Mtoto Mchanga Auwawa Kwa Kufungwa Plasta Mdomoni na Puani Kisha Kutupwa

Mtoto mchanga, amekutwa ametupwa pembezoni mwa barabara ya Kawe-Beach, huku puani na mdomoni akiwa amefungwa plasta, iliyosababisha kukosa pumzi na kufariki.

Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja ambaye hakujulikana jina lake wala kujua anapoishi, anasadikika kutenda ukatili na unyama wa hali juu kwa kumuua huyo mwanaye na kisha kumtupa pembezoni mwa barabara hiyo.

Wavuvi wa eneo hilo waliona mfuko pembezoni ukiwa na damu hali ambayo iliwashtua na kuamua kusogea karibu, ndipo walipomkuta mtoto huyo mwenye jinsi ya kike, akiwa amefariki huku akiwa amefungwa plasta mdomoni na puani.

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu unyama gani jamani.. binadamu tumekua washenzi mpaka shetani anatushangaa!!!

    ReplyDelete
  2. Mmmh jaman yaan hyo mwanamke alaaniwe nktazama pcha ya hyo Mtoto naumia sana kwa nn wanawake tumekuwa na roho za knyama kias hk jaman Mtoto umbebe mimba miez tsa afu uje umuue tena kwa kfo cha mateso kama hcho c bora angempeleka msiktn au knsan Mmmh

    ReplyDelete
  3. Daah najuta mungu wewe ndio unajua yote naamin atapatikanatu

    ReplyDelete
  4. Ni kweli kuna dhambi nyingine hata shetani atakuja kutukana kwamba sio yy aliye tutuma kwa kweli!

    ReplyDelete
  5. Kwann ufanye ngono zembe! Haya ndo matokeo yake. Jins mimba inavyosumbua miez tisa kisha unatupa mtot? Maskin hakustahili haya
    .

    ReplyDelete
  6. Bado tunamachungu ya mtt wa box na hili tena eemola watu hawana hofu ya Mungu hata kidogo!!!!!

    ReplyDelete
  7. malipo ni hapahapa....

    ReplyDelete
  8. Inna lillahi wainna ilaihi raajiuun,Pumzika kwa amani malaika uliyedhulumiwa nafsi yako ila huyo mamake nafsi itamsuta mpk siku ya mwisho

    ReplyDelete
  9. inauma sana ila wanaume wengi hukataa mimba zao jambo ambalo sio zuri pia cha muhimu ni sote kukubali matokeo.

    ReplyDelete
  10. sasa mume anakataa mimba ndo uzae utupe mtoto?, yan nikae na tumbo miez 9 kisha nitupe, hapo alaumiwa nani kama c mama mtupa mtoto?,

    ReplyDelete
  11. serekali lazima imtafute mtenda kosa hilo ili achuliwe sheria

    ReplyDelete
  12. mwananamke mwenye akili hawez tupa mtt ukikumbuka mateso ya mmba na kuzaa ni bora umlee kwa shida unaweza pata msaada kuliko kmuua

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad