Msekwa: Hatuhitaji Katiba Mpya, Kitu Chochote Kinachotakiwa Kingeweza Kuingizwa Katika Katiba iliyopo.

Spika mstaafu, Pius Msekwa amesema haoni haja wala sababu ya msingi ya Tanzania kuandika Katiba Mpya kwa sasa kwani hakuna matukio makubwa ya kisiasa nchini yanayolazimisha kufanya hivyo.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam jana, Msekwa alisema hata hivyo, anakubaliana na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuruhusu kufanyika kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa sababu alikuwa na sababu zake na alikwishazieleza wazi.

Alisema, “Sioni haja ya kuwa na Katiba Mpya. Mnatunga Katiba Mpya kama kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa, yaani mabadiliko ya kiutawala,” alisema.

Alifafanua Katiba ya Tanganyika na hata ya Tanzania ilibadilishwa pale palipokuwa na matukio makubwa ya kiutawala, lakini pia kuna matukio mengine ambayo hayakulazimisha kuandikwa upya kwa Katiba.

Msekwa aliyeshiriki michakato yote ya katiba zilizotangulia ikiwamo hii ya sasa, alisema kwa kawaida Katiba Mpya inaweza kuandikwa panapokuwa na mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini kama ilivyotokea mwaka 1962 baada ya Tanganyika kupata uhuru wake, lakini Malkia wa Uingereza akaendelea kuwa mkuu wa nchi.

“Katika mazingira hayo Watanzania hawakujua maana ya uhuru ni nini, ikaleta sintofahamu, ikabidi Mwalimu (Julius Nyerere) na wenzake waamue kufanya mabadiliko makubwa ya kisiasa kutoka kuwa chini ya Malkia kwenda kwa uongozi wa wananchi,’’ alisema.

Pia, alieleza kuwa kuanzishwa kwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lilikuwa tukio jingine kubwa na la msingi lililosababisha kuandikwa kwa Katiba Mpya ya mwaka 1977.

“Mfano wa pili tulipoingia katika Muungano mwaka 1964, hapa kulikuwa na nchi mbili ambazo ni sovereignty (nchi zenye utawala kamili) tukaziunganisha, mazingira kama hayo yalidai Katiba Mpya.

Hata hivyo, Msekwa alisema hata mabadiliko kama ya mwaka 1965 kutoka mfumo wa vyama vingi vya siasa kuingia chama kimoja licha ya kuwa tukio kubwa, hayakulazimisha kuandikwa kwa Katiba Mpya, bali iliyokuwepo ilifanyiwa marekebisho.

Alisema tukio jingine ni la mwaka 1984 ambako mabadiliko mengine yalifanyika katika Katiba kwa kuingiza kipengele cha haki za binadamu na ukomo wa kipindi cha urais kuwa wa vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja ambalo halikuhitaji Katiba Mpya.

Badiliko jingine kubwa ambalo halihitaji katiba mpya, Msekwa alisema ni lile la mwaka 1992 la kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini … “Tuliporejea mfumo wa vyama vingi hatukutunga katiba kwa kuwa haikuwa lazima. Unaondoa vile vifungu vinavyoondoa chama kimoja na vingine vinaendelea kama kawaida.

Kwa hiyo hata sasa hakuna haja ya kuandika Katiba Mpya, kitu chochote kinachotakiwa kingeweza kuingizwa katika Katiba iliyopo.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tabu tupu ni lazima ibadilishwe kwa kuwa tunataka utanganyika wetu shwain

    ReplyDelete
  2. never let old pple decide for youths. just allow them to giv advice. vijana tuungane kutunga katiba itakayotufaa sisi na vizaz vijavyo.

    ReplyDelete
  3. we uliikuta Tanganyika au unaijua Tanganyika na ninawaswas ata baba yako auikuta Tanganyika Umezaliwa Tanzania unataka kitu usicho kijua ata mipaka ya Tanganyika uhijui kaz kelele tu kamaunahijua Tanganyika wewe bunge la Tanganyika lilikuwa linakaa vikao vingap kwa mwaka? kama ujui kitu kidogo hvy kwa nin uitake nchi ambayo uhijui ujui mipaka yake umbea tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. unajua wewe mwenye jina la kike la mbele sijui baba yako ni mwanamke?sikia kupenda kwako ccm na ufisadi sio woote na hupashwi kumchagulia mtu cha kufanya kama ni saporter wa tanganyika muache wewe inakuuma nini?mijitu yote inayosaport ccm huwa hamnazo kabisa shwaini mkubwa!

      Delete
  4. wazee wa sisisieeeem hao, wanata waleee tu mpaka wapasuke!! TUNATAKA KATIBA MPYA!! ama zenu zishapita!

    ReplyDelete
  5. Msekwa uoni haja ya katiba wewe kwa sababu ya sasa una manufaa makubwa uliyopata sisi tunaomba ipatikane nyingine labda inaweza kutusaidia walau hata kupata hata kwenye hospital za serikali

    ReplyDelete
  6. Wewe Vincent hapo juu mkundu wako kwenda zako na mawazo.mgando ya ma CCM wenzako kwani km mdau anataka Tanganyika ww unawashwa nini? Nabii yako na ukoo wako wa majambazi,peleka papuchi yako ikakunwe huko maana inakuwasha kahaba mkubwa weeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad