Mwenyekiti wa baraza la maimam na muhubiri maarufu nchini Kenya Sheikh Mohammed Idris, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa.
Sheikh Mohammed Idris ameuawa karibu na msikiti ulio karibu na nyumbani kwake eneo la Likon baada ya kuvamiwa na kundi la watu waliokuwa na silaha, wakati akitoka nyumbani kuelekea msikitini.
Taarifa kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa Sheikh Mohammed Idris alikuwa akipata vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa kundi la vijana wa kiisilamu wanaodai mabadiliko, na amewahi kutoa taarifa za vitisho hivyo na kusema kuwa anahofia maisha yake.
Decemba mwaka jana Sheikh Idris na mpinzani wake Mohamed Khalifa walinusurika kifo baada ya msikiti wao kuvamiwa na vijana zaidi ya 100, ambao walitawanywa na polisi.
Mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya kumbukumbu ya Pandya, mjini Mombasa
Pamekuwa na matukio ya mara kwa mara ya mauaji ya viongozi maarufu wa dini katika mazingira ya kutatanisha.
R.I.P Sheikh Idris
Dah jamani hata watumishi wa Mungu wanauawa Je ni upendo gani huo sasa tujifunze? Ingawa ukweli siujui vizuri ila kuua sio suruhisho Bali masikilizano kaani chini enyi wakenya haaa viongozi wa dini na kundi la vijana hao na kama kuna hoja ya msingi wasikilizeni ili usuruhishi upatikane
ReplyDeleteMungu akulaze pema Peponi,yy kakutanguliza ILA na yy atakwenda hko hko.mbele yake nyuma yetu
ReplyDeleteThis is bad km tunafikia hukusasa chuki zanini.nimeckitikasana hivi ukimuua mwenzio wewe unafaidika nanini?ndio utaishi kwa furaha kwanini kupandikiza laana ambazo zita cost wewe na familia yako.manalaana yamungu itaangamiza kizazi chako tu kwanamna yoyote ile.
ReplyDeleteAliyeko nyuma ya mauaji haya mbona anajulikana. si alishatoa ruhusu kwamba 'wanaoeneza masomo ya jihad wauawe'(shoot at sight). Hao vijana(radical youths) wamepandikizwa tu ili kuchochea wazidi kuuana wenyewe kwa wenyewe.
ReplyDelete''Allahuma ghafirlahu war'ammahu saqna fil jannah Mohammed Idris''.
ReplyDeleteLaanatullah kwa wote waliohusika,yaallah wadhalilishe wote wanaoua mashekhe hapa ulimwenguni na akhera