Siku chache baada ya kutokea shambulizi kubwa la bomu katika soko kubwa ‘Mall’ jijini Abuja, Nigeria mtoto mwenye umri wa miaka 13 amesaidia kuwaokoa raia wa Nigeria kushambuliwa na bomu kubwa baada ya kulishitukia na kutoa taarifa polisi.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Kano, aliyejitambulisha kwa jina la Magaji Majiya, mtoto huyo wa kiume alipata mashaka baada ya kuona gari fulani bovubovu likiwa limetelekezwa huku likiwa na mzigo mkubwa karibu na msikiti mmoja.
Na ndipo alipolichungulia kuona vitu kama mabomu na akatoa taarifa mapema.
“Bomu liliwalenga watu walioenda kuabudu katika msikiti huo na lilikuwa limewekwa kwenye gari aina ya Toyota Tercel.” Alisema Majiya.
Polisi walituma kikosi maalum cha kutegua mabomu ambacho kilifanikiwa kulitegua bomu hilo.
Mtu mmoja amekamatwa kutokana na tukio hilo.
Mtoto wa miaka 13 aikoa Nigeria Kulipuliwa na bomu kubwa
5
June 29, 2014
Tags
safi sana dogo, ingekua hapa kwetu huyo dogo angeanza kukagua kutaka kujua hicho ni nini, natamani tungekua tunafundishwa shuleni aina za mabomu ili hata ukiliona uweze kulitambua,
ReplyDeletemimi na ukubwa wangu hata bomu sikijui zaidi ya kuona picha
Yaani police wetu walivyo na dharau wala wasinge wahi lingelipuka
ReplyDeleteGud boy
ReplyDeleteUyo mtoto ni HERO...hongera zake dogo
ReplyDeleteHongera jembe.
ReplyDelete