Okocha amlaumu kocha wa Nigeria

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Jay-Jay Okocha amemlaumu kocha wa timu hiyo kwa matokeo mabomu ya timu ya Nigeria iliyocheza dhidi ya Iran Jumatatu.
Timu hizo zilicheza mechi ya kwanza ya sare tasa katika michuano hiyo nchini Brazil.

"mechi hii ilipaswa kuwa ya ushindi wa Nigeria lakini hatukujitosa kimasomaso kushinda. Hatukufanya vyema , tulishindwa kabisa,'' alisema Okocha.
"Keshi hakufanya kazi ya kutosha kuanda timu. Mchezo wao haukufana hata kidogo Keshi anapaswa kuwajibika,'' aliongeza kusema Okocha
Mechi kati ya Nigeria na Iran haikuwa na msisimuko kama mechi zengina ambazo zimechezwa kufikia sasa.
Okocha, ambaye yuko kwenye kamati ya timu ya taifa ya Nigeria, alionekama kukosoa sana uamuzi wa Keshi kuhusu wachezaji walioshirikisha timu ya taifa.
Alielezea kutofurahishwa, zaidi na kocha kwa hatua yake ya kumuondoa uwanjani mchezaji wa Liverpool,Victor Moses katika kipindi cha pili, na kumbadilisha na Shola Ameobi, ambaye aliondoka Newcastle msimu huu.
"Osaze (Peter Odemwingie) alikuwa na mchezo mzuri alipoingia uwanjani na tulihitaji acheze zaidi,'' alisema mchezaji huyo wa zamani.
Jonathan Akpoborie, ambaye ni mchezaji wa zamani, pia alihisi kuwa Super Eagles walikosa mwelekeo katika mchezo wao.
''Ninaamini kuwa pia tulipoteza mweleko katika mchezo wetu na tukaanza kucheza mipira ya mbali , mchezo ambao sio kawaida yetu, '' alisema Okocha
Mechi itakayofuata katika kundi F itachezwa Jumamosi dhidi ya Bosnia-Hercegovina, walioshindwa katika mechi yao ya ufunguzi kwa mabao 2-1

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nigeria zamani si sasa wakati wa mwenyewe jj okosha,ulise,taribo west kanu,rashid yakini agahowa, amukachi hao walikuwa wababe wa mpira huko,bt sasa sioni ikienda kokote kiukweli wamekuwa wasindikizaji tu,....

    ReplyDelete
  2. Kweli kaka yani Nigeria wabovu kabisa nowadays

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad