Msanii Mwingine Aibuka na Kusema Diamond Kumuibia Nyimbo

Malalamiko ya wasanii kuibiana au
kupigana kanzu kwenye kazi zao
yaliripotiwa sana mwaka jana na
mwaka huu mambo yalikuwa
shwari, lakini baada ya kuvuka nusu
ya mwaka yameibuka tena.
Mshiriki wa shindano la kuimba la
Bongo Star Search (BSS) , Wababa
amewatuhumu maswaiba wa ‘Muziki
Gani’ Nay wa Mitego na Diamond
Platinumz kwa kumuibia kazi zake
kwa wakati tofauti.
Akiongea kupitia Friday Night Live
ya East Africa TV, Wababa amesema
Diamond amemuibia wimbo wake
ambao alikua anaiita ‘Kitorondo’ na
kwamba aliibadilisha jina baadae.
“Kiukweli kuhusu Diamond, mimi
mwenyewe nimetumiwa hiyo ngoma
ambayo ameitoa, nimeiskiliza jinsi
ilivyo kuanzia idea, mwendo, style
ambazo anafanya. Ambayo
ameibadilisha jina tu baada ya ya
kwamba ilikuwa mitandaoni nilikuwa
nimemfatilia ilikuwa inaitwa
Kitorondo mwezi mmoja kama
uliopita. Kwa hiyo nilishindwa
kulalamika kwa sababu yeye
mwenyewe alikuwa analalamika
kuwa imevuja. Kwa hiyo sikuona
sababu ya kuongea kitu kwa sababu
haikuwa official. Kwa hiyo sikuwa
na sababu ya kucomplaini kwa
sababu haikuwa official, lakini
mpaka jana ina maana ilikuwa
serious kama biashara.” Ameeleza
Wababa.
Alipoulizwa ni wapi ambapo
Diamond aliusikia wimbo huo,
amesema huo ni wimbo wake
alioutoa miaka minne iliyopita akiwa
na Dogo Asley na aliuweka kwenye
mtandao wakati anatumia jina la
Nurdi, kabla hajaanza kutumia jina
la Wababa aliposhiriki BSS. “Ni
nyimbo ambayo iko mtaani na watu
wengi wanaielewa. Kwa hiyo
sijaelewa..”
Kwa upande mwingine, Wababa
amedai kuwa alifanya kazi na Nay
wa Mitego katika studio za Mazoo
lakini baaadae Nay alirudi studio na
kuongea na Mazoo kutaka kuunua
wimbo huo kwa shilingi milioni
moja bila kumshirikisha Wababa.
“Hivi karibuni nimefanya ngoma
mpya na Nay wa Mitego, ni ngoma
ambayo ilikuwa iko paid kwake
pamoja na studio. Lakini kitu cha
kushangaza ni kwamba siku mbili
baada ya kufanya kazi nikapigiwa
simu na producer akaniambia
kwamba jamaa amerudi tena kwa
ajili ya kutaka kununua wimbo kwa
milioni moja, auchukue wimbo
aende akaufanye sehemu nyingine.
Baada ya hapo hata mahusiano
yangu na mshikaji yamekuwa sio
mazuri. Ukimpigia simu anakwambia
yuko busy kuna kazi anafanya
atanicheki, hadi kufikia leo sielewi .”
Nay alipigiwa simu lakini hakuwa
anapatikana kwa muda huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad