafu hebu mucaheni mzee wa watu..mbona mnasumbua wafuaten mawaziri wachafu zaidi ya huyo john komba

    ReplyDelete
  2. Wacha muviee iendeleee, mbona yanajulikana haya haya ya hwa viongozi, sema huwa hayafiki kwenye viombo vya habari, angelwatamtam amwshamaliza yote, komba ache ujinga wake kwanza wa kudanganya umma, na hito tabia ya kupenda ndogndogo. Alafu nyie viongozi, wacha wanahabari wafanye kazi yao. kukomesha maovu katika hii jamii, msilete udikteta na umafia hili ni Taifa la wote watanzania lijengwe kwenye misingi ya maadili sio umfya hapa wa nyinyi viongozi wapumbavu. lazima atakae fanya upumbavu kiongozi wote na raia wa kawaida wote mnawajibika.

    ReplyDelete
  3. wacheni mambo yenu, kwani yy kuna ubaya gani nyinyi wenyewe waandishi mna mambo mangapi mnafanya? mbona hamuyasemi ya wenzenu umbea juu. ila picha hizi ni za kughushi bwana, demu kanga moko muheshimiwa ana nguo zake zote kama yuko jukwaani. msimsingizie babu wa watu.

    ReplyDelete
  4. Na yule ELIZAbeth vip mbona amuongei!!!!!

    ReplyDelete
  5. kwani akipiga nae picha kunani....je ni under 18??? mwacheni mzee ajilie vitu vizuri, tatizo la vijana wa Kitanzania wanataka vitu vizuri wale wenyewe tu.....lo hamna aibu...mbona nyie mnatoka na majimama...!!!!!

    ReplyDelete
  6. Angalia back ground ya hiyo picha.inathibitisha forging

    ReplyDelete
  7. Muacheni mzee jamani coz hakuna ubaya wowote kupiga picha wa aina yoyote ubaya tu umepiga mbele ya akina nani? Kama asingeonyeshwa kwenye mtandao isingekuwa tatizo lolote, umbeya tu unawasumbua

    ReplyDelete
  8. Kidemu chenyewe kibovu au mnafataga nyuchi tu na si sura pole komba bora ungebaki na lulu tu

    ReplyDelete
  9. kademu kenyewe kabaya kanaona raha apo iyo pic kawapa anatafuta umaalufu

    ReplyDelete
  10. Mwaka 2014 ni mwaka wa sodoma na.Gomorah- Kapten Komba vs Angel kissanga, mh Kapuya vs Elizabeth, Mchungaji Gwajima vs Flora Mbasha, Mh adam Malima Vs Changudoa.IGP Mahita vs Housigeli, Kapten Komba vs Lulu,Mchungaji Agustine Mwingira vs Mrs.E.Mbuya.Waheshimiwa hawa wanaabudu nyapu za akinamama kupita maelezo.

    ReplyDelete
  11. Acheni ujinga, sasa si bora kdemu chenyewe? huyo Bonge tumuweke category ipi? mimi hata kwa bure tu simtaki maana anaweza asipite hata kwenye mlango wa nyumba yangu, yuko kama pipa.

    ReplyDelete
  12. JIHADHARINI MTAFANANA NA BABU SEYA HIIII !

    ReplyDelete
  13. jinsi ya kutengeneza pesa kupitia computer yako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad