Muamuzi Kutoka Japan Ageuzwa Sababu kubwa ya Ushindi wa Brazil

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Croatia Niko Kovac, ametoa tahadhari kwa maafisa wa shirikisho la soka duniani FIFA, kuwa makini na waamuzi wanaochezesha michezo ya fainali za kombe la dunia ambazo zimeanza jana nchini Brazil.

Kovac, ametoa tahadhari hiyo kufuatia hisia kumtuma kikosi chake hakikutendewa vyema wakati wa mchezo wa ufunguzi ambao ulishuhudia wenyeji wakichomoza na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Kocha huyo ambae aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Croatia kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2008 amesema muamuzi kutoka nchini Japan Yuichi Nishimura, hakuwatendea haki kufuatia maamuzi ya kuwazawadia penati wenyeji ambayo amedai haikuwa sahihi.

Kovac mwenye umri wa miaka 42, amesema anaamini mashabiki wote duniani waliokuwa wanaufuatilia mchezo huo hawakuridhishwa na maamuzi hayo isipokuwa wachache wenye mapenzi na Brazil.

Amesema hata ukiangalia kwa mara ya pili picha za televisheni za tukio lililosababisha penati kwa wenyeji, utaona ni vipi mshambuliaji wa Brazil Frederico Chaves Guedes Fred, alivyomuahadaa muamuzi kwa kumuaminisha alisukumwa na beki wake Dejan Lovren.

Mchezo wa ufunguzi kati ya Brazil dhidi ya Croatia ulimalizika kwa wenyeji kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja ambayo yalifungwa na wachezaji chipukizi Neymar da Silva Santos Júnior aliyefunga mabao mawili pamoja na Oscar dos Santos Emboaba Júnior huku beki wa pembeni Marcelo Vieira da Silva Júnior akiwazawadia bao la kufuta machungu wageni baada ya kujifunga mwenyewe.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ya hata Mimi sikuridhishwa kabisa na mwamuz japo hata kipa wao ninamashaka nae

    ReplyDelete
  2. Tatizo kipa sio penati wewe kocha acha usenge. Marefa ni kawaida kukosea uwanjani. Goli 2 za mbali hivo angekuwa Cassilas zisingepita hizo asilani.

    ReplyDelete
  3. We anonymous wa hapo juu wa june 13, 2014 at 5:21 pm umemshuhudia cassilas wako jana alivyotambaa kama mtoto mchanga???

    ReplyDelete
  4. hahahaaa.... Cassilas ni meli ya udongo dah ile jana aibu

    ReplyDelete
  5. JE SPAIN ILIYOPIGWA 5-1 JE TUSEME REFA ALIPENDELEA UHOLANZI WASIMTISHE REFA HABEBWI MTU HAPA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad