Namsubiri Kwa Hamu Maximo Yanga Afufue Vipaji Vilivyopotea

Na Baraka Mbolembole
MARCIO MAXIMO alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa muda wa miaka minne. Kuanzia, juni, 2006 hadi juni, 2010 kocha huyo raia wa Brazil alifanikiwa kusaidia, Stars kufuzu kwa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, CHAN 2009. Zaidi ya hapo alijitahidi kila awezalo kuisaidia, Stars kupiga hatua lakini mwishowe akaondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
Japokuwa alionesha dalili ya kutaka kuendelea na kazi hiyo nchini, mashabiki, wadau na baadae, TFF, walihitaji kuona mabadiliko yakifanyika kwa kuamini kuwa hakuwa na kipya na uwezo wake wa kuisogeza mbele kisoka, Tanzania ulifikia mwisho baada ya kushindwa kuisaidia, Stars kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika na michuano ya kombe la dunia, mwaka 2010..
Miaka miwili iliyopita, Mwalimu huyo alihusishwa na kujiunga na Yanga kama mbadala wa kocha, Kostadin Papic lakini nafasi hiyo ikaangukia kwa Mbelgiji, Tom Saintfiet ambaye alikuja kutimuliwa ndani ya miezi miwili kufuatia kujibizana maneno na mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji. Yanga ilimchukua kocha raia wa Uholanzi, Ernie Brandts ambaye alitimuliwa disemba mwaka jana baada ya Yanga kuchapwa magoli 3-1 na mahasimu wao Simba katika mchezo wa hisani.
Brandts aliondolewa siku chache baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili baada ya kuingoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2012/13. Yanga walimchukua, Hans Van der Pluijm na kumpatia mkataba wa muda mfupi wa miezi sita na kocha, Muholanzi tayari ameingia mkataba klabu ya Al Shoalah ya Saudi Arabia hivyo timu hiyo ipo katika mazungumzo na kocha, Maximo kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kilichopoteza ubingwa wa ligi kuu msimu uliomalizika kwa Azam FC kutwaa taji lao la kwanza.
JE, MAXIMO ATAITULIZA YANGA NA TIMUATIMU YA MAKOCHA…
Katika nchi ambayo mashabiki wa soka si wavumilivu hata pale timu inapopoteza mchezo mmoja kwa mwaka, anaweza kupata wakati mgumu. Kama mashabiki wa Yanga walikuwa sehemu ya mashabiki wa soka nchini waliotaka kuona, Mbrazil huyo akiondoshwa, Stars miaka minne iliyopita, Maximo atapambana nao klabuni. Wakati akiwa kocha wa Stars iliwahi kusema kuwa ana mapenzi na Yanga kwa kuwa huvaa jezi zenye rangi wanayoitumia timu yao ya Taifa.
Ukitoa yote hayo, kufanya kazi na viongozi, wachezaji, na mashabiki wanaotaka matokeo wakati wote wa klabu ya Yanga ni kazi nyingine inayohitaji moyo wa uvumilivu, busara na kuwa tayari kupambana na vyombo vya habari ambavyo havitaacha kuandika kuhusu mambo ya ndani ya klabu. Brandts aliondolewa japo alipoteza mchezo mmoja tu wa kimashindano. Kuifunga mara kwa mara, Simba ni kigezo ambacho kitawekwa mstali wa mbele kupima kama anaweza kufuta ‘ timua timua’ ya makocha ndani ya timu ya Yanga. Kigezo hicho kinaweza kisiwe tatizokama atakuwa ngangari na katika kuelezea sababu za kimpira  zaidi mara baada ya matokeo mabaya uwanjani
. Kama mashabiki huwa wanasema kuwa wachezaji baadhi huuza mechi wakati wa mipambano ya watani wa jadi katika soka la Tanzania, basi, makocha wa timu za Yanga na Simba wasingekuwa wanatimuliwa. Hivyo, pamoja na ubora wake wote unatajwa kuwa utaipaisha Yanga endapo akipewa kazi ya ukocha kama inavyotarajiwa, Maximo anatakiwa kujipanga kuwashinda mahasimu wao kila wanapokutana.
Wachezaji hutolewa ‘ kafara’ tu pale mambo yanapokwenda mrama kwa kuwa hakuna mchezaji yoyote aliyetiwa hatiani kwa tuhuma hizo za uuzwaji wa michezo ya Simba na Yanga. Anaweza kutumia uzoefu wake wa kuifundisha, Stars kwa miaka minne na kuisaidia, Yanga katika michuano ya kombe la shirikisho barani baadae mwaka ujao. Atakumbana na wachezaji ambao aliwatuhumu ni watovu wa nidhamu wakati akitanga kikosi cha Stars. Juma Kaseja, Athumani Idd, Kelvin Yondan ila anaweza kumaliza tofauti na nyota hao na kutengeneza timu kabambe ambayo ina wachapa kazi na wachezaji wenye vipaji vya haliya juu.
Ni mtaalamu wa kutengeneza timu katika kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza, mbinu hizo zilimfanya kuwa tishio kwa timu nyingi kubwa za Afrika  wakati zikija nchini kucheza na Stars wakati akiwa kocha mkuu wa kikosi hicho. Endapo atatua klabuni hapo itakuwa faraja kwa mshambuliaji Jerry Tegete ambaye pamoja na makali yake ya ufungaji mchezaji huyo amepoteza kujiamini na kufanya vibaya uwanjani, Maximo ndiye muibua Tegete wakati akiwa sekondari ya Makongo kwa kumuita katika kikosi cha Stars akiwa hana timu ya ligi kuu.
Atakutana na vipaji vya ufungaji kama Hamis Kizza,  Said Bahanunzi, Hussein Javu ambao wanaweza kumaliza tatizo lililomuondoa Tanzania kwa mara ya kwanza akiwa kocha wa Stars. Maximo alishuhudia Stars ikiosa magoli ya wazi  katika mechi muhimu hivyo inawezekana   kufanya kwake kazi katika klabu Brazil kwa miaka mine kunaweza kuwa kumempatia tiba ya tatizo hilo. Kama akifanikiwa kuifanya Yanga ifunge magoli bila shaka timua timua  ya makocha itapungua, ila akishindwa hakutakuwa na kitu kigeni akioneshwa mlango wa kutokea. Namsuribi kwa hamu, Marcio Maximo afufue kipaji cha Tegete na vipaji vingene vilivyosahulika ndani ya Yanga.
0714 08 43 08
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ah wapi, izo siasa zenu,,,, mbona alipokwepo taifa starz hakufufua ivo vipaji

    ReplyDelete
  2. Jerry tegete, kigi makasi, geofrey bonny, ni baadh tu . Jarbu kufatilia fatilia mpira bas hata kdogo ..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad