Picha:Mwanamke Ajifungua Kiumbe cha Ajabu Mkoani Singida.

Mwanamke  mmoja  mkazi  wa  Kintinku, Wilayani  Manyoni  mkoani  Singida  amejikuta  akimwaga  machozi  baada  ya   kujifungua  mtoto  mwenye  kichwa  cha  ajabu (  tepe tepe).
Tukio  hilo  limetokea  jana  asubuhi    katika  hospitali  ya  Kintinku  Health  Center  iliyopo  Wilayani  Manyoni…..


Akiongea  na  Mpekuzi  kwa  sharti  la  kutotajwa  jina  lake  kwa  madai  kuwa  yeye  si  msemaji  wa   hospitali  hiyo, Mkunga  mmoja  wa  hospitali  hiyo  amedai  kuwa  mama  huyo  alifikishwa  hospitalini  hapo  akiwa  katika  hatua  za  mwisho   kujifungua.


“Alifikishwa  hapa  akiwa    katika  hatua  za  mwisho .  Hakuwa  na  kadi  yoyote  ya  Clinic  kwa  kuwa  hakuwahi  kuhudhuria  Clinic  tangu  abebe  mimba  hiyo.

“Pamoja  na  kutokuwa  na   kadi  ya  Clinic, tulianza  kumsaidia  kujifungua, lakini  mtoto  aliyezaliwa  alikuwa  ni  wa  tofauti  kidogo  na  alikuwa  amefariki  dunia.Kichwa  chake  kilikuwa  tepetepe  na  kimebonyea bonyea.

“Ilikuwa  ni  ngumu  kwetu  kutambua  tatizo  alilokuwa  nalo  mama  huyo  kwa  kuwa  hakuwa  na  kadi  yoyote  ya  Clinic  ambayo  ingeweza  kutusaidia  kujua  maendeleo  ya  mtoto  huyo  alipokuwa  tumboni “, alisema  Mkunga  huyo.

Mpekuzi  ilifanya  mahojiano  na  mama  huyo  ambaye  naye  alionyesha  kushangazwa  na  tukio  hilo  na  kusema  hajui  tatizo  lililomfanya  ajifungue  mtoto  huyo  kwa  kuwa  hakuwahi  kusikia  maumivu  ya  aina  yoyote  wakati  wa  ujauzito  huo  hadi  alipofikia  hatua  ya  kujifungua….

Katika  mahojiano  hayo, mama  huyo  alisema  kuwa  huo  ni  uzao  wake  wa  6  na  hajawahi  hudhuria  Clinic

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duh! Jaman iki kiumbe si pepo hili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uo ni uwezo mwenyewe sir God anafanya atakacho 2cmkufuru

      Delete
  2. Radiation poisoning!! Fukushima isnt over, its still leaking radioactive substances

    ReplyDelete
  3. Duh!!....Aiseeeeee

    ReplyDelete
  4. madhara ya abortion hayo....

    ReplyDelete
  5. mh! Jamanii!!!

    ReplyDelete
  6. watu wangu msisahau singida hasa maeneo hayo ya manyoni kuna deposit kubwa sana ya madini ya uranium so kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa huyo mama aliathiriwa na hiyo mionzi kwa namna moja au nyingine ndio ikatokea mulfunctioning ya hizo gene kwenye uumbaji wa huyo mtoto

    ReplyDelete
  7. Huyu alijar kutoa mimba ikang'ang'ania kwa kuwa hakuna historia ya makuzi ya mimba

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad