Polisi wafanikiwa kumkamata Mwanamke aliyekuwa akimtesa binti yake wa kazi kwa kumjeruhi kichwani

Polisi wamefanikiwa kumnasa mwanamke anayedaiwa kumtesa kwa kipigo na kumng’ata mtoto Merina Mathayo (15), kumsababishia majeraha makubwa kichwani.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura akizungumza na Mwananchi jana alisema walifanikiwa kumnasa juzi, mwanamke huyo akiwa mafichoni Mbagala wilayani Temeke.
“Tumefanikiwa kumnasa juzi usiku akiwa mafichoni kwa jamaa zake, ni mwanasheria wa kujitegemea ana umri wa miaka 44, lakini inashangaza kwa hayo aliyoyatenda, anaendelea kuhojiwa wiki ijayo tunatarajia kumpandisha kizimbani,” alisema Wambura.

Mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Boko, anadaiwa kumtesa mtoto huyo ambaye ni mtumishi wake wa kazi za nyumbani, ambaye sasa amelazwa katika wodi ya dharura ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI) Muhimbili Dar es Salaam.
Wakati huo huo, Uongozi wa MOI umejizatiti kulinda usalama wa mtoto huyo, kwa kuzuia vyakula kutoka nje ya taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kudhibiti watu kumtembelea na kuzungumza naye.
Mmoja wa wauguzi katika wodi aliyolazwa alieleza mtoto huyo kwa sasa anahudumiwa kila kitu na taasisi hiyo.
Ofisa Uhusiano wa MOI, Patric Mvungi , alieleza kwamba majibu ya kipimo kikubwa cha CT Scan alichofanyiwa yametoka, ambapo yameonyesha hakuna mfupa uliovunjika kichwani.
Mtoto Merina amelazwa Moi baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Mwananyamala alipokuwa amelazwa awali, kutokana na majeraha hayo ya kung’atwa meno na kupigwa na vitu mbalimbali.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uyo shetanu aliefanya unyama huu apewe adhabu kali kabisa, mxuuu!!

    ReplyDelete
  2. Jaman hivi huwa mnakumbuka kama kuna mungu,siku ya mwisho no Julia name kusaga meno,hao in binadamu kama sisi,kama humemshindwa si humrudishe kwao,Huu unyama umfanyiao mtoto wa mwenzio fikiria kama ungekuwa wewe,hii dunia tu,kumbukeni kuna MOTO,sisi Dada yetu was nyumbani tunakula nae mezani,analala pazuri,nguo,kila hitaji la binadamu linalohitajika anapata,mpaka birthday tunamfanyia kama watoto wengine, Huo ndio upendo Mungu hanaohuitaji,

    ReplyDelete
  3. hivi hawa wamama mbona wamekuwa na roho mbaya hivi. hawo wanaofanyia wenzao hivyo hawajui uchungu wa kuzaa hawo ndio wale wanaotumbukiza vichanga choon. laana tuli lah.

    ReplyDelete
  4. sasa tunakoelekea jaman sio kuzur hiv wanawake tumekua naroho mbaya sana wallah sijui tatzo nn hbu fikilia mtu anakufanyia kazi zako tena ukifikilia umri wake mdgo mm nilivyomvivu namuheshim sana mtu anaenifanyia kazi sijui kama nahapo ukute kuna kesi nying zakuwatesa wafanyakzi wandani

    ReplyDelete
  5. Nasikia afunguagi mlango na hakuna jirani hata mmoja anaywkwenda kwake wahaya wote wamerahani kitendo Hicho.mwanasheria gani huyo feki kabisa..

    ReplyDelete
  6. Kuna watu wana roho mbayaaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad