Mwigulu Nchemba Afutilia Mbali Vikao vya Chai Serikalini "Maendelo Kwanza"

Vikao vya chai marufuku
Katika kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, Mwigulu alisema fedha zitapelekwa kwenye mambo muhimu.
ìKama hali ngumu na wananchi wanalazimika kula mlo mmoja kwa siku, walioko ofisini pia wanaweza kukosa chai ili kuwezesha mambo mengine muhimu yafanyike kwa wakati.
Tunachotaka wizara zibane matumizi tubaki na yale yenye umuhimu. Tunaomba wenzetu kwenye wizara watuunge mkono ili kuhakikisha bajeti hii inakwenda na wakati kwa maana ya mgawo wa fedha badala ya kuchelewa kama ilivyo sasa,î alisema.
Mwigulu alisema jambo lingine la nne litakalozingatiwa ni usimamizi wa fedha zinazopatikana kwani pamoja na makusanyo kidogo, lakini pia kuna uvujaji.
ìTunataka fedha inayopatikana na kupangiwa kazi fulani itumike kwa shughuli iliypokusudiwa kama. Tutahakikisha tunasimamia na kudhibiti matumizi yake,î alisema.
Alisema lengo ni kuhakikisha matumizi yaendane na thamani kwa uhalisia wa jambo
Naibu Waziri huyo wa fedha alisema eneo la tano ambalo litaangaliwa ni eneo la fedha ambazo hazitokani na kodi bali zinachangwa na wananchi na wadau wengine katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Alisema eneo hilo ni muhimu mbalo serikali inaona kuna haja ya kulisimamia vizuri ili kuhakikisha fedha za wa wananchi zinatumika vizuri.
ìKuna wakati wananchi wanachanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa zanahanati au jengo la ofisi. Wakati mwingine fedha zao zinakuwa nyingi kuliko zinazotolewa na serikali.
ìUnakuta wananchi wamejenga jengo baadae anakuja mhandisi anasema ujenzi wake haukufutwa vigezo hivyo livunjwe. Hili litaangalia haiwezekani fedha za wananchi zikapotea bure ndio maana tumeweka kipaumbele katika eneo hili,î alisema.
Alisema upotevu wa fedha ni upotevu, hivyo serikali itakuwa makini katika fedha za umma zinachangwa na wananchi katika miradi ya maendeleo.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Rudisheni kwanza bilioni 200 zetu za escrol na zile bilioni nyingine zilizopotea hazina ndio uanze kuongea uanze kuongea upuuzi wako huo.usitake kujikomba kwa watanzania na vijisenti vya chai hapa na wakati mnakwapua mabilioni ya jasho la walipa kodi wa Tanzania. muda wenu ccm na wezi wote wa serikali ya ccm unahesabika.

    ReplyDelete
  2. Jana.nilikuwa kwenye ofisi ya meneja mmoja wa TRA,kunakabati.kubwa limesheheni vyombo vya nyumbani kama hotpots,masinia,mabakuli,juice blender,thermos,sahani,vijko'uma,visu nk nk.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau.unamaanisha nini kwamba anahongwa au ameamia pale aendi nyumbani ? maana hiyo nayo.kali?

      Delete
  3. ni kweli mh. mwigulu pesa za wananchi zinaliwa bila woga.kula nao sahan imoja hao wabunge mie niko na wewe shoulder to shoulder.

    ReplyDelete
  4. wewe pumbavu ebu mwache mwigulu afanye kazi hizo billion 200 yeye hakuwepo kazini na ndo maaana anaanza kufanya mavituz.kuwa na kumbukumbu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwahiyo kama hakuwepo kazini unataka nani sasa azifuatilie?kwani wizi umetokea kwenye wizara gani?si hiyo anayoiongoza?unajua saa zingine sio lazima kucoment uharisho wako humu bilion 200 wewe mkundu unaona ni mchezo sio?mijitu kama hii sijui hata kama inajitambua kuwa yenyewe ni nani!tango pori mkubwa.

      Delete
  5. We fala nini kutokuwepo ofisini sio sababu wala utetezi,kenge ww,hapa tunataka maelezo ya kutosha na fedha zirudishwe haijalishi nani alikuwepo maadam ni serikali ile ile ya CCM. Nyambaff tuondolee ujingapa

    ReplyDelete
  6. HILI NI CHANGA LA MACHO, YEYE MWENYEWE MBONA AJASEMA AKIENDA BUNGENI KWENYE VIKAO ASILIPWE, KWA SABABU HALI NGUMU YA FEDHA? HAPA KILA MTU ANAKULA KWA UREFU WA KAMBA YAKE. YEYE MWENYEWE VIKAO AJAACHA KUSAINI! KALABAGAO

    ReplyDelete
  7. Hana lolote linawazuga tu hapa naye ni Walewale mafisadi wakuu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad