Nape Avuna Aibu SAUT Mwanza (Picha)

Atumia asilimia 90 ya hotuba yake kuwashambulia dr Slaa,Lissu ,CDM na UKAWA,
mkutano wake wasogezwa mbele ili kuwasubiria watu wafike uwanjani
Magari yasomba watu kutoka nje ya SAUT baada ya wanafunzi wa SAUT kutojitokeza uwanjani hapo
Awafanisha upinzani na vichaa,asema yeye alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi bora 3 waliofaulu kati ya 100 Bukumbi primary

Katibu wa itikadi na uenezi taifa wa CCM jana alijikuta anavuna aibu ya mwaka pale alipojikuta anahutubia watu waachache tofauti na gharama zilizotumika na malengo ya mkutano huo,kwani kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na uongozi wa CCM tawi la SAUT Mwanza,walisema wamemwandalia mkutano huo kwa ajili ya kuja kuongea na wasomi wa chuo kikuu cha mtakatifu Agustino (SAUT) tawi la Mwanza pamoja na kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa CCM chuoni hapo,awali mkutano huo ulikuwa uanze saa 8 kamili za mchana lakini ulilazimika kuchelewa kuanza na kusogezwa mbele mpaka saa kumi na dakika 27 jioni kutokana na kukosa watu,kwani mpaka kufikia saa 9 za mchana watu walikuwa wachache sana hali iliyowalazimu CCM SAUT kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa kuanza kuratibu zoezi la kuhamasisha watu wasombwe na magari kutoka kwenye matawi mengine yaliyoko mjini Mwanza.

Mara baada ya magari kadhaa kusomba watu,iliwalazimu pia kukodisha vikundi vya maigizo na mziki wa asili kuja kutoa burudani ili kuwavuta wananchi wafike uwanjani hapo,zoezi ambalo kimsingi nalo lilikwama kwa kushindwa kuzaa matunda hali iliyopelekea katibu huyo mwenezi wa CCM kuanza kuhutubia hivohivyo kwa watu wachache,ikumbukwe kuwa awali zilivuja taarifa ya Nape kupitia serikali ya wanafunzi chuoni hapo kuchinja ng'ombe 3 na mbuzi 10 usiku wa kuamkia siku ya mkutano huo,

Bwana Nnauye alijikuta akitumia zaidi ya asilimia 90 kuwashambulia na kuwaongelea wapinzani hasa Dr Slaa,Lissu ,CHADEMA na UKAWA,hali iliyowakera wasomi wachache waliofika mkutanoni hapo na baadhi ya raia wakazi wa maeneo jirani na chuo,wakiongea kwa masharti ya kutotajwa majina wasomi na raia hao walihoji faida ya mkutano ule kwa wanafunzi na raia wanaoishi maeneo jirani na chuo hicho kwamba hawakuona tija ya mkutano ule kwani walitegemea kma kiongozi wa chama tawala angeongelea masuala mbalimbali ya kitaluma yanayowakabili wanafunzi na mfumo wa elimu kwa ujumla,huku kukiwa na taarifa kwamba kuna baadhi ya maeneo ya chuo hicho hayana huduma ya maji takribani mwezi 1 sasa,walisema hawakwenda pale kuambiwa habari za dr Slaa wala UKAWA,bali walikwenda pale kusikiliza sera na majibu ya kero zao zinazowakabili,nao raia waliokuwa wakitoa maoni baada ya mkutano walisema walishangazwa na namna Nape alivyotumia mda mrefu kuwaongelea wapinzani huku akiacha kuzungumzia kero yao ya mda mrefu ya migogoro ya ardhi eneo la Luchelele ambapo vigogo kadhaa wa CCM na serikali wamejimilikisha mapande makubwa ya ardhi huku wakiwafukuza wakazi wazawa wa eneo hilo.

AWAFANANISHA WAPINZANI NA VICHAA

Wakati akiendelea kuhutubia,mara mara alisikika akiwaita wapinzani ni vichaa huku akiunga mkono wapinzani kunyimwa uwanja huo kufanyia mkutano wa siasa kwa madai kwamba hawana sera zaidi ya kutaka kuwaambukiza wasomia pia aliendelea kusema CCM ni chama dora wanauwezo wa kufanya lolote kwa wakati wowote huku akisema serikali yote kwa mfano ipo pale,miongoni mwa viongozi wa serikali waliokuwepo pale huku wamevaa mavazi rasmi ya chama cha Mapinduzi ,bwana Nape aliendelea kuwapolomoshea wapinzani matusi na kashfa kwa kusema "kale kababu kameshajichokea,kameshakuwa kalemavu wa mkono kapumzike ili sisi vidume tupige kazi"

VURUGU ZA ZUKA /MWANAFUNZI WA SAUT AKAMATWA

Mwanafunzi wa mwaka wa 3 anaesomea masomo ya mawasiliano ya umma chuoni hapo Nicholaus Kilunga,alijikuta akipigwa na walinzi wa CCM na wanaCCM na baadae kukamatwa na polisi kwa kosa la kumtaka Nape azungumzie ufisadi wa bilioni 200 za IPTL kupitia kwenye account ya Escro,mwanafunzi huyo alishikiliwa kwa zaidi ya saa moja hatua iliyopelekea wanachama wa CDM SAUT kuanza kukusanyika kwa wingi kushinikiza mwenzao huyo aachiwe huru kwani hakuwa na kosa lolote,dalili za kutokea vurugu mkutanoni hapo zilianza kuonekana mapema hasa pale Nape alipokuwa akimponda dr Slaa kwamba anakuja kuwadanganya watu kwa maneno ya "people's "huku wanafunzi waliokuwa mkutanoni hapo kuitikia "powerr"hali iliyowakera CCM.

KAULI YA RAIS WA SAUT YAZUA UTATA NA KUWAGAWA WANAFUNZI
Katika hatua nyingine leo chuoni hapa kumezuka sintofahamu na kuongeza hali ya uhasama na sintofahamu kufuatia kauli aliyoitoa rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho mkutanoni jana ndugu Philibert Saimo,pale alipokaribishwa awasalimie wageni na watu waliofika kwenye mkutano huo,huku akiambatana na makamu wake wa rais,waziri mkuu,spika wa bunge la wanafunzi chuoni hapo na waziri wa michezo alitamka maneno haya"Nimeamua kujiunga na CCM,kwa wale wote ambao hawataki kuongozwa na rais ambaye ni mwanachama wa CCM,wale wasio wa CCM na wale wanaoipinga CCM chuoni mjiandae kuhama chuo"kauli ambayo imezusha sintofahamu chuoni hapa hasa ikizingatiwa kwamba kiongozi wa serikali ya wanafunzi hapaswi kujihusisha na vikundi vyenye mlengo wa kidini,kikabila na kisiasa huku ibara ya 53 ya sheria zinazoongoza vyuo vikuu ikikataza siasa kufanyika vyuoni,wanafunzi wengi wameutaka uongozi wa chuo hicho umchukulie hatua kwani hakuchaguliwa na wanaCCM pekee wala kuchaguliwa awahudumie CCM pekee,wakiendelea kusema kwa wale wasiokuwa na vyama vya siasa ama wale wanafunzi wafuasi wa vyama vya upinzani hawatakuwa huru kwenda kupata huduma kwenye serikali hiyo,
Na alipotafutwa na kuhojiwa juu ya kauli yake hiyo,rais wa chuo hicho bwana Saimon alisema yeye anahaki ya kujiunga na chama chochote cha kisiasa,na kwamba pamoja yeye kuwamwanaCCM atahudumia watu wote bila kujari vyama vyao,katika mkutano huo jumla ya wanachama 2 walijiunga na CCM wakitokea CDM nao ni rais wa mwaka jana chuoni hapo bwana Dovakamwene Mcheshi na huyu rais wa sasa Philibert 
By kilunganicholaus@yahoo.com
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nnape nilidhania baada ya kupata cheo ccm ungeacha kuvuta bangi.Hauko juu ya sheria kama unavyofikiria,iko siku utadakwa na kushtakiwa.

    ReplyDelete
  2. Wewe rais wa SAUT umezungukwa na wajinga.nakupa pole na siasa changa ktk fikra zako.na huyo mwezio CDM aliitumikia mpka akapata vidond na kutobolew tumbo CCM waangalie sana hawa mathalani Mashushuu Ya CDM
    . .

    ReplyDelete
  3. kwani nape anavuta bangi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na kufirwa vile vile!

      Delete
    2. Kwani ww unaishi wapi,kuna asiyejua Nnape anabwia tangu tunasoma nae shuleni?

      Delete
    3. Marehemu baba yake alimkimbizia ulaya mashariki kusoma propaganda ili kuficha aibu baada ya kufeli shule na kumdhibiti asiivute bangi kumbe haikusaidia kitu.

      Delete
  4. Pia ni MZINZI mkubwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad